CULTURE YA NCHINI MAREKANI ILIVYOITEKA AFRIKA KUPITIA MUZIKI TOKA ENZI HIZO..

CULTURE YA NCHINI MAREKANI ILIVYOITEKA AFRIKA KUPITIA MUZIKI TOKA ENZI HIZO..

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
OLD MEMORIES OF BLACK HIP HOP CULTURE & ELEMENT IN
AFRICA... WAY BACK 🔙 1980 - 2005 ...


Historia ya Muziki wa Rap / Hip hop Duniani 🌎 inatueleza kuwa Asili ya Muziki wa Rap ni 🌍 Afrika.

Wasanii Kutoka Taifa la marekani wanaofanya muziki aina Rap ..
wengi hupenda/ tunapenda kuwaita " 🖤 Black American...


Aina Hii ya Muziki ilianzishwa na " wamerekani weusi " ili kupinga ukatili ambao ulikuwa unafanywa na wazungu kwa watu wenye Rangi nyeusi..

Maana wazungu walikuwa wanawafanyia vitendo vya kikatili lakini real mc's ( 🖤 Black American people) waliokuwa wanafanya Muziki aina ya Rap..

Kupitia Tungo / lyrics kali zenye ujumbe..
Waliweza kulikemea jambo hilo kupitia Muziki aina ya Rap kwa kutoa Nyimbo na kupeleka radioni , wengine walipata fursa ya kufikisha ujumbe kuhusu ukatili huo kupitia majukwaa makubwa yanayopinga ukatili huo.


Yaliandaliwa matamasha na wasanii wa Hip hop waliparform na kufikisha ujumbe kwa jamii na viongozi juu ya ukatili uliokuwa unafanywa na wazangu..

Kuna sprit fulani ambayo tuliipata sisi kama waafrika juu ya upanguzi huo wa ndugu zetu uliokuwa unafanywa wazungu Dhidi ya Waafrika wanaoishi ughaibuni..

Na movement mbalimbali zilizilianzishwa nk...

Muziki wa Hip hop umetumika sana kufikisha ujumbe au message kwa jamii kuhusu jambo fulani.
Ujumbe kwa wanasiasa , viongozi wa serikali na mambo mengine yote yasioipendeza & hayana impact kwa jamii..


Kama utumiaji wa Drugs nk..

Kuna kumbuka zimeniijia kichwani nikakumbuka enzi nasoma shule ( shule ya Msingi & sekondari) wanafunzi wengi sana enzi hizo tulikuwa na passion ya kuja siku moja kuwa kati ya wasanii wakubwa wanaofanya Muziki wa Rap na kuendeleza movement za kupiga ubanguzi uliokuwaafanya wazungu Dhidi ya ndugu zetu Waafrika wanaoishi ughaibuni..

Kitu kingine pia nakumbuka baadhi ya wasanii ambao walitu inspire kufanya Muziki nao ni..

50 cent, 2 pac, eve, ashanti , ludacris , Dmx , snoop doggy , ice cube , puff daddy nk.

Kwa upande wangu na wanafunzi wengine kwa miaka hiyo ya nyuma tulifikia Hatua tukaacha kudili na masomo na tukajikita zaidi kuandika lyrics za nyimbo za wasanii kutoka Marekani kama 2 pac shakur, fat joe, rudacris , shaggy , sean paul nk... Katika madaftari yetu ya kuandikia notes za shule Darasani.. notes kwetu zilikuwa ni lyrics ( vise versa tuliandika lyrics za wasanii Hao na kubandika picha za wasanii Hao katika madaftari yetu .. na katika kunta za nyumba tunapolala maghetoni kwetu.

Wengine walijiita majina ya wasanii hao.

Mimi nakumbuka niliitwa " Eminem"
Na kwa kipindi kile ilikuwa ukikosa picha ya msanii kuweka katika kunta za chumbani kwako ulionekana we ni mshamba picha hizi tulizipata kupitia mangazeti ya udaku & sports yaliotoka kila Alhamis & ijumaa...


Unakutana lyrics za nyimbo za wasanii wa zamani enzi hizo na picha za wasanii Katika kurasa za nyuma za mangazeti hayo...

Naimani wengi mnaosoma andiko Hili mnakumbuka vyema.

Pili tulishindana kukalili Mashairi/ lyrics zao na kuchana kila sehemu mtaani wengine tulifikia kipindi tukawa tunajirekondi kupitia 📻 za mfumo wa cassette ..

