Kwa maana nyingine mnataka kusema kuna ufisadi ndani ya CUF ,hapo mtakuwa sio mmepotea dira tu ,bali hata mnakokwenda hamkujui ,maana ukipoteza dira unaweza kubahatisha na kusema labda ni huku au kule.Nyinyi hampo mawazo yenu yamefilisika na kuona kuna ufisadi tu ,sasa kuna ufisadi ,haya nini faida mmepata hadi hii leo toka muoneshe na kugawa data za mafisadi naona mnapiga makelele mengi sana kiasi ya nchi kutikisika na wengine kuporomoka lakini data zinaonyesha walioporomoka wamepata pa kukamata na wanapanda juu.Au uongo ?
Fedha ipo na inatunzwa kushinda serikali inavyotunza fedha yake na haitumiki kwenye kampeni kama wengine mlivyopendekeza ,CUF haitatumia fedha kumlaghai mwananchi na kumdanganya au kununua uhuru alionao wa kuchagua kumnunulia kanga au kumuwekea pipa la mvinyo,Wanachama ndio watachangia kampeni za Chama Chao pale sehemu husika na Chama kitatoa sehemu ndogo tu ya kusaidia kama kuna kukodiwa jenerataz na vifaa vyengine muhimu na sio kuandaa masufuria ya pilau ,hilo halipo.
Halafu mnashindwa kuelewa kuwa CUF ni Chama Cha Wananchi tofauti na vyama vingine ambavyo huwa ni vya kundi fulani tu au genge la watu ,kuna vyama kibao havina hata ofisi katika upande wa pili wa Muungano nikikusudia kule Zanzibar.
Ilivykuwa hiki ni Chama Cha Wananchi kama kinavyojulikana kwa lugha yetu ya kiswahili ,wananchi wenyewe ndio wakukiendeleza na si kutegemea feza ya ruzuku na kwa msisitizo huo ndio ukaona Chama kimeenea sehemu kubwa hapa Tanzania ,kwani wananchi wamekipokea kama Chama chao wanachotarajia siku yeyote ile watakiwezesha kukipa dhamana ya kuwaongoza na kuwakata vichwa hadharani mafisadi wote pindipo watakuwa na hatia ya kuhujumu core ya uchumi wa Tanzania ,hivyo wataishia jela milele ikiwa watashindwa kurudisha senti tano ya mwisho wa fedha waliyokwiba au kuhujumu na kama haitoshi mali yao yote sio itasimamishwa bali itafilisiwa.
Kuna mtu amesikika akisema kuwa CUF haina mbunge hata mmoja T/Bara ni kweli inawezekana hivyo kwani ndivyo ilivyopangwa na Sultani CCM maana Sultani CCM ndio mwenye kushika vyombo vyote vya nchi hii ,anaamua na kupanga atakavyo hakuna wa kumzuia ,polisi wanafuata amri yake,majeshi wanafuata amri zake mahakama wanafuata amri zake ,sasa unategemea nini kama hao wengine sio walishinda ,bali waligaiwa hizo nafasi za ubunge ,huo ndio ukweli ,nafasi hizo wanazoringia ni za kugaiwa kutokana na mipango ya Sultani CCM ili atumie nafasi hizo kujificha ,kuna wangapi waligombania nafasi na hata kura yao haikuonekana kwa maana walipata sifuri ,inamaana hata yeye mwenyewe hakujipigia kura ,hapana hiyo ni mipango ya Sultani CCM kudhoofisha upinzani na kuudhalilisha ,wapi tunaelekea ni katika kuidai katiba mpya ya Nchi hii ,hili si lakulichezea au kulifanyia mchezo ni jambo la kufa na kupona ikiwa tunataka haki itendeke ni lazima Katiba ibadilishwe ,mahakama ziwe huru na hizi tume za kila siku ziwe huru ,zaidi ya hapo Sultani CCM kwa kutumia mawakala wake aliowapenyeza kila sehemu ndio watakuwa wakitupangia matokea na wakijaza kasumba waTz kuwa bila ya wao nchi haitakalika ,siku moja hii ruzuku itakuja kugomewa kwani inaonekana ni rushwa wanayopewa vyama vya upinzani ili kutishiwa kukoseshwa ruzuku ikiwa watasimama kidete ,ni wakati tu ndio tunaokwenda nao.
Naona Pro Safari ameaanza ,sijui ndio haya aliosema atayaandika hadharani ,aloo ataandika mengi sana na kutoa nyaraka nyingi sana ila ndio hivyo ameshapigwa na chini,sasa ndio anakata roho ,na inaonyesha alikuwa na agenda ya kuzivalia njuga hizi fedha ,ni hatari sana ,amemulikwa na kukurupushwa.