Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Kwahiyo wabunge wa
Pasco Leo kasema yote!hajamung'unya maneno!huo aliosema ndio kweli yenyewe!hakuna mzaha wala kubembelezana!
cuf kutoka znz nao watakufa na
Hivi pasco unajua znz kuna wabunge wa cut?
 
Kila siku najiuliza hili swali
watu wanaosema 'tutaulinda muungano wetu' kwa gharama yoyote

exactly wanamaanisha nini?
why huu muungano ulindwe kwa nguvu?
Muungano unatumika kuwapatia "maisha bora" wadanganyika.
CCM imeng'ang'ania madaraka Zanzibar tangia 1995 ili kuipa uhai CCM Tanzania bara. Kwa hiyo, kuulinda Muungano tafsiri yake ni kuendeleza maigizo ya uchaguzi mkuu na Tume "huru" ziendelee kumtangaza Mgombea wa CCM wa nafasi ya Urais "mshindi".
Anguko la CCM Zanzibar linalazimisha CCM kutumia vyombo vya dola kubaka demokrasia kwa manufaa ya CCM ili kutoa sura kuwa CCM ni Chama chenye nguvu na kinapendwa na wananchi Tanganyika (Tanzanaia bara)na Zanzibar.

CCM bila mbeleko ya vyombo vya dola ni sawa na kumsukuma mlevi. Wananchi wamechoka kufaidi maendeleo na"maisha bora" yanayoletwa na CCM.

Pia ukipitia huu uzi utaona sababu ya CCM kubaka demokrasia(kulinda muungano kwa gharama yoyote).
Link Kwanini CCM inaogopa Ushindi wa Maalim Seif (UKAWA) Zanzibar?

Umeona vipi CCM walichakachua Rasimu ya Warioba, CCM wanalinda kitumbua chao(mbeleko). Mbeleko ya CCM ni Muungano na vyombo vya dola.
Uhai wa CCM unatengemeana na kulinda Muungano kwa gharama yoyote. Tena Muungano wenyewe ni wa aina hiyo aliyoieleza Lukuvi, kaka mkubwa na ndugu mdogo, Muungano wa serikali mbili.

Uzi huu pia unaweka bayana mazingaombwe ya Muungano. Link Tundu Lissu na Kiinimacho cha Muungano

Kwa kifupi ,(Marais walioteuliwa na CCM)CCM wanamaanisha chama cha upinzani hakitaachiwa kushika madaraka hata Chama hicho kikishinda kwa wingi wa kura. Hiyo inaendana na kusimikwa kwa Tume "huru" za NEC na ZEC ili kutangaza matokeo ya Uraisi ambayo hayawezi kuhojiwa au kupingwa mahakamani.

Link Hakuna Chama cha Upinzani kitaongoza Serikali Tanzania
 
Kwahiyo wabunge wa
Pasco Leo kasema yote!hajamung'unya maneno!huo aliosema ndio kweli yenyewe!hakuna mzaha wala kubembelezana!
cuf kutoka znz nao watakufa na
pasco wabunge wa cuf znz watashindwa kukiokoa chama kisife?
 
Kila siku najiuliza hili swali
watu wanaosema 'tutaulinda muungano wetu' kwa gharama yoyote

exactly wanamaanisha nini?
why huu muungano ulindwe kwa nguvu?
Mkuu The Boss, huu muungano unalindwa kwa gharama yoyote, kwa sababu una sababu!, kinachofanya nchi yetu kuitwa Tanzania ni huu muungano wetu!, tunaigharimia Zanzibar kwa gharama kubwa kwa ajili tuu ya huu muungano!, hivyo unalindwa kwa nguvu kwa sababu!, nikikuambia kuna uwezekano hata Abedi, ilimbidi aondoshwe ili kuulinda huu muungano!, Jumbe mpaka leo yuko kizuizini ili kuulinda huu muungano!, chama au mtu yoyote atakayeonekana ni threat kwa majaaliwa au mustakabali wa muungano huu, kamwe hawezi kupewa nchi!, mnaweza kukuta hata Jecha ni mtekelezaji tuu wa maelekezo!.
Kama una nafasi pitia nyuzi hizi
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano
Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano ?!...
Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano?!.
Jee Wajua Kuwa Kuna Uwezekano Tanzania Sii Nchi Halali Kisheria?!.
Bunge Maalum Lapigwa Changa la Macho!? Lapewa"Act of Union" badala ya "Articles of Union!".
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa Zanzibar!.
Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu!.
'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'-Karume
Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, Then Twende Kwenye Nchi Moja Serikali Moja!.
Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili Ndio Utavunja Muungano!.
Pasco
 
