Ni nani aliyekuwa amejitoa ktk muafaka jamani? CCM au CUF? Mnawapa masifa yasiyowastahili hawa jamaa!! JK aaache mambo makubwa ya nchi aende akashughulikie muafaka ? Muafaka wa nini? Kwani kuna watu bado wako Shimoni au? JK komaa na mambo muhimu siasa za Wapemba na Waunguja Mkapa alizimaliza 2001 . Ni nani aliyechinja askari tena tokea 2001? Visima vina kinyesi kama 2001? Hata maalim sasa kanyoa madevu. Muafaka wa nini?
Heshima
mbele mkuu, huko serious au unatania maana naona kama unasema mpaka CUF waue polisi, CCM na CUF waanze kunya kwenye visima ndo CCM ifikirie muhafaka. this will be a great shame on JK ambaye nchi za Africa sasa wanamtegemea kutatua migogoro yao.
Mkuu lazima tukubali hata kama wewe ni mwanachana wa CCM kuwa hamko serious katika ili mnachotaka ni kupitisha muda ili ifie 2010 kwa uchaguzi mwingine muwaibie tena halafu muamze muhafaka mpya, huu ni usanii na ufisadi wa kisisasa.
JK kila alichowaaidi wananchi naona kinagoma kutimia, maisha bora kwa kila mtanzania imekuwa ni maisha bora kwa mafisadi tu, kutatua mgogoro wa Zanzibar naona kumeota mbawa, kama yuko serious na hili hii ni nafasi pekee ya kuwadhibitishia wananchi kuwa anaweza, sijui ajira 1,000,000 zimeshia wapi maana sasa hivi viwanda vingi vinafukuza wafanyakazi kila siku.