CUF Bukoba watinga bungeni

CUF Bukoba watinga bungeni

Kiranja

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2007
Posts
751
Reaction score
336
Viongozi wa CUF Bukoba watinga bungeni. Spika awatambulisha. Je, hii ni sehemu ya mkakati wa kumkabili Lwakatare?
 
Viongozi wa CUF Bukoba watinga bungeni. Spika awatambulisha. Je, hii ni sehemu ya mkakati wa kumkabili Lwakatare?

Lwakatare atakabiliwa kule kule Bukoba na si Bungeni .Kwanza Bunge ni la wote bila ya kujali vyama .Sema kutambulishwa ni new twist kwa CUF maana hii ni tabia ya CCM sasa na CUF wameanza kuimba wimbo huo sawa ni haki yao .Kuna kampeni kule Dodoma jumba la baridi au sijaelewa ulitaka kutueleza nini ?
 
Waswahili wanasema ujanja kuwahi. CUF wanakumbuka shuka wakati kumesha kucha? CUF Tanzania Bara ilijikita katika MUAFAKA na CCM ikasahau kwamba Tanzania Bara Muafaka sio issue. Ikasahau kwamba suala la Ufisadi na Umasikini ni mambo muhimu kwa watu wa Bara. Matokeo yake Chadema imechukua nafasi Muhimu hasa baada ya Kampeni ya Operesheni Sangara. Kwa CUF kuanzisha Operesheni Zinduka wakati huu ni sawa na kukimbizana na mkia wa Mbwa! Bila Rwakatare CUF is as good as dead in Bukoba.
 
Huyo Katare alikuwepo katika kampeni B/muro na mbona sisieeemu wakavuna ushindi?Nenda muendako hawa jamaa ndio waongoza nchi tuu mtabaki kutosaini daftari ya matokeo halafu ndio nini?!
 
Hii misafara ya wanasiasa na Wapambe kushindana kwenda bungeni Dodoma inanitia kichefu chefu. Hawa watu wanafanya kazi saa ngapi?

Huenda kuna maskini huko wilayani anasubiri huduma zao na kila siku anaambiwa njoo kesho, mheshimiwa hayupo.

Tunahitaji mabadiliko makubwa TZ; mabadiliko ya fikra na matendo.
 
Ni kawaida hiyo hapo bungeni,huwepo na wageni waalikwa natumai hii hata mbunge akitaka kumpeleka mwanawe basi anaruhusika kwa kufuata taratibu na Soika atawajibika kumtambulisha.
Naona mna mchecheto hata mambu bado ,kwani Chadema mtamsimamisha Lwakatare kugombea ubunge ???
 
Ni kweli kabisa tunahitaji mapinduzi ya kifikra na kimatendo, tusikubari mawazo yao wala kujikomba kwao....CCM sasa wamejikita kwenye kununua shada za wapiga kura na kuwanunua wasimamizi wa upigaji kura.
Kinachoendele Dom ni mikutano ya kibiashara tu..
Wamejikita kwenye ufisadi wakusanye pesa za kuwapa ushindi.
Inatia kichefu chefu.
 
Huyo Katare alikuwepo katika kampeni B/muro na mbona sisieeemu wakavuna ushindi?Nenda muendako hawa jamaa ndio waongoza nchi tuu mtabaki kutosaini daftari ya matokeo halafu ndio nini?!

Majibu ya jazba yanakushushia mtu hadhi na mleta mada hii nadhani hakuiweka vyema maana CUF Bukomba kuwepo bungeni ni haki sema style ya kutangazwa kwamba wapo ndiyo inazua maswali .Mimi nimesha fika Dodoma pale Bungeni mara 4 kwa kuonana na waheshimiwa wa CCM na Chadema lakini sikuwahi kusema niombe wala kuwaza kutangazwa kwamba nimekuja kwa ajili mtu fulani .Mtizamo tu huo na sijaona faida yake .Mle mjenoni nimekaa sana na mara kibao lakini hata kujulikana niko mjengoni sijawahi kutaka .

