Culvin Mavuga: Football Performance Analyst for Simba SC

pakao

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
381
Reaction score
533
Hivi wakuu huyu mtu pale Simba ana faida gani, maana muda wote aliokaa pale Simba makosa ya wachezaji wetu ni yale yale au makocha hawamuelewi na kama hawamuelewi kwanini yupo kwenye hiyo nafasi. Kila nikijaribu kuwaangalia wachezaji wa Simba wanavyojipanga uwanjani ni kama ng'ombe tu hasa hasa kwenye mipira ya kutenga.

Tunafungwa magoli yale yale kila siku, michezaji inakaba kwa macho na wengi wanaduwaa uwanjani. Niseme tu kimataifa hapa tulipofika ni pakubwa sana ukilinganisha na uwezo wa team yetu. Mwisho Pablo ni kocha wa mchongo.
 
Unaonaje ukiichukua Simba wewe na kuwa kocha Mkuu utatusaidia sana kutufikisha Kanani!
 
Itapendeza zaidi ukipewa wewe hiyo nafasi nadhani utafanya kazi bora kabisa ya kumfundisha Pablo namna y kuwapanga mabeki na pia utamwambia Onyango au Banka Inonga aache kukodoa mimacho.

Hebu sasa tueleze kazi za huyu analyst ni zipi na wewe ukifika pale utafanya nini tofauti na anachofanya.
 
Wewe unajielewa, Tena hapo mlipofika Ni kwa kubahatisha ru, yaani timu inachexa mpira mbovu hakuna mfano
 
Nimewahi kuwaza hiki kitu, tangu atambulishwe pale Simba hakuna 'impact' yoyote ameleta kwenye benchi la ufundi.

Nakazia Pablo ni Minziro mweupe.
 
Mavunga ni match analyst au msomaji wa mbinu za timu pinzani kujua udhaifu wao na ubora wao lakini cha ajabu uyu mavunga yeye mara zote anafanikiwa kwa mkapa tu wakipanda ndege kwenda ugenini pengine kila kitu anakiacha dar maana aieleweki mchango wake kwenye mechi za ugenini uwa ni upi, kwenye mechi karibu zote za ugenini simba inazidiwa kila pembe na aina ya upangaji wa kikosi uwezi kusema eti timu inae mtu Kama uyo,,,uyo mtu anakula mshahara wa bure ni bora iyo kazi akaachiwa kocha mwenyewe, na ata mechi za dar anasaidiwa tu na mechi kuchezwa nje ya uwanja na si vinginevyo
 
Mkuu naona umenielewa sana, huyo mavuga hana lolote na kama kazi yake anafanya vizuri basi benchi lote ni la kupiga chini akiwemo mswahilina Matola
 
Waambie hao... Maana Simba wana ujuaji sana. Hili jambo hata siku ile kwenye group letu la Yanga tulijadili afadhali umelileta huku nao simba walione.
 
Wachezaji wetu wanakimbiakimbia tu kama Ng'ombe uwanjani,utafikiri hawana mwalimu poor Pablo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…