Bw. Ngekewa na Mheshimiwa mwenzio mnaonekana hamtaki kusaidia kujibu suala lililowekwa katika bandiko hili. Hivi ruzuku hutumikaje kwa mintarafu ya kuendeleza Chama (CUF) huko Tabora, Tanga na Dodoma na kwengineko. Ama mimi nasema hata huko Kitovuni (Pemba) ruzuku haijaonekana ikitumika kutengeneza majengo ya matawi katika hilo eneo ambalo CUF tunaambiwa inapata kura asilimia zaidi ya thamanini.
Sasa bandiko feki inabidi lijibiwe kifeki ,ruzuku Lipumba na seifu haiwatoshi vipi wataipeleka kwengine,wanachama wenyewe wajenge matawi yao,si wao ndio Chama Chao ,ruzuku ni rushwa kutoka kwa serikali CUF wanairudisha hawaipokei.
Barua ya asili ilikuwa imerudisha ruzuku ila msajili akadai kilichorudishwa ni kidogo ndio akaonyesha feza yote iliyotoa tokea 1995 kwa maana feza iliyorudishwa haikutimia.