VIONGOZI wa Chama cha Wananchi (CUF) kimemtaka mmiliki wa makampuni ya GSM, Ghalib Said kutoa msaada pia kwa vyama vingine vya siasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Wakizungumza jijini Dar-es-salaam , baadhi ya viongozi wa CUF wamesema kitendo cha kampuni hiyo kuchangia Shilingi bilioni 10 kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaonyesha dhamira ya kusaidia shughuli za kisiasa, hivyo ingekuwa vyema msaada huo ukatolewa kwa vyama vyote ili kuhakikisha ushindani wa haki.
View attachment 3442819