Elections 2010 CUF wazindua kampeni 2010

Wana tofauti kubwa sana na chadema. CUF hawana tofauti na CCM - angalau safu ya juu ya uongozi wa ccm na safu ya juu ya uongozi wa CUF
Kwa hiyo unatuthibitishia kuwa CHADEMA ni chama cha kikristo!?
 
Kwani CUF ni chama cha Kidini ama Kisiasa?

Cha kisiasa mkuu,
so far naona CUF wameenda vizuri kwamba wapo against CCM, hebu tusubiri tuone kama watakishambulia Chadema na kwa kiwango gani na kwa sera zipi, hapo ndipo tutakijaji chama hiki kinakuja na mlengo gani?
 
Prof Lipumba anamwaga sera hapa..anakosa ahadi ambazo ccm walizitoa kama zimetekelezwa au laa?!
Maisha bora kwa mtanzania...
Ajira kwa wananchi
Bei za bidhaa zimepanda sana....
 
Ah ah ah ah kwa hiyo Chadema wao siku ya sabato au sio?

Leo nimekupiga bao loooh unaona aibu mtu mzima, Jamaa wametoka Msikitini wakaenda kwenye kampeni haina shida.....yote siasa! Ila muache chuki CUF jamani.
 
Kimerushwa kijembe kwa CCM kuwa chini ya kamanda said miraji haanguki mtu Jukwaani...Hakiiiiiiiiiiiiiiiiiii
.

Nina hofu kwamba hivi vijembe vikiendela kwa mgombea wa CCM vitamsaidia zaidi kupata kura kuliko kumuangusha. Binadamu wameumbwa na huruma hususan wakati wa magongwa kwa sababu hakuna ambaye hataumwa au kufa. Wasiwasi wangu ni kwamba tukielekeza tafakuri zetu zaidi kwa tatizo lililompata kikwete pale jangwani badala ya sera haitakisaidia chama CUF.
 
Leo nimekupiga bao loooh unaona aibu mtu mzima, Jamaa wametoka Msikitini wakaenda kwenye kampeni haina shida.....yote siasa! Ila muache chuki CUF jamani.
Pole sana ungejuwa msimamo wangu wala usinge kurupuka kuyasema hayo yote... pole sana kijana!
 
Naona wengine watakuwa kidongo chekundu ila ki mwelekeo JF imekaa kichadema chadema tu ngoja kesho wakizindua utaona thread zitakavyogongana

senetor, umenena mtandao wa Chadema hapa JF mpana inabidi tufanye kazi ya zaida kuubomoa. Kesho tusubiri uzinduzi rasmi wa chadema utaona posts zikimiminika kama mvua na ole wako uzipinge utashambuliwa kama nyigu.
 
Hivi umeelewa swali au unakurupuka kujibu tu... wacha jazba elewa maandishi kabla uajibu!

Kulikuwa hakuna swali hapo. Ilikuwa statement yenye alama ya kuuliza mwishoni (kinafiki kama kawaida yako).

Kama kuna swali liulize na usikurupuke kutoa mapovu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…