CUF kuandamana nchi nzima

Ah Ndugu yangu Bwana. Mkataba gani uliokubaliwa. Kamati ya Muafaka ni kama Kamati ya Wataalmu iliyofanya "spade work" kutayarisha hayo mambo. Wewe unayaita Mkataba , umekubaliwa wapi, umetiwa saini wapi. CUF wamepeleka kikao cha juu -kimekubali, sawa. Huo ni upande wake. CCM nao wamepelka kikao cha juu (Halmshauri), haikukataa, lakini imeona kuna mapendekezo (ya kuboreshwa) inafaa yafanywe. Kosa liko wapi? Kuwa mtulivu, na pitia vizuri hayo mambo uyafahamu, kuliko kuweka mbele kulaumu tu.Kuhusu maoni ya Muungano ni jambojengine hilo subject to discussion wakati unapowadia.
 
Wakati hii process ya majadiliano ya muafaka ikiendelea kwa miezi 14, je ccm walilijua hili au wamekumbuka leo hii baada ya kuona kuwa kuna miaka mingine miwili wanaweza kuzungushana na CUF kwenye hili hadi ifike 2010?
Tatizo watu wengi wamedandia mambo!!! huu ni muafaka wa nne... na CCM wamesema hivii, tangu 1957 kila baada ya uchaguzi kulikuwa kunatokea hali za kutoaminiana na hivyo kuwa na process za miafaka... ndio maana wa sasa ni wanne (4)...

This time wakasema ni vyema waende taratibu lakini watafute suluhisho la mwisho sasa wewe wasema miezi 14 ni mingi... je miezi hiyo ni mingi zaidi ya miaka ya 50 ya wasiwasi na miafaka isiyoisha?.

Kumbuka kwamba hili wazo la kura ya maoni limekuja baada ya makubaliano ya kuwa na serikali ya mseto... kwa mwenye akili timamu anaelewa wazi kwamba wazo la utekelezaji lisingekuja kabla ya makubaliano...


Kama bunge linawakilisha wananchi na kama ulivyosema kuwa yote yaliyopita bunge lilishirikishwa, hili la serikali ya pamoja lina tofauti gani na mengine yaliyopita ikiwemo muungano?

Nimekueleza demokrasia kila mwaka zinakuwa... na sasa utawala bora ni jambo ambalo linatamkwa miaka ya 1977 wakati wa katiba yetu haikuwa kitu muhimu... sasa kama unasema tufanya kama mwaka 1977 then... you must be kidding
 

Mwafrika,
Hayo yote yanajadilika katika kamati ya muafaka. Lini hiyo kura ya maoni itapigwa au serikali shirikishi itaundwa yanajadilika katika mezani, hakuna kisichowezekana kama kweli nia ipo ya kufanya maamuzi yatakayolenga kuwanufaisha wananchi wa Unguja na Pemba na wala siyo viongozi au makundi fulani.
 

Mh. nakubaliana nawe kabisa. Unajua CUF wana vijana wazuri tu wasomi na mahiri, na kama umefika Zanzibar wale wafuasi wao ni miongoni wa wale waliosoma sana na wenye nafasi nyingi za utendaji(maofisa Watendaji katika vyombo vya Serikali). Lakini uongozi wake wa juu uko shghla baghla (naamini si kiuwezo au umahiri)- sijui kuna shetani gani pale.
 
My take;

Kama kweli nchi hii ingekuwa na waandishi wa habari wanaoandika mambo kwa uwazi bila ushabiki... hakika suala la CCM kule Butiama lingekuwa jambo la ku-pongezwa badala ya jambo la kulaumiwa, kubezwa.

Kwa hakika CUF inatumia advertage ya vyombo vya habari kupotosha... na wakati huo huo ujinga wa wananchi wetu kuchambua mambo... binafsi sijui wanaandamana kwa sababu ipi? Tena kwenye chama hicho kina-professa....


Moja; Walivunja MOU ya kutosema jambo walilokubalina mpaka makatibu wakuu wote wafanya joint press conference... CUF ikafanya tofauti.