Mleta mada alitakuwa ku save muda wetu tujadili hoja za maana hii si hoja .

Kusema CUF ndiyo cha kiongozi nakubali kwamba ni Chama kiongozi Visiwani lakini Bara CUF hailkubaliki hata mara moja .Kukandia kwamba Chadema wanakataa usaini daftari ni ujinga huu maana hata CUF hawajawahi kusaini walipo ibiwa na kupiorwa ushindi na hata leo wanalia na muafaka .

Jamani fikirieni acheni jazba .

Lazima tukubali kwamba Bara Chama pekee ni Chadema na CC na Visiwani ni CUF na CCM .
 
Huyo Katare alikuwepo katika kampeni B/muro na mbona sisieeemu wakavuna ushindi?Nenda muendako hawa jamaa ndio waongoza nchi tuu mtabaki kutosaini daftari ya matokeo halafu ndio nini?!

Kazi ya CCM ni kubaka ushindi wa wengine, na kujitangazia ,wameisha kama mchuuzi wa makongoro hawana hadhi kabisa , even among themselves ni majungu kulalamikiana tuu , kushitakiana wako total confused siku za enda mbio mwisho wao waja
 
Kile ni chuma cha moto...hao vijana ni sawa na DEBE SHINDA....na daima MBIO ZA SAKAFUNI....., tu usubiri mwisho wa mziki wenyewe.
 
Amosam naamini kuna siku utaujua ukweli, labda nawe kama ni kama wao. Hata hivyo wewe si mmoja wao kwani ,hawamo humu.
Pole ,hata kama hukuona yaliyotokea bmlo, na bado unafikiri miaka ya 95.
 
hiyo ni njaa tu inawasumbua si unajua tena uchaguzi umekaribi wale waliozoea kuisha kwa kutegemea si hasa ndio wakati wao huu.Mageuzi ya kweli yatatokea pale wananchi wote kwa pamoja watakapoacha unafiki na kutanguliza maslahi ya nchi mbele na sio maslahi binafsi.
 
Lwakatare atakabiliwa kule kule Bukoba na si Bungeni .Kwanza Bunge ni la wote bila ya kujali vyama .Sema kutambulishwa ni new twist kwa CUF maana hii ni tabia ya CCM sasa na CUF wameanza kuimba wimbo huo sawa ni haki yao .Kuna kampeni kule Dodoma jumba la baridi au sijaelewa ulitaka kutueleza nini ?

Juzi Mwenyekiti wako Freeman Mbowe alitambulishwa bungeni na Spika akiwa ni mgeni wa Dr Slaa. Je Chadema na wanaiga tabaia ya CCM?

Exuper Kachenje na Leon Bahati

MKUTANO wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma umechukua sura mpya, ukionyesha wabunge kutuumia kama jukwaa la kampeni na pia sehemu ya kuundia mikakati ya kisiasa ya kujenga mazingira mazuri ya kushinda katika uchaguzi mkuu ujao, Mwananchi Jumapili limebaini.

Tangu kuanza kwa mkutano wa 16 wa Bunge la Bajeti Juni mwaka huu, idadi kubwa ya wageni waliotembelea wabunge mjini humo, wamekuwa wakibeba taswira ya kisiasa zaidi hali inayodhihirisha kampeni za chinichini kuingia bungeni huku wabunge wakitumia nafasi hiyo kujiosha kwa wapiga kura wao majimboni.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo ya kisiasa, waliliambia gazeti hili kwamba wanachofanya wabunge kinaelekea kuwa ni kuwavuta karibu wale watu mashuhuri majimboni mwao, ambao wana nafasi nzuri ya kuweza kufanikisha malengo yao ya kisiasa.

Kila baada ya kipindi cha maswali na majibu Spika wa Bunge, Samweli Sitta, hutangaza wageni wanaowatembelea wabunge na uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wageni wengi ni wale wanaotegemewa kwenye malengo ya kujiimarisha kisiasa kwa wabunge.

