Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
mambo ya kuzingatia:
a. Baada ya CCM, CUF ni chama cha pili kinachopokea ruzuku nyingi toka serikalini.
Kwa sasa tunaangalia CUF tu kwani kupatwa kwao fedha hakutegemei chama kingine kinapata kiasi gani. Ikifika zamu ya CUF na wengine tutaangalia hivyo.
Hivi ruzuku ikifutwa vyama vitakufa?
Je kiasi hicho kinatumika kwa kiasi gani huku bara katika kujiimarisha kisiasa?
Kwa sasa tunaangalia CUF tu kwani kupatwa kwao fedha hakutegemei chama kingine kinapata kiasi gani. Ikifika zamu ya CUF na wengine tutaangalia hivyo.
Nadhani Mwiba atatuambia jinsi zinavyotumika Bara!
Naona nyingi zinatumika kuiangamiza CCM Pemba na kusaidia mikutano ya vile vijembe vya Seif kule Kibandamaiti!
Ni vema pia kujua ktk 2.6 billlions ni ngapi zilitumika bara na ngapi kule Visiwani!
Haya masuala ya ruzuku kusema ukweli yanatakiwa kuondolewa, ni upotevu wa fedha za walipa kodi bure. Hizo mnazoona za CUF, ikitolewa wanayopata CCM ni balaa. Manake ruzuku hutolewa kwa kufuata uwiano wa wabunge wa chama husika.
Vyama kwa kuwa vina wanachama, viachwe vijihudumie vyenyewe, TANU ama ASP (nisisahau na Hizbu, Mwiba akanibana) zilipata wapi fedha, ilikuwa ni kutoka kwa wanachama na wapenzi. Kwa nini sasa tupoteze fedha zote hizo kwa sababu ya vyama badala ya kusaidia miundo mbinu yetu. Na hili la ruzuku ndio kimekuwa kikwazo kwa vyama pinzani kushirikiana pale ambapo kuna kila dalili kuwa kama vitashirikiana vyaweza kuishinda CCM, kila chama kinataka kipate Wabunge wengi ili na ruzuku iwe kubwa. Wizi mtupu!.
Pamoja na kuwa CCM wanapata mara nyingi zaid ya CUF, lakini kama CUF wangekuwa na moyo wa maendeleo then hicho kidogo kingeonekana kinafanya nini, wajitolee waonyeshe mfano kwa kujenga shule moja wa wazazi wa CUF na kuindesha kwa gharama nafuu kwa ajiri ya wanachama wao, au wachangie ujenzi wa madarasa ya shule za serikali badala ya kuendelea kukamua wananchi
TANU na ASP walishikilia madaraka ya nchi na hakukuwa na tofauti kati ya serikali na Chama. Wakati huo wakijichotea watakavyo. Ama hayo ya HIZBU Mwiba ndiye atakaetusaidia.
Unaweza kuwa na mtaji mkubwa ukashindwa kuutumia.Maximo anakula mshahara mkubwa hawezi kuleta kombe.Kwa kiasi ambacho CUF wanapokea inakuwaje hawana mbunge Tanzania bara? au kushindwa vibaya kama kule Mbeya au Tarime? Kwanini hata maeneo ya pwani ambapo naweza kusema ni ngome yao (Tanga, Dar, Pwani) hawana mbunge hata mmoja!