Nakumbushia tu kuwa mfalme hajavaa nguo. Mfalme anatembea mbele ya umma bila ya kuvaa nguo.

Uchaguzi ulishafanyika na haukuwa na dosari. Ushahidi uko wazi. Hakuna Mgombea au wakala wa chama chochote aliyejaza fomu ya malalamiko na kuiwasilisha ZEC.

Lubuva alitoa taarifa kuwa hakukuwa na kasoro za uchaguzi zilizoripotiwa kwa NEC kutoka Zanzibar.
Kwa kupotosha kabisa Jecha pia hajawahi kusema kuwa ZEC ilipokea fomu za malalamiko zinazolalamikia kasoro za uchaguzi.

Msikilize Lubuva kuanzia dakika ya 6:40
 
Mkuu iL Buono, huu ndio mjadala wa bandiko hili, jee CUF watasusia uchaguzi wa marudio na kufa natural death, au wataingia tena kwenye uchaguzi na kwenda kupokea kichapo?!. Tusubirie matokeo ya hivyo vikao vyao!.

Pasco
 
Afadhali wewe umeliona hilo eti chama kisiposhiriki uchaguzi kinakufa, Pasco ni wewe au kuna mtu kakusaidia kuandika leo?
Mkuu Pasco wa jf ni yule yule juzi jana na leo!.

Unaweza kupitia kwenye hii michango yangu kuhusu Zanzibar uangalie kama nimebadilika!.
Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto https://www.jamiiforums.com/threads...-kelele-tu-bila-kuchukua-hatua-zozote.974722/
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukuhttps://www.jamiiforums.com/threads...-maalim-seif-na-cuf-ndio-walioshinda.1001701/
IMETHIBITISHWA PASI SHAKA KUWA NI KWELI KABISA, ZAhttps://www.jamiiforums.com/threads/kama-hii-ni-kweli-ccm-zanzibar-ndiyo-bye-bye.77191/
Kama hii ni kweli, CCM Zanzibar ndiyo Bye Bye? https://www.jamiiforums.com/threads/kuna-haja-ya-kuhofia-kurudiwa-uchaguzi-zanzibar.989403/
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? https://www.jamiiforums.com/threads/iwapo-ccm-itashindwa-zanzibar-nini-majaaliwa-ya-muungano.838604/
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muunganohttps://www.jamiiforums.com/threads...a-haitumiki-zanzibar-pinda-akiri-utata.66012/
Kumbe Katiba ya Tanzania Haitumiki Zanzibar! https://www.jamiiforums.com/threads...-wingi-wa-matangazo-ccm-ndio-washindi.925526/
Kama Ushindi wa Uchaguzi Utatokana na Wingi wa Matangahttps://www.jamiiforums.com/threads...-wa-zanzibar-kabla-hajamwaga-sumu-hii.737375/
Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar https://www.jamiiforums.com/threads/kumuepushia-aibu-ya-kushindwa-ccm-isimsimamishe-dr-shein.807695/
Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shttps://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lichopo-ni-makubaliano-tuu-ya-muungano-2.html
Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano ?!...
Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano?!.
Jee Wajua Kuwa Kuna Uwezekano Tanzania Sii Nchi Halali Kisheria?!.
Bunge Maalum Lapigwa Changa la Macho!? Lapewa"Act of Union" badala ya "Articles of Union!".
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa Zanzibar!.
Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu!.
'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'-Karume
Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, Then Twende Kwenye Nchi Moja Serikali Moja!.
Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili Ndio Utavunja Muungano!.
Pasco
 
Mkuu Pasco tambua siasa za Zanzibar tofauti na bara pia cuf kwa pemba ni Zaidi ya siasa
 

Sijui nini kimekukuta Mkuu! Mihemko iliyokupata katika kuandika uzi huu sijui unatokana na nini au kuna mtu kakuandikia?
Yaani badala ya kumuombea Busara imwongoze JP, wewe unaendeleza hii falsafa iliyokwisha anzakushindwa hata mwaka haujaisha!