Ambazo tulichukua bila idhini ya wazee wetu .

Cassette za nyimbo za Muziki aina ya Bolingo ambazo wazee wetu walikuwa wakisikiliza..

Lakini sisi tuliziaharibu na kurekondi Mashairi yetu, wengine tulikuwa tukisikia Ngoma inapingwa radioni Hasa kwa wasanii tuwapendao tulijikuta tulirekondi nyimbo hizo kutokana na mahaba ya kupenda msanii Huyo kupitia kazi zake za sanaa nk.

ingawa tulipata changamoto ya matangazo katikati ya Ngoma tukiwa tunarekondi / jingle za madjs wa kipindi husika ( dj anaehost kipindi) na kupelekea katika nyimbo huwepo wa jingle ..

Kingine Bora ni nikose kipindi " Darasani kuliko kukosa kipindi cha Muziki " show za vijana" katika vituo vya radio enzi hizo mida wa mchana saa 7 - 10 jioni..

Kwa maana enzi hizo djs & radio prisenters walitukosha kwa style yao nzuri ya kuprisente kitu fulani katika show ( vipindi walivyo host) nyaani ilikuwa vibe fulani Hatari..

Bila kusahau playlist za kijanja kutoka kwa madj wakali..

Ni tofauti na sasa sio prisenters wala djs wanaweza kunifanya niache kufanya jambo fulani muhimu nikae kumsikiliza.

Wakati enzi hizo unavunja ratiba zako ili usikilize kipindi cha radio Hasa hivi vya vijana mida ya mchana..

Mimi kitaani nilijikuta wakiniita " mzee wa Top 20 " kwakuwa nilikuwa sikosi kusikiliza show ..

Pia nakumbuka katika mahafali mashuleni pia tulipanda majukwaani.. wengine majukwaa yetu yalikuwa ni juu ya meza .. kisha unaanza kuflow na beat..

Hapo unakutana beat la still by dk. Dre

Unaanza yo yo yo yo🎤🎤🎤🎤🎤🎤 nyani ni hatari ..

Huku vibe likibadishwa na watoto wa kike wakikuita majina yakuvutia...

Hii inshu ya usanii shuleni ilinifanya nipendwe na madem wengi shuleni kila corner hi.." Eminem" coz ndio jina la kisanii nililotumia..

Nilikuwa na t 👕 moja Kubwa sana ya picha ya " Eminem " kila nikipanda jukwaani lazima nivae ..

Mida ya breakfast nimekunya chai Bure kwa kununuliwa na mademu ..

Mida ya runch mchana ndo kabisa...

Kwa mabinti wanatoka mikoani bajeti yake ya kuanzia January hadi juni ziliishia kwangu ( Fedha za matumizi shuleni walizopewa na wazazi Hao)

Na jinsi unavyojua maisha ya Boarding..

( usiulize kama rado )

Mtoto wakike walikuwa hawaoni noma kunibariki kwa kuninunulia chai " breakfast 🥞 " Asubuhi na runch haoni shidah...

Nakumbuka
Ulikuwa unafanyika usahili ili kufahamu ni yupi atapaform siku ya sherehe... Hapa na maanisha Darasa la Saba kwa shule za Msingi na form four kwa shule za sekondari)


Maana enzi hizo kila mwanafunzi alikuwa na ndoto za kuwa msanii sio kwa wavulana wala wasichana..

Ila tuliopewa kipaumbele ni wale walioflow kwa kugha ya kingereza..

Ila pia nakumbuka nilikuwa ni mchoraji mzuri shuleni . Kwahy nilikuwa mchoraji wa picha na maandishi katika ubao.. Darasa ambalo linakuwa limeandaliwa kwaajili ya sherehe..

Utamaduni / culture ya hip hop ilitutesa sana enzi hizo.

Kupitia makala hii una lipi lakukumbuka.

Ukwaju wa kitambo
#tunakurudisha_kaleee!!!
 

Attachments

  • 1726719248604.jpg
    1726719248604.jpg
    181.4 KB · Views: 2
Hivi huyu jamaa ni mzima kweli? hii colour uliotumia hapa inasomekaje sasa? kulikuwa na ulazima gani wa kuweka andiko kwa rangi hafifu namna hii!
 
Back
Top Bottom