1. Sitapenda kujadili historia ya Zanzibar, asili ya mtanziko wa kisiasa huko; lakini mimi naomba nichangia suala la principle tu hapa- kwamba pande mbili zimekaa zimajadiliana na kukubaliana mambo Fulani Fulani; baadaye upande mmoja umeanza kwenda tofauti. Its a political problem, that needs a political solution.
2. Nimesoma neno kwa neno rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM ambayo ilishakubaliwa na kamati zote mbili. Suala la serikali ya pamoja linapaswa kutekelezwa kabla ya mwaka 2010.
3. Nimesoma ripoti ya Kamati ya CCM iliyopeleka Butiama kwa ajili ya Kamati Kuu na baadaye halmashauri Kuu; ukweli ni kuwa hoja ya kura ya maoni haikuzuka kikaoni- iliandaliwa kabla kwa pendekezo la Karume na kukubaliwa na wanakamati. Pamoja na uzuri wa dhana ya kura za maoni, lakini nia(motive) yake hapa si nzuri! Kwa serikali ambayo haifanyagi referendum katika masuala muhimu kihistoria kama Muungano, Katiba, Mfumo wa Vyama vingi, kumuundoa Rais wa Zanzibar kama makamu wa Rais(ambalo lilikuwa ni suala katika makubaliano mama ya muungano); inatia shaka serikali kama hiyo itakapo suala la kura za maoni Zanzibar. Ni Kikwete huyu huyu ambaye alipokwenda Kenya hakutaka wakina Raila na Kibaki wafanye kura za maoni, akata wasaini makubaliano na kuyatekeleza. Wakati wa kuibwa kwa kura hakuitishwa kura za maoni, kosa moja haliwezi kuhalalisha kosa, lakini kosa moja linaweza kutoa ishara ya kosa lingine! Kwa ujumla ukiisoma ripoti hii ya Kamati ya CCM; ukisoma na Barua ya Mwisho ya Makamba; utagundua kuwa Makamu Mwenyekiti Msekwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete- hawakusema kweli wakati wakieleza mchakato wa Maazimio ya NEC ya CCM na Matokeo yake!
4. Nilikuwepo Diamond Jubilee jana na nimemsikiliza Lipumba toka mwanzo mpaka mwisho. Nilichokielewa ni kwamba CCM imekuwa ikiwatapeli CUF toka baada ya uchaguzi, ikiwafanyia unafiki wa hali ya juu- CUF nayo kwa upande wake ilikuwabali ku-give in too much; ikakubali ghilba za aina zote ikiwa na matumaini makubwa kwamba Kikwete yuko genuine! Na kwa kiasi kikubwa mambo yote haya yalifanyika kwa siri ya pande mbili; kwa mategemeo makubwa ya CUF kwamba pengine serikali ya mseto ingetokea. Kumbe CCM wakati wote ilikuwa ikiweka kadi chache mezani na nyingine nyingi zaidi kuzificha chini ya meza.Ukiangalia mtiririko wa matukio katika hii miaka mitatu kuhusu Zanzibar utagundua ama Rais Kikwete anafanya unafiki wa hali ya juu wa kisiasa, au ni kiongozi dhaifu katika CCM kama mwenyekiti anayezidiwa nguvu na makundi mengine ndani ya chama chake. Kwa vyovyote vile, hali hii ikiachwa bila panga kuitwa panga na si kisu kikubwa ni ishara mbaya kwa utangamano wetu kama taifa haswa kwa kuwa kwa sasa CCM ndicho chama tawala!
5. Tunaungana mkono na CUF katika hili, kwani kitisho cha demokrasia mahali Fulani ni kitisho cha demokrasia mahali pote. Maandamano ya jumamosi, hayapaswi kuwa maandamano ya CUF, yanapaswa kuwa maandamano ya umma! Ama hakika, uwongo una mwisho- lakini ukweli unapaswa husimama milele, na ukweli hauna itikadi. CUF wanaweza kuwa walijikwaa mahali Fulani katika mchakato huu; lakini sasa ni wakati wa kutazama mbali zaidi, kutazama picha kubwa zaidi- CCM ikiwachwa ikapita katika hili, itandelea kuacha na ufisadi mwingine ukatawala kwenye RICHMOND, BOT nk na hatimaye kuweka misingi ya ufisadi wa kudumu zaidi katika uchaguzi mkuu 2010. Hatupaswi kuacha utadamuni wa ufisadi, usanii wa kisiasa, uchezeaji wa haki, na wananchi kukaaa pembeni kama watazamaji na wanyooshaji vidole kuendelea katika taifa letu. Ni wakati mwingine wa kuandelea kuchukua hatua!
JJ
PS:
Mwenye Hotuba ya Jana ya Lipumba atuwekee hapa tafadhali
Mwenye rasimu ya makubaliano ya CUF na CCM iliyokubaliwa na kamati za pande mbili aiweke hapa pia tafadhali