Nafikiri unahitaji kwenda ndani zaidi katika uchambuzi wako. Ni busara ukajiuliza suala la nyongeza . Ni kwa nini hiyo CUF ikawa na uwezo wa kushinda kule Chanja-Mjawiri na Chokocho tu? na siyo popotepale pengine katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Ndio maana yake lakini inaonekana wana agenda ya siri ,si tunafahamu vyombo vya habari vinavyotika kupotosha ukweli ,sasa hata Mwanakijiji nae anatumika ndio maana yake.
MWANAKIJIJI,
Una maswali mawili ya kkutujibu Kwanza kwa nini msingi wa Baruwa umeweka kapuni na kuleta udaku?
La pili nawe umeshakuwa biashara na mtazamo wako?
Naona ujaona bandiko la Mwiba, ambae anadai kuwa CUF bara(Tabora) wameshindwa kulipia pango la ofisi hadi kunyang'anya ofisi hiyo kwa kuendekeza pombe.Wewe Kibunango, wakati mwingine acha utani wakati watu wanapojadili mustakabali wa Taifa. Kila siku wanywa tende, huna msamiati mwingine. Kuwa CCM sio sababu ya kila kitu cha mpinzani ukione ni upuuzi, wote tuko TZ tunapata matatizo sawa, labda useme mwenzetu na ndugu zako wote mko matawi ya juu.
Huyu Mzee Mwanakijiji anahitaji kumwinyishwa kwa lugha nyingine kuzabwa kibao 😀 Wazee wengine ni wachinvi tu.MWANAKIJIJI,
Una maswali mawili ya kkutujibu Kwanza kwa nini msingi wa Baruwa umeweka kapuni na kuleta udaku?
La pili nawe umeshakuwa biashara na mtazamo wako?
Bw. Ngekewa na Mheshimiwa mwenzio mnaonekana hamtaki kusaidia kujibu suala lililowekwa katika bandiko hili. Hivi ruzuku hutumikaje kwa mintarafu ya kuendeleza Chama (CUF) huko Tabora, Tanga na Dodoma na kwengineko. Ama mimi nasema hata huko Kitovuni (Pemba) ruzuku haijaonekana ikitumika kutengeneza majengo ya matawi katika hilo eneo ambalo CUF tunaambiwa inapata kura asilimia zaidi ya thamanini.Karibu tena PAKACHA! Hatukuoni mpaka tuijadili CUF au Wapemba? Kuna Zengwe hapa la CCM na mapigano ya matusi na shutuma hebu tuwe pamoja nawe.
Sasa bandiko feki inabidi lijibiwe kifeki ,ruzuku Lipumba na seifu haiwatoshi vipi wataipeleka kwengine,wanachama wenyewe wajenge matawi yao,si wao ndio Chama Chao ,ruzuku ni rushwa kutoka kwa serikali CUF wanairudisha hawaipokei.Bw. Ngekewa na Mheshimiwa mwenzio mnaonekana hamtaki kusaidia kujibu suala lililowekwa katika bandiko hili. Hivi ruzuku hutumikaje kwa mintarafu ya kuendeleza Chama (CUF) huko Tabora, Tanga na Dodoma na kwengineko. Ama mimi nasema hata huko Kitovuni (Pemba) ruzuku haijaonekana ikitumika kutengeneza majengo ya matawi katika hilo eneo ambalo CUF tunaambiwa inapata kura asilimia zaidi ya thamanini.
Barua ya asili ilikuwa imerudisha ruzuku ila msajili akadai kilichorudishwa ni kidogo ndio akaonyesha feza yote iliyotoa tokea 1995 kwa maana feza iliyorudishwa haikutimia.
Hili la ruzuku limekubana, na huna pa kutokea!Sasa bandiko feki inabidi lijibiwe kifeki ,ruzuku Lipumba na seifu haiwatoshi vipi wataipeleka kwengine,wanachama wenyewe wajenge matawi yao,si wao ndio Chama Chao ,ruzuku ni rushwa kutoka kwa serikali CUF wanairudisha hawaipokei.
Barua ya asili ilikuwa imerudisha ruzuku ila msajili akadai kilichorudishwa ni kidogo ndio akaonyesha feza yote iliyotoa tokea 1995 kwa maana feza iliyorudishwa haikutimia.