Umesikia Dodoma wakilalilia wadudu?

 
Siamini kama wapiga kura wote walioko Zanzibar na pemba watakubaliana na mawazo ya viongozi wa CUF au hata CHADEMA kuususia uchaguzi ambao tarehe yake imeishatangazwa.Ndio wapo wenye akili za kushikiwa watakaokuwa tayari kufuata maagizo ya CUF kama nyumbu,lakini wapo wale wanaojitambua ambao kwa kutumia busara zao wataiona picha kubwa ya mtafaruku huu na matokeo yake baadae na kuamua vinginevyo kwa maana ya kwenda kupiga kura tena.CUF wangewahamasisha wafuasi wao waende kupiga kura maana kwa kuwa wana uhakika wa kushinda wangepata uhalali wa kukabidhiwa nchi sasa,Hata kama wakishindwa kupata mwaka huu ni vyema wakajiandaa vizuri kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na hasa kupigania katiba mpya. Huu ubinafsi wa viongozi wa kutaka kushika au kubaki madarakani na kujiona kuwa ni wakati wao kuingia madarakani hauwezi kujenga zaidi, sana ni kubomoa.Naunga mkono mawazo ya mtoa mada kwa kuwa ushindi unapatikana kwenye sanduku la kura tu na si vinginenyo.
 
Njaa ni kitu hatari sana ! yaani pasco unajidhalilisha kwa kiwango hiki ! kwa bei gani uliyolipwa ? huwezi kufuta cuf kwa kusimika wabunge wa uongo pemba , yalitokea haya siku za nyuma .
Huyo Pasco anaifikiria Tanzania kama kisiwa; hakuna taifa linaloweza kukiuka misingi ya kidemokrasia na kuendelea kubakia salama katika ulimwengu wa sasa. Yalimshinda Bagbo na wengineo naye Nkuruznz anakiona cha moto; huku ni kukaribisha majanga kwa mustakabali wa taifa nzima
 
Mkuu Pasco tambua siasa za Zanzibar tofauti na bara pia cuf kwa pemba ni Zaidi ya siasa
Mkuu hili kila mtu anayefuatilia mambo ya siasa za Zanzibar analijua, kuwa kule Pemba CUF ni zaidi ya chama cha siasa, na vingozi wa CUF ni zaidi ya viongozi wa siasa, naamini hata wale vijana wa Amiri Jeshi Mkuu, hili wanalitambua, na zile kauli kama "jino kwa jino", na haya ni baadhi ya majina ya Maskani Zao, 'Osama Camp', 'Al Zawahir', ' Tora Borra', 'Liwalo na Liwe' Maskani Msichoke!'
'Kifo Kimeumbwa', 'Kuzaliwa Siku Moja, Kufa Siku Moja' etc, hivyo mshindi wa uchaguzi wa marudio akiishatangazwa, hawatasubiri majuto ni mjukuu, watatumia kinga ni bora kuliko tiba!.

Pasco
 
Alaa umekubali kuwa hata Jecha ni mtekelezaji wa maelezo ya kufuta uchaguzi!

Mkuu Pasco

Tuwe wawazi tuache ushabiki, kufutwa kwa matokeo ni kwa sababu ccm imeshindwa uchaguzi, hakuna sababu nyengine.

Suala la muungano huwezi kulilinda milele na huwezi kulilinda kwa bunduki, ipo siku hata watanganyika nao watadai tanganyika kwa nguvu za Umma wakati ukifika kama wazanzibari wanavyo dai zanzibar yenye mamlaka kamili.