Wabunge wa CCM ndiyo wanaotia fora kwa kuwa na wageni hao, ambao mara nyingi ni wale wanaohusika katika vikao vya maamuzi na wale wenye uwezo mkubwa wa kufanya kampeni.

Wageni hao ni kama vile makatibu na wenyeviti wa CCM ngazi za tawi, kata, wilaya na mkoa, viongozi mbalimbali wa jumuiya za chama, madiwani, wasanii, wafanyabiashara na wanafunzi wa vyuo na sekondari.

Wageni hao wanapofika Dodoma, hupata fursa ya kufanya vikao visivyo rasmi na wenyeji hao kwa ajili ya kupanga mikakati mbalimbali ya kisiasa.

Spika wa Bunge Samuel Sitta, hakuficha ukweli wa wageni wake waliomtembelea Alhamisi iliyopita, kwa kuthibitisha kuwa huyo ndiyo nafasi yake ya kujidhihirisha kisiasa.

Huku akitamba, Spika Sitta alitambulisha wageni wake wajumbe wa Kamati ya Siasa jimboni kwake Urambo Mashariki, akiwaelezea kuwa bila ya wao hawezi kufanya chochote.

Huku akitambulisha uongozi wa kamati hiyo kwa majina, alieleza kuwa kamati hiyo ndiyo inayomshauri na kuwa iwapo kuna mbunge hajawa na kamati kama hiyo basi ni wakati muafaka wa kuunda kamati hiyo.

``...Waheshimiwa nimechukua muda mrefu, kuwatambulisha hawa kwa sababu hili ndiyo jukwaa langu na huu ndiyo wakati muafaka. Waheshimiwa wabunge kama huna kamati ya kukushauri unda haraka, huu ndio wakati muafaka,`` alisema Spika Sitta.

Awali kabla ya kutambulisha wageni wake hao, Spika Sitta alitambulisha wageni wa wabunge mbalimbali pamoja na wageni aliowataja kuwa ni wa Shelukindo bila kufafanua yupi, mwenye wageni hao kati ya Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo na Mbunge wa Kilindi Beatrice Shelukindo.

Pamoja na wageni hao Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alitambulishwa kuwa mmoja wa wageni waliokuwepo bungeni jana, akiwa mgeni wa Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa.

Pamoja na wageni hao wa Shelukindo, Spika pia alitambulisha wageni wanne wa Kapteni John Chiligati mbunge wa Manyoni Mashariki ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), idara ya Uenezi, ambao wametoka Jimbo la Biharamulo Magharibi lililofanya uchaguzi wake wiki iliyopita na mgombea wa CCM, Oscar Mukasa kuibuka mshindi.

Hata hivyo, hali hiyo iliendelea katika vikao vya siku iliyofuata ambapo katika kikao cha Ijumaa asubuhi Spika Sitta alitambulisha wageni wa Mbunge mpya wa Jimbo la Biharamulo Magharibi (CCM) Oscra Mukasa aliyeapishwa Ijumaa asubuhi, aliowataja kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Buhie, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Biharamulo na Katibu wake.

Vilevile, katika kikao hicho cha Ijumaa Spika alitambulisha wageni wa James Lembeni ambaye ni Mbunge wa Kahama aliyetembelewa na Katibu wa CCM Wilaya, Mwenyekiti wa CCM Kata pamoja na Kada wa chama hicho mmoja huku Mbunge wa Rombo Basil Mramba akitembelewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Anthony Tesha.

Baadhi ya wageni wengine ambao waliwahi kutambulishwa bungeni katika vikao vilivyopita ni wa Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu ambaye alitembelewa na kamati ya wapangaji wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) walioongozwa na Mzee Gwao pamoja na Mchungaji Christopher Mtikila wa chama cha siasa cha DP.

Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, alitembelewa na ambao ni wenyeviti na makatibu wa Kata wa CCM, wakiongozwa na Katibu wa Siasa na Uenezi, Wilaya ya Moshi Vijijini, Hussein Jamal.

