Customer care Exim Bank ni mfano mzuri wa kuigwa...

Customer care Exim Bank ni mfano mzuri wa kuigwa...

queenkami

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2010
Posts
1,694
Reaction score
1,249
Kila mmoja wetu anajua jinsi asilima kubwa ya customer care ya ofisi nyingi za Tanzania ilivyo mbovu.Kila siku tumekua tukilalamika jinsi wafanyakazi wa huduma kwa wateja walivyo na lugha mbaya na dharau kwa wateja.

Ila tusiwe watu wakuandika pale tunapoona mabaya tu,wanaofanya vizuri tuwasifie ili wazidishe juhudi na wanaofanya vibaya wajifunze.

Kuna uzi fulani humu unazungumzia Dollar account,ule uzi ulinivutia na mimi na baadhi ya wakuu fulani tukahamisha mazungumzo PM mwishowe nikaamua kuchukua hatua ya kufanya kwa vitendo.Nikawapigia simu Exim bank.Nilipowapigia kwa mara ya kwanza nilifurahi sana jinsi mhudumu wa huduma kwa wateja alivyonipokea vizuri.Nimeongea nao zaidi ya mara moja na nimeongea na wahudumu tofauti tofauti na wote wana lugha nzuri sana.

Mimi hao ndio nimejisikia kuwasifia leo.
 
wanaofanya vizuri tuwasifie ili wazidishe juhudi

bank teller wa NMB alishwahi kuniongezea sifuri nyuma ya kiwango halisi nilicho deposit from 260,000. to 2,600,000.
she's the best teller i have ever met. japokuwa ili nisababishia usumbufu baadae ila yule dada namshukuru sana ni mfano wa kuigwa na azidishe juhudi.
 
Hongera.
Na siku atakapopunguza sifuri moja iwe 26,000 badala ya 260,000 uje umsifie pia ili aongeze juhudi.
 
Kila mmoja wetu anajua jinsi asilima kubwa ya customer care ya ofisi nyingi za Tanzania ilivyo mbovu.Kila siku tumekua tukilalamika jinsi wafanyakazi wa huduma kwa wateja walivyo na lugha mbaya na dharau kwa wateja.

Ila tusiwe watu wakuandika pale tunapoona mabaya tu,wanaofanya vizuri tuwasifie ili wazidishe juhudi na wanaofanya vibaya wajifunze.

Kuna uzi fulani humu unazungumzia Dollar account,ule uzi ulinivutia na mimi na baadhi ya wakuu fulani tukahamisha mazungumzo PM mwishowe nikaamua kuchukua hatua ya kufanya kwa vitendo.Nikawapigia simu Exim bank.Nilipowapigia kwa mara ya kwanza nilifurahi sana jinsi mhudumu wa huduma kwa wateja alivyonipokea vizuri.Nimeongea nao zaidi ya mara moja na nimeongea na wahudumu tofauti tofauti na wote wana lugha nzuri sana.

Mimi hao ndio nimejisikia kuwasifia leo.

Wana mwezi watatu sasa exim master card hazifanyi kazi online ...
 
EXIM wanasitahili pongezi, niko nao sasa ni mwaka wa sita

sidhani kiivo kwani rafiki yangu mpaka sasa hawajamrudishia hela yake iliibiwa kwenye account yake hapo exim so now for me hata wafanye mema mia nshawaona wezi tu..
 
Wana mwezi watatu sasa exim master card hazifanyi kazi online ...

sidhani kiivo kwani rafiki yangu mpaka sasa hawajamrudishia hela yake iliibiwa kwenye account yake hapo exim so now for me hata wafanye mema mia nshawaona wezi tu..

Ni wazuri ila ATM zao mara nyingi hazipigi mzigo...hasa wikend.

Wakuu mnafanya vizuri kuelezea kasoro walizo inaweza kusaidia wakaboresha kama wanapitapita huku.
Ila mada yangu inahusu kupongeza customer care japo pia wana mambo mengine mengi mazuri.
 
Huduma yao itakuwa ni nzuri kati ya Branch na Branch ila si kwamba ni nzuri kwa Tanzania nzima,

Mwaka jana nilitaka kufungua acount tawi la Mtwara nilichoambulia kwa yule mhudumu nilitoka spidi na sirudi tena ktk majengo yao popote. Kwa bahati nilipata benki flani muafