PROFESA LIPUMBA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS: Tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi wapinzani wamekuwa wakisimamisha wagombea wale wale tu. Hii desturi ya kujaribu jaribu itaisha lini? Hivi huko kwenye vyama vya upinzanii hakuna wengine wenye sifa ya kubadili japo vionjo?
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba akichukua fomu za kugombea nafasi ya Urais kutoka kwa Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Kinondonio, Mh. Kassim Chogamawano katika ofisi za CUF wilaya ya Temeke jijini Dar leo.
Kikwete akichukua fomu CCM unaweza kuuliza kwani hakuna mwingine? Kila Chama kina katiba na utaratinu wake wa kupata wagombea, na sidhani kama Lipumba hata kama ni mwenyekiti anauwezo wa kujiteua kugombea urais kwa niaba ya CUF, na sidhani kama wana CUF hawajui kama wengine wapo. Naamini kuwa wao kuamua kumpa fomu Lipumba ajaribu kugombea si wajinga, wanafahamu wanachofanya ndio demokrasia yenyewe.
hawaitaji kumpromote mtu mwingine mpaka mwnyekiti atakapo maliza muda wake madarakani?
Mkuu mbona kwa CUF mambo 'ize tu' mwanachama yoyote hakuzuiliwa wala "...hatokufa" kama anataka kupambana na Maalim Seif au Prof.Lipumba kila mtu yupo huru, muhimu kufuata taratibu tu.
Yes I agree. But Lipumba ni kupoteza muda. Bora angesimama hata Seif Sharif Hamad kwa Urais wa Jamhuri ya muungano. Lipumba hata akiteuliwa kugombea uenyekiti wa kijiji chake cha ilulangulu-Tabora hachaguliki.
Kwa miaka 15 tangu aanze kugombea upresidaa, sikumbuki CUF kuwa na wabunge wa kuchaguliwa kutoka bara zaidi ya Rwakatare aliyekuwa mbunge bukoba vijijini 2000-2005.
He is absolutely of no use. Ana cripple CUF
Kwani Lipumba kuchukua form ina maana wengine hawaruhusiwi?. Mbona anatekeleza haki yake kikatiba?. Tatizo ni kwamba the more he stays in the race the more popular he is na hicho ndicho kinawatisha critics. Mwache Prof atumie haki yake, kwani at the end ni wanachama wa CUF ndiyo watakuwa na haki ya kusema ni nani wanamuona anafaa kuwakilisha chama chao uchaguzi mkuu, whether Lipumba su somebody else.