Anna Abdallah (Viti maalumu-CCM), alitembelewa na wasanii wapatao 20 wa Kikundi cha Curser Film Production kilichokuwa kikiongozwa na viongozi watano; Mlezi wa Kikundi Mwanate Abdallah, Kiongozi wa Kikundi Charles Magari, Mwongozaji wa Filamu Bahati Tundu, Mkurugenzi wa Kikundi Hussein Mwala, na Katibu wa Kikundi Kuruthum Juma.

Dk Haji Mwita (Muyuni-CCM) Haji alitembelewa na viongozi wa CCM jimboni kwake ambao ni Katibu mwenezi, Ali Miraji Hassan, Katibu Fedha na Uchumi, Makame Mwadini Makame, Katibu wa Kata Wazazi Kibigija Juma, Mwenyekiti wa CCM, Tawi la Jozani Chumu.

James Lembeli (Kahama,CCM) alitembelewa na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Kahama, Jumanne Mayunga, diwani wa kata Kahama Mjini, Furaha Kagoro, diwani wa Kata ya Nyandekwa Hassan Mponya, mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata ya Ulowa Robert Mdula.
William Shellukindo (Bumbuli,CCM) alitembelewa na Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Lushoto, Paul Twakyondo na wakati huo huo, Zungu naye akatembelewa na wanafunzi 25 kutoka Sekondari ya Azania ya jijini Dar es Salaam wakiongozwa na mwalimu Abdul Mohamed pamoja na Katibu CCM Kata ya Upanga, Khamis Kundya.
 
Juzi Mwenyekiti wako Freeman Mbowe alitambulishwa bungeni na Spika akiwa ni mgeni wa Dr Slaa. Je Chadema na wanaiga tabaia ya CCM?
Mkuu Masatu,

Kwa kuwakamata wanafiki na wewe ni bingwa. Lunyungu anaimba tu ya CCM, haoni ya CHADEMA, kawa kipofu!
 
Huyo Katare alikuwepo katika kampeni B/muro na mbona sisieeemu wakavuna ushindi?Nenda muendako hawa jamaa ndio waongoza nchi tuu mtabaki kutosaini daftari ya matokeo halafu ndio nini?!
wacha weee wakavuna ushindi kwa kura zinazosemekana za wizi.Kazi ipo! hapa najua mkuu kibunango atanishukia tu
 
Ni kawaida hiyo hapo bungeni,huwepo na wageni waalikwa natumai hii hata mbunge akitaka kumpeleka mwanawe basi anaruhusika kwa kufuata taratibu na Soika atawajibika kumtambulisha.
Naona mna mchecheto hata mambu bado ,kwani Chadema mtamsimamisha Lwakatare kugombea ubunge ???

Mwiba.
Mgombea ubunge kwa CUF huko Mbeya vijijini amenunuliwa na Chadema juzi,jee unasema Ndugu Mwiba?
 
juzi mwenyekiti wako freeman mbowe alitambulishwa bungeni na spika akiwa ni mgeni wa dr slaa. Je chadema na wanaiga tabaia ya ccm?

hii sikuiona mkuu wangu.umekuwa kama field masrshal es na kumkoma nyani giradi?
 
Mkuu Masatu,
Kwa kuwakamata wanafiki na wewe ni bingwa. Lunyungu anaimba tu ya CCM, haoni ya CHADEMA, kawa kipofu!

Mkuu Mtanzania kweli unadiriki kumwita Lunyungu mnafiki ? Ndiyo lugha kweli za hapa kwa wanao heshimiana ?
 
Mkuu Mtanzania kweli unadiriki kumwita Lunyungu mnafiki ? Ndiyo lugha kweli za hapa kwa wanao heshimiana ?
Mkuu,

Kwa JF ukiwa mnafika utaitwa mnafiki; tunamkoma nyani giladi mchana kweupe. Hakuna urafiki wala kuheshimiana, JF where we dare to speak openly bila kuambiwa huyu si mwenzetu. Najua Lunyungu hatanyima soda tukionana.
 
Back
Top Bottom