Uchaguzi 2020 CUF hakuna watia nia?

Uchaguzi 2020 CUF hakuna watia nia?

AVRAM

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
616
Reaction score
885
Habari zenu waungwana.

Naomba kuulizia kuhusu watia nia wa Chama cha Wananchi CUF. Sijasikia taarifa yoyote kutoka katika vyombo vya habari kuhusu wachukua fomu za Urais, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani au mara hii CUF imeamua kuunga mkono juhudi za Chama chengine. Kama ndivyo kwa nini wasitoe taarifa angalau sisi wananchi tukaelewa msimamo wa chama kitaifa.

Nimesikia taarifa nyingi kutoka kwa vya tofauti kuhusu watia nia wao kwa ngazi zote ila sio CUF. ACT, CCM, CHADEMA, CHAUMA, NCCR, TLP na vyenginevyo ila CUF sijapata kuisikia au ni mimi ndio sijasikia taarifa za watia nia wa CUF. Kama kuna taarifa zozote za watia nia kuhusu chama cha wananchi CUF tujuzane waungwana.

Ahsante
Natangukiza Shukran kwa wale waungwana watakao amua kuweka taarifa kuhusu watia nia wa CUF.
 
Nimesikia taarifa nyingi kutoka kwa vya tofauti kuhusu watia nia wao kwa ngazi zote ila sio CUF. ACT, CCM, CHADEMA, CHAUMA, NCCR, TLP na vyenginevyo ila CUF sijapata kuisikia
Chauma pia umesikia? Ya kweli haya?
 
Lipumba hana cha kuongea baada ya kuachwa kwenye mataa na Sharif Hamadi,maccm yamemtelekeza,labda tusubili msajili wa vyama anaweza kumuingizia tena fedha kwenye akaunt binafsi.
 
Hashim Rungwe ameshachukua fomu ya urais muda sasa anasubiri mapambano tuu
 
Kwanini unamkubali mkuu?
Sababu anaongeaga vitu vizito kwa lugha nyepesi ambavyo wenye akili ndogo hawamwelewi. Anazungumzia welfare state matters ambazo zimezifanikisha Scandinavian countries kufika mafanikio ya kimaisha katika lugha complex kidogo na wachache saana tunamwelewa.

He is simply a legend who makes a lot of senses to the geniuses only.
 
Habari zenu waungwana.

Naomba kuulizia kuhusu watia nia wa Chama cha Wananchi CUF. Sijasikia taarifa yoyote kutoka katika vyombo vya habari kuhusu wachukua fomu za Urais, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani au mara hii CUF imeamua kuunga mkono juhudi za Chama chengine. Kama ndivyo kwa nini wasitoe taarifa angalau sisi wananchi tukaelewa msimamo wa chama kitaifa.

Nimesikia taarifa nyingi kutoka kwa vya tofauti kuhusu watia nia wao kwa ngazi zote ila sio CUF. ACT, CCM, CHADEMA, CHAUMA, NCCR, TLP na vyenginevyo ila CUF sijapata kuisikia au ni mimi ndio sijasikia taarifa za watia nia wa CUF. Kama kuna taarifa zozote za watia nia kuhusu chama cha wananchi CUF tujuzane waungwana.

Ahsante
Natangukiza Shukran kwa wale waungwana watakao amua kuweka taarifa kuhusu watia nia wa CUF.
Wana wasubiri wenzao CCM waungane kwenye kampeni
 
Back
Top Bottom