Hili la ruzuku limekubana, na huna pa kutokea!
Sijaona mbano wowote hapo ,labda ikiwa ni mgeni wa siasa ndio unaweza kubabaika ,ila kwa mimi naona hoja haina mshiko.
Bw. Ngekewa na Mheshimiwa mwenzio mnaonekana hamtaki kusaidia kujibu suala lililowekwa katika bandiko hili. Hivi ruzuku hutumikaje kwa mintarafu ya kuendeleza Chama (CUF) huko Tabora, Tanga na Dodoma na kwengineko. Ama mimi nasema hata huko Kitovuni (Pemba) ruzuku haijaonekana ikitumika kutengeneza majengo ya matawi katika hilo eneo ambalo CUF tunaambiwa inapata kura asilimia zaidi ya thamanini.
Pakacha, Mi ni Muunguja mwenzio hivyo tusiwe wanafiki. CCM huko kwetu mmefanya nini kwa ruzuku mnayopata? Matawi mengi aidha ni magifu yakiyoachwa na Wamanga au ukilona lina sura nzuri basi lilijengwa na serikali wakati wa ASP. Hata Makao Makuu ya CCM pale Kisiwandui yalijengwa na Marehemu Mzee Karume na hadi sasa hakuna maendelezo yoyote mbali ya kupokea mamilioni ya pesa za kodi kwa Wapemba mliowakodisha kuzunguka hilo jengo. Jengo la Umoja wa Vijana Darajani taabani. Sasa hizo pesa za Ruzuku nanyi mnazipeleka wapi na mnapata karibu mara mbili za wanaopata Watani wenu CUF? Wacha nisimame hapo mengine labda kama utayatafuta.
Hili la ruzuku limekubana, na huna pa kutokea!
Naona si kawaida yako kuacha kusoma thread inavyokwenda. Kwa hili hata mie nisiyekuwa mwanachama wa CUF lisingenitowa jasho seuze mpinga Usultani MWIBA.
Nafikiri kuna mchangiaji alyezigawa hizo pesa billioni karibu tatu kwa mwezi ni karibu 250 millioni kwa mwezi hebu fikiria kiasi hicho kama ni tegemezi la kuendesha chama nchi nzima utafika wapi.
Nafikiri kuna mchangiaji alyezigawa hizo pesa billioni karibu tatu kwa mwezi ni karibu 250 millioni kwa mwezi hebu fikiria kiasi hicho kama ni tegemezi la kuendesha chama nchi nzima utafika wapi.
Ngekewa,
2.6 Bil ukigawa kwa miezi 12 ni shilingi milioni 105 tu kwa mwezi!
Zii pesa nyingi!
Fikiria ukuwa na mkutano Mkuu.. na wajumbe wote toka kila wilaya Tanzania ni shs ngapi?
Hivyo unaamini kuwa Fedha ndio kila kitu? Basi CCM isingeshindwa kupata viti kule Pemba na CUF wangeanza kupata viti vingi kule Umguja.
Hata hivyo CCM walistahili kushinda nchi nzima kwa vile walikuwa na ruzuku mara kumi zaidi ya CUF na mabilioni ya wananchi kwa kupitia EPA. Nafikiri pesa si suluhisho bali ni kukubalika na wananchi. Tatizo la CUF kutopata nguvu BARA ni kasumba yetu:
-CUF chama cha kidini
= CUF ni chama cha Waarabu
= CUF kinataka kuleta usultani
-CUF viongozi wake wabaguzi
Mpaka hapo wananchi wa Bara watakapoondokana na dhana hiyo iliyojengwa makusudi na CCM hata wapate pesa za EPA CUF wataendelea kusuasua tu Bara.
si kwamba hawakupata bali hawakupewa kwa uleule mtindo wa kubadilisha matokeo ,CUF ilishinda karibu sehemu zote walizosimamisha mbunge ,lakini tume ya Uchafuzi ndio iliorudi na matokeo wanayoyataka wao.
Mkuu mbona unakidhalilisha chama chako? Chama makini lazima kiwe na njia za kulinda kura zake. CUF inashindwa kufanya hivyo?
Kauli zako zinabishana zenyewe! But Kanyaga twende tutafika tu