TangataUnyakeWasu
JF-Expert Member
- Dec 18, 2016
- 1,268
- 1,611
CUF HAITAKUWA IMARA TENA! MISSION IMEKAMILIKA KWA 80+℅
CUF sasa inaishilia, ni kama mpango unakamilika, mpango mkakati umetengenezwa kimkakati zaidi, kuhakikisha CUF haina nguvu tena, ili kuleta unafuu visiwani. Wabunge wa majimbo wakishavuliwa uanachama, majimbo yao yatakuwa wazi, uchaguzi utarudiwa, kama hujui ni mpango,: kumbuka kauli ya juzi ya mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, pale aliposema' ikiwa wabunge wa CUF watavuliwa uanachama, tume imejiandaa kwa dharula yoyote na bajeti ipo! Akili kumkichwa' mkurugenzi wa tume anazungumzia uchaguzi mdogo kwenye majimbo ambayo bado yana wabunge! MISSION
Lipumba sasa anatambuliwa na kila taasisi ya sirikali, anatambuliwa na Bunge, anatambuliwa na Msajili, anatambuliwa mpaka na taasisi ya jikoni! MISSION
Kete kwa upande wa CUF Halisi ilikuwa imebaki moja tu (MAHAKAMA) baada ya makosa kufanyika nyuma! Ndiyo makosa yalifanyika mwanzo kabisa kwa upande wa Maalim Seif kumdharau Lipumba na kumuona ni mtu mmoja tu anayetapatapa kisha atatulia, hawakumuona mapema aliyekuwa nyuma ya Lipumba! Hili lilikuwa Kosa kubwa! Wamekuja kushituka na kuiona nguvu yake kipindi ameingilia bodi ya wadhamini ya CUF! Hapo ndo walishituka na kumbe tayari walikuwa wamechelewa! Walipaswa kumshughulikia mapema!
Sasa kete ya mahakamani nayo inaanza kufeli, kwa nini nasema inafeli?
1😛amoja na kesi ya kutomtambua Lipumba na kauli ya Msajili kuwa mahakamani! Bado Lipumba ameendelea na shughuli za chama kwa kujitanua hadi kufukuza wabunge bila woga na hakuna mhimili unaohoji!
2: Kutupiliwa mbali kwa mapingamizi ya wabunge wa CUF waliovuliwa uanachama, ni pigo kubwa kwa upande wa Maalim Seif! Hata wakirekebisha vifungu walivyotakiwa kuvirekebisha, wao wako mahakamani, Lipumba anaendelea na shuguli za chama huku akijipanga kuwaita na kuwahoji wabunge wa majimbo!
3: Kutotambulika kwa maazimio ya CUF upande wa Maalim wa kuwavua ubunge wabunge wawili ni pigo kubwa pia.
NANI ALAUMIWE
1. Mtatiro;
Ndiyo, huyu ni mtu wa kwanza kabisa kulaumiwa na wana CUF' atanisamehe. Yeye alipewa jukumu kuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, Lakini amekuwa akifanya siasa za mtandaoni zaidi, kila Lipumba akifanya jambo, yeye huja kulalamika mtandaoni na hukomea kuandika tu bila ya kuelezea njia mbadala ( rejea post zake kwenye plofile yake) Sasa kama yeye kiongozi analalamika na kujibu mapigo ya Lipumba mtandaoni, wengine watafanyeje? Yeye huiongelea CUF baada tu ya Lipumba kufanya kisanga, Lipumba akiwa kimya' na yeye yuko kimya. Kwa hiyo amekuwa akicheza ngoma ya Lipumba!
2. Maalim Seif
Yeye namlaumu kwa kutochukua hatua mapema, Lipumba hakupaswa kupewa nafasi mapema, naye sasa amekuwa akijibu mapigo ya Lipumba tu badala ya Lipumba kujibu mapigo yake! Lipumba akiita Baraza lake, naye anaita lake, Lipumba akifukuza wabunge, naye anafukuza! Amechelewa sana!
NINI CUF YA MAALIM IFANYE?
Kwa sasa CUF ya Maalim imebanwa sana na Lipumba, na naona imebakiwa na option mbili tu!
1. Mahakama;
Mahakama pekee kwa sasa ndo imebaki kuweza kuamua kama CUF iwe ya Lipumba au ya Maalim. Na ikitokea mahakama ikaamua kuwa CUF iwe ya Lipumba, Maalim atabaki na option mbili tu, mosi kuungana na Lipumba au
2. Kuongeza nguvu CHADEMA.
Option ya mwisho kabisa kwa Seif ni kutangaza kuachana na siasa za CUF ya Lipumba na kuongeza nguvu upande wa CHADEMA. Faida kubwa kwa upande wa CHADEMA ikiwa hili litatokea, ni kupata wafuasi wengi Zanzibar bila chenga! Na hapo ndipo msemo usemao "Waliokuwa nyuma ya Lipumba waliruka mkojo wakakanyaga kinyesi" utatimia.
Sent using Jamii Forums mobile app