Sasa mnapiga makele wakati Wapemba wametishia tu ,ila kama wakifanya kweli itakuwaje ,tato mnachanganya hisia na ujumbe wanaowakilisha WaPemba,ionekane tu kuwa wanachokitetea Wapemba kinagusa Taifa zima,shida na taabu wanazozipata wao zimejaa na kuenea Tanzania nzima ,kunatokea malalamiko kuwa mahospitali hakuna dawa,mashuleni hakuna walimu wenye kiwango ,na huduma nyengine mbovu kila kona ya Tanzania ,na yote haya yanatokana na utawala mbovu wa CCM ,mtu anaweza kusema ndani ya CCM si wote wabovu nakubaliana nae,ila ndani ya Serikali na vigogo wa Chama kumekuwa na rushwa ya kitaifa na kimataifa ,hivyo hata awemo ndani ya CCM kiongozi mzuri mbio zake zitakwama au juhudi zake zitakwamishwa.
Pemba ni kisiwa kidogo sana hivyo shida na madhila yanapotokea huwakumba watu wote tena kwa wakati mmoja ,maana ikizima genereta moja basi ndio Pemba nzima hakuna umeme usitegemee kama mtaa wa pili au mkoa mwengine kuna umeme ni pemba nzima halikadhalika na maji nayo ndio hivyo hivyo ,yaani mtoto alimuuliza baba yake ..eti baba CUF imeshinda ,,,baba akauliza kwa nini mwanangu...mtoto akamjibu baba yake kuwa nimeona maji yanatoka kwenye bomba !!!
Unajua kama watu wa pemba hivi sasa wamekaa kama mabundi mchana hawaoni vizuri lakini usiku utawashangaa wanavyoona na kukatiza njia za vichochoroni ,yaani mtu anaendesha baiskeli kwenye kiza totoro na anakwenda spidi.Dhiki za maisha zimewafanya wabadilike na hali ya mazingira.