Sio kweli kwamba zanzibar inahudumiwa na serikali ya muungano kwa kodi za watanganyika, MCC isinge zuiya zile fedha kwa sababu wanajua kuwa kuna mgao wa Zanzibar humo humo, kwa maana suala la zanzibar ni kubwa tofauti unavyo fikiri. Na pesa ambayo serikali ya Tanzania inaipa zanzibar ni moja ya mchango ilitoa 11 percent katika bank Kuu.
Zanzibar inapewa 4.5 tu kwa mwaka, hata hivyo fedha hizo zanzibar hupata less than that na nyingine kuishia katika matumbo ya viongozi wako.

Wazanzibari wanautaka muungano lakini wa haki kwa kila upande, na mfano wa Zanzibar ilikuwa ikipenda ushirikiano na nchi jirani ni Eac, zanzibar ilikuwa ni member wa East Africa community.

Ccm nyie mushazoea siasa za maji taka, ubaguzi wa rangi na dini, na haya ni kwa sababu viongozi wenu walianza kupalilia na kuyalinda na kuwasomesha watoto wetu huu ubaguzi, kaanza Nyerere, mizengo pinda, lukuki, na sasa Shein nae anayapokea kwa maandamo mabango ya ubaguzi.
 
Mkuu GHIBUU, sijasema Jecha ni mtekelezaji nimesema usikute ni mtekelezaji tuu!, kuhusu hili la sababu ya kufutwa kwa uchaguzi halina mjadala ni kweli CCM ilishindwa.

Nakubaliana na wewe kuhusu kuboresha muungano ili uwe muungano wa haki.

Kwa ajili ya ushaui huu sasa mimi ndio nimekuwa CCM?!.

Pasco wa jf, ni yule yule, juzi, jana na leo, sio mwanachama, mshabiki, mfuasi au mkereketwa wa chama chochote cha siasa, ni mfuasi wa ukweli halisi jinsi ulivyo!.
Pasco
 
Pasco

Nimekushutumu kuwa ni mfuasi wa ccm kwa sababu siku zote nakala au hata maoni yako ni kuukosoa upinzani au kuikosoa zanzibar, sioni nakala za kuikosoa ccm juu ya suala la muungano au something else.

Wazanzibari mkuu hawana tija na muungano, kumbuka Nyerere ndio alie mshawishi Abeid Amani Karume kuunda muungano.

Nyerere ndiye alimlazimisha or mshauri Aboud Jumbe kuunganisha vyama vyao vya siasa ili kuweza kuitawala zanzibar kisiasa, baada ya hapo siasa nayo ikatungiwa sheria ili kuwa na madaraka na nguvu, hapo Nyerere alitumia mwanya kumuangusha Jumbe.

Mkuu

Suala la zanzibar juu ya muungano sio suala la manufaa kwa zanzibar, wala hatufaidiki na chochote. Hata ukichukulia hoja ya Wazanzibari wanao ishi bara kuwa huru, hata kabla ya muungano walikuwa huru, na biashara zilifanyika katika ukanda huu wa East Africa, zanzibar, mombasa Kenya na Tanganyika hata Comoro.

Tujadili fact zenyewe katika muungano, ni nani hasa anae faidika na huu muungano?
 
Hivi Ww Mtu Una Shida Gani!!!?? NANI Anakuambia WANACUF Ndio Wenye UDINI Na WanaCCM Ni Mapagani!!!!?? Hivi Wkt Zanzibar Walipokuja Na Hoja Ya KUJIUNGA Na OIC, Ww Ulikuwa Na Umri Gani?? Maana Kama Ungekuwa Na "AKILI "Kwa Kipindi Hicho, Sidhani Kama Ungesema Eti CUF Ndio Wataleta KUJIUNGA Na Mashirika Ya Kidini, Wkt Hilo Suala Lilipelekwa Bungeni Na WanaCCM Wenyewe, WAULIZENI Wakubwa Zenu!!! PIA Suala La Muungano Ni Wa MAKUBALIANO Kati Ya NCHI 2 Zenye MAMLAKA Kamili!!! ILA Kwa Kubembeleza Kwao Kuingia Ktk Muungano, Walikubali Kuifuta Tanganyika Yao!!
 
maneno ya kujitapa yanini hata gadafi alikuwa na maneno kama haya alijishutikia anatokwa na haja ndogo bila kupenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…