Tetesi: CUF: Lipumba kuwafuta uanachama wabunge wote wa kuchaguliwa majimbo yote ya Bara

Wapi nilipomtaja LOWASA? Hivi kwanini Lowasa anawafanya muweweseke hata wakati wa kujadili vitu vya msingi?
Kwanini LIPUMBA HAKUPATA ZAIDI YA VITI VIWILI BARA KIPINDI CHAKE CHOTE NA ALIZUNGUUKA NCHI NZIMA AKIJINADI NA KUINADI CUF? KWANINI VITI VYA TANGA, MWANZA NA KILWA VILIPOTEA CHINI YAKE WAKATI HUO? hilo ndilo lilikuwa swali langu na aliyempokea EL UKAWA anajulikana ukihitaji ushahidi zaidi tutauweka hapa
 

Attachments

  • 1.jpg
    15.6 KB · Views: 34
Jinsi sakata lilivyo huwezi kumuacha Lowasa kumtaja, yeye ni mwanasiasa na wala sio dhambi kutajwa ktk mambo ya kisiasa, ondoa hofu mkuu sijui kwanini akitajwa huyo mtu mnajawa hofu na kupaniki..

Kumpokea Lowasa ktk ule mkutano aliyetangaza alimtangaza kiitifaki tu, na ndio maana baadaye alijitoa kutokana na nafsi kumsuta, na kwasababu hiyo hiyo Katibu mkuu wa Chadema alijiuzulu siasa, ni ujinga wa mbowe na Maalim uliopelekea leo Chadema inakatibu mkuu asiyejua majukumu yake.. Hahahaaa (natania tu mkuu)

Suala la viti nimeshakujibu, hiyo dhambi haiwezi kuwa ya Lipumba peke yake ukamuacha Seif.
Nikakuambia hayo Mafanikio ya Ukawa yametokana na Uasisi wa Dr. Slaa na Prof. Lipumba kabla mvurugaji hajaja kuvuruga...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Seif alizunguuka Zenji alipata viti vingapi? Ili tutathmini kila mmoja upande aliouzungukia
 
Seif alizunguuka Zenji alipata viti vingapi? Ili tutathmini kila mmoja upande aliouzungukia
Ni utendaji wa taasisi gani huo unaopimwa kulingana na mtu pale anapotokea?
Seif si Katibu wa Zenji peke yake, ni katibu mkuu wa Tanzania, utendaji wake unapaswa kupimwa kulingana na matokeo chanya ya Tanzania sio sehemu moja peke yake...

Chadema imeimarika zaidi kaskazini kuliko kusini, hapo unataka kusema nini kiutendaji? Unataka kumbagua nani umuhusishe nani na mafanikio ya Chadema?

Lau kama Seif alikuwa akifanya kazi kwa kuangalia Zanzibar peke yake basi hilo nalo ni jambo lingine la kukosoa kiutendaji, hafai kuwa kiongozi wa umma mtu anayeangalia kwao pekee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee kumbe zile halmashauri nyingi ambazo CDM inaongoza zote ni za kaskazini? Mbeya ni kaskazini pia? Maalim Seif kama katibu alitenda kazi yake, Mwenyekiti akawa anatengua kwa maslahi yake. Viti vya Tanga, Liwale, Mtwara na Mwanza viliuzwa na le profesale na wachumia tumbo wenzake. (nasubiri povu tena hapo!) teh teh teh.
Tanzania kazi tunayo!!!
 
Bado nitajaribu kukuelekeza...
Nimesema hivi, Chadema imeimarika zaidi kaskazini..!!
Huo msemo umeuelewa lakini??

Na hapa nakukumbusha, wewe ndiye uliyeleta hoja za viti, nilichofanya ni kukujibu kulingana na hoja zako..!!
Ila ukitulia nadhani utaelewa kwa usahihi mantiki yangu..!!

Sina haja ya kujibu hizo porojo zako za kuuza viti sijui nini, hizo kwangu ni kama sauti za mbwa au paka jalalani.!!
Hazina matiki yoyote ya kujadiliwa na wenye akili timamu. Labda kama utaweka hapa hati za hayo mauziano...

Sehemu uliyobold ni jibu la maneno
yako haya...

Seif alizunguuka Zenji alipata viti vingapi? Ili tutathmini kila mmoja upande aliouzungukia

Sasa sijui katibu mkuu kazi yake iliishia huko huko Zenji peke yake, jibu unalo..!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna taifa la ajabu kama Tanzania. Unawezaje Kuua demokrasia namna hii mchana kweupe?ccm Mungu anawaona. Hii Dhambi mtaibeba hadi Jehanam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maalim Seif kujua anatumikia Chadema ni ngumu Sana, kazingirwa.
Mpango unahakikiwa kiufundi Sana huku akiamini CCM ndo wamabaya wake.
Acha aijenge Visiwani Chadema kwa kupambana na Lipumba.

Lipumba si kama kina James Mapalala, Hamad Rashid. Ni type nyingine kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lipumba kwa nguvu ya 'CCMserikali' atafanikiwa kuiua CUF na kubaki na Magdalena na 'wenzao' katika usaliti. Kitu ambacho watakujagundua hatimae ni kuwa, Wao nao ndo watakuwa wamemalizika kisiasa kama ganda la muwa. CCM haitowahitaji tena kama ilivyowafanyia wengine ilowahi kuwarubuni. Wananchi ndo kabisa hawatakuwa na shughuli nao. Kama ilivyokuwa kwa Mrema na Cheyo, baada ya uchaguzi 2020, Lipumba nae atabaki gamba lisilo na mvuto tena la CUF.
Wahenga walisema: WISE MEN LEARN FROM OTHER PEOPLES' MISTAKES. LAKINI Lipumba na wasaliti wenzie wanaanda kwa kujivunia mazishi yao wenyewe kisiasa. HIVI Uprofesa wote uko wapi? Au ndo kama anavyokejeliwa PROPESA!
 
Bora hata yule mwenzake aliyekwenda zake kanada kula mihogo ya kule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ndio siasa. Tulia dawa iingie.
 
Tayari nimepata majibu ya point zako na nimekutambua vema unani wewe! mnatambulika kwa visigino vyenu na uwezo wenu wa kutoa majawabu ambayo hakika yanaendana na sifa zenu.

Ukimkuta mtu anajisifia akili zake... unatambua yu nani usiulize!!!
 
Yaani Chadema mnaiua CUF bila huruma?
Maalim Seif akijiunga na Chadema itakua kajimaliza jumla

Sent using Jamii Forums mobile app
Minadhani maalimu akijiunga chadema,CUF ndo itakufa Zanzibar,na CHADEMA kuwa na nguvu Zanzibar,kwa sababu maalimu anaushawishi mkubwa sana Zanzibar,na Lipumba analijua hilo ndo maana kila siku anamwita buguruni akampangie majukumu.kumbuka zitto walipomtimua CHADEMA walisema ndo washammaliza,lkn hata alipokwenda ACT wazalendo alishinda pia na kwa maalimu ni hivyo hivyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…