Mbili: Wamelipuka kujibu hoja za CCM kabla ya Kuzipata au hata kuzijua.

Tatu: Barua waliyoandikiwa na CCM ni ya kurudi mezani; wao wanarudi mitaani.... Chama gani hiki? Yet Watanzania wanaJF wanawaunga mkono watu ambao nia yao ni kuingia madarakani kwa namna yoyote ile....

Nne: I think wanataka kurudisha popularity yao ambayo iko karibu kuondoka... lakini wafahamu kwanza Watanzania hawasemi hawapigi makelele... kazi yao ni wanawaadhibu wasanii kwenye kura tu.

Tano: Chama kilichoko mbele kutetea demokrasi na haki sawa kwa wote, leo hii wanakaa wananchi wakishirikishwa kwenye maamuzi makubwa.

Sita: Hivi si chama hiki hiki kinaitwa CUF kilichosema miaka yote kilikuwa kinashinda kilikuwa tu kinapokonywa ushindi... sasa kwa kuwa hoja za Daftari la Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi zitakuwa zimekubaliwa na kufanya kazi... si ndio hiyo kura ya maoni watashinda kwa kishindo? sasa wanakataa nini?

Saba: Kwa kuwa vyama vyote CCM na CUF vimekubali serikali ya Mseto... si ndio iko wazi kabisa kwamba zaidi ya 75% ya Wazanzibar watapenda serikali ya Mseto... kwani hata sasa wanaokataa si wale walioko madarakani tu... mtu ambaye hayuko madarakani kwake serikali ya mseto... italeta utulivu siasa hivyo ataikubali hiyo.
 

CUF Ni wachochezi na wanafiki wakubwa wao siku zote hotuba zao huenda na neno hilo hapo jeusi.

CUF ni wanafiki wakubwa hadi leo CUF zanzibar hawamtambui Karume ya kwamba ni mwizi aliwaibia kura leo hii wanataka ushirikiano na mwizi .Hivi unaweza shirikiana na mwizi kuleta maendeleo?? Ama Mtu akikuibia kitu muafaka wake unamlilia huyo mwizi aliyekuibia mgawane hicho alichokuibia??? huu sio unafiki kweli

Hivi hiyo LULU ya CUF wanayotutangazia kila siku ndio wameamua kuichanganya na nguruwe??
 
Ahsante. sasa Mheshimiwa umeuona upande wa pili wa shilingi. Lakini iangalie vizuri CUF. wanachama wake ni safi kabisa. Vijana wake safi kabisa. Wataalamun pale -ni safi kabisa. Lengo lao is justifiable. Ukizungumza na wenyewe wanachama huko chini Wanataka equality -haki yao, wanataka maisha bora ni sawa, kila kilichopo Unguja na Pemba kiwepo sawa (Ah hata huko Bw. Wa Welsh si wanataka kila kitu nao kiwepo Cardiff kwenye Capital yao)Lakini viongozi wanapigania ku-reverse hali. Wawaondoe watawala CCM watawale wao. Wawaondoe wanaoonea sasa hivi ili wapate kuonea wao, wanaoiba sasa hivi ili wapate kuiba wao.wanaodhulumu sasa hivi sasa ili wadhulumu wao. Hao bwana ni shaghla baghla.
 

kwani dar es salama ni sawa na kigoma ,mbeya ni sawa na kigoma,arusha ni sawa na Siginda ??Kama hawajitumi wanafikiri maendeleo Maalim atawapelekea ,Wafanye kazi wajitume na wajenge shule zao nzuri na mambo mengine ya maendeleo captal yao itazidi hata hiyo ya unguja.
 

Kama hakuna kilichokubaliwa, then kinachoengelewa hapa ni nini?
 

Bado hujaeleza kuwa kinachoengelewa sasa hivi kina tofauti gani na hiyo miafaka minne iliyopita?

Kumbuka kwamba hili wazo la kura ya maoni limekuja baada ya makubaliano ya kuwa na serikali ya mseto... kwa mwenye akili timamu anaelewa wazi kwamba wazo la utekelezaji lisingekuja kabla ya makubaliano...

Makubaliano yepi unayoongelea hapa?




Nimekueleza demokrasia kila mwaka zinakuwa... na sasa utawala bora ni jambo ambalo linatamkwa miaka ya 1977 wakati wa katiba yetu haikuwa kitu muhimu... sasa kama unasema tufanya kama mwaka 1977 then... you must be kidding

Bado sijaelewa hii spinning ya kurusha miaka inaelezea nini kitendo cha ccm cha kuzungusha makubaliano ya amani ya zanzibar kuanzia mwaka 1995 hadi leo.

Kinachoshangaza zaidi hapa ni usahaulifu kuwa CCM wameua watu wengi huko zanzibar kila baada ya uchaguzi na sasa hii standard ya juu ya kujiona kuwa wataka amani imetoka wapi?
 

Majadiliano yapi unayosema hapa wakati CCM wamekataa meza ya majadiliano na wanataka kura ya maoni?
 

Viongozi na vijana gani wasomi unaongelea hapa? Wale waliofukuzwa kazi toka serikalini na Komandoo baada ya uchaguzi wa mwaka 1995?
 
Kesho au leo kwa wengine ni siku ya Karume...

Ni nini mtazamo wa Karume ktk Pemba?
 

Kasheshe,

Wanaojaribu kutumia vyombo vya habari ni nyie wanaccm na wenzako hapa kina pundamilia. CUF ina chombo gani cha habari? Hii spin ya kuwa victim CCM mmeianza lini?


Moja; Walivunja MOU ya kutosema jambo walilokubalina mpaka makatibu wakuu wote wafanya joint press conference... CUF ikafanya tofauti.

Mbili: Wamelipuka kujibu hoja za CCM kabla ya Kuzipata au hata kuzijua.

Wewe ni msaidizi wa Makamba nini? hiyo MOU wewe umeipata wapi? Iweke hapa ili tuhakikishe kuwa CUF hawakutakiwa kusema chochote kuhusu Muafaka.

Ninachoelewa mimi, CUF walifanya Baraza la chama na wakapitisha makubaliano ya kukubaliana na kamati ya muafaka ili kuunda serikali ya mseto. BBC na vyombo vingine vya habari wakaripoti kile kilichojadiliwa kwenye kikao cha CUF kama vile wanavyoripoti yaliyotokea Butiama kwa CCM


Sasa hapa unajichanganya, mara unasema kuwa CCM wanataka CUF warudi kwenye meza ya maelewano, mara unasema unataka ipigwe kura ya maoni. Unachotaka ni nini?


Unataka kuanzisha ubishi kuwa CUF haikushinda uchaguzi Zanzibar? kama CCM mnaamini kuwa CUF hawakushinda, makubaliano na kura za maoni ni ya nini?


Kasheshe,

Kubali kuwa Kikwete kama kawaida yake ya kuchemsha amekosea kwa kuingia kichwa kichwa katika suala la Zanzibar wakati anajua kabisa kuwa chama chake na wababuzi huko zanzibar kina Karume hawataki amani na wenzao wa Pemba...

Endeleeni kuleta siasa kwenye mambo muhimu ya nchi. Yetu sisi ni macho na masikio tu.
 
Kesho au leo kwa wengine ni siku ya Karume...

Ni nini mtazamo wa Karume ktk Pemba?

Kuna report kuwa Karume alisema Butiama kuwa hakuna Mpemba atatawala Zanzibar wakati yeye akiwa hai..... haya mengine atakayosema hapa ni marudio tu!
 
Kuna report kuwa Karume alisema Butiama kuwa hakuna Mpemba atatawala Zanzibar wakati yeye akiwa hai..... haya mengine atakayosema hapa ni marudio tu!

duh! watu kweli kiboko, habari ambazo hata hazijaandikwa kwenye magazeti watu wanazo, na hao critics wa ccm sidhani kama wangekaa kimya kama wangesikia haya ! so, that cant be !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…