CUF wameionya Urusi ikome kuwatumia Watanzania kwenye Vikosi vyake Vitani

Sio watanzania tu, ni vijana wa Afrika. Wamekuwa wakihadaa kutoa scholarships kwa vijana wa Afrika, ukifika huko unapewa kesi za mchongo, mateso makali gerezani hadi unatamani kujiua, kisha wanakupa ofa, ubaki gerezani au ukapigane frontline.

Ukitafakari mateso yao inabidi kwenda tu ukafie huko kuliko gereza la Urusi.
 
Wameongea saa ngapi tena? Mbona mbatupa habari nusu nusu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
CCM imekaa kimnya tu, mtu anatolewa jela ya serikali urusi kafungwa, hivi mtu au kikundi kinaweza kumtoa mtu segerea bila serikali kuhusika,,leo tumtoe mrusi tukampiganishe vita msumbuji, hao Warusi watakaa kimnya?

Halafu liwaziri linatoka huko na mimacho yake kinasema Mtanzania haluhusiwi kujiunga na jeshi..mtu alikuwa jela ANAJIUNGA vipi na jeshi? Kama sio kulazimishwa?

Bora CUF mmesema kidogo hongeleni sio hii mibwanyenye ya CCM.
 
Kwa nini wafunge wanafunzi walio kwenye scholorship badala ya kuwarudisha makwao?
 
Kuna mtz aliepewa scholarship kwenda Urusi akabambikiwa kesi???
 
Inasemekana kuwa:kesi ya Bwana Nemes ilikuwa bado iko mahakamani so hakuwa amethibitiswa na mahakama kuwa ni mhalifu ila Putin akampeleka frontline.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…