mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,188
- 1,090
Kuna biashara kubwa sana (inayohusisha mabilioni ya fedha) baina ya nchi yetu na China, India, Uturuki, Afrika Kusini n.k.
Taifa letu bado ni tegemezi katika kuagiza vitu, vifaa, chakula, nguo na mengine toka katika nchi mbalimbali. Hili linafanya wafanyabiashara wanaoagiza kuhitaji na kutafuta fedha za kigeni haswa Dola ya Marekani kila leo. Bidhaa zinaagizwa kwa dola na kisha kuuzwa kwa fedha ya Tanzania (madafu) na hivyo kulazimu wafanyabiashara kununua dola kwa bei ya soko ili kuagiza bidhaa.
Tatizo linakuja kwenye mfumuko wa bei, uhaba wa dola. Bei ya kununua Dola ya Marekani kupanda kila leo hivyo kuleta usumbufu mkubwa sana kwa wafanyabiashara na mwisho walaji wa mwisho wa bidhaa. Hivi sasa kupata (kununua)dola 10000;20000;100,000;300,000;600,000;1000,000 n.k si jambo rahisi kupitia benki.
Kwa mujibu wa sheria za fedha kimataifa inawezekana kufanya currency SWAP baina ya nchi na nchi. Hili hufanyika kwa Benki kuu za nchi husika kukubaliana kila nchi kufanya manunuzi katika nchi ya mwenzie Kwa kutumia fedha yake.
Mathalani tunanunua nondo China, invoice inakuja katika Yuan na wafanyabiashara kufanya malipo kwa kutumia shilingi sawa na thamani ya Yuan, vivo hivyo Kwa rupees na zingine.
Hili litaondoa utegemezi wa Dola ya Marekani lakini mfumuko mkubwa wa bei unaotokana na fedha yetu kushuka thamani pia fluctuations.
Yawezekana IMF na World Bank wakawa Kikwazo katika kufanikisha hili lakini naamini watendaji na viongozi wetu wakiwa shupavu tunaweza.
Uimara wa biashara na wafanyabiashara ndio uti wa mgongo katika maendeleo ya nchi pamoja na ustawi.
Heri ya Miaka 60 ya Muungano kati ya TANGANYIKA na Zanzibar (Unguja na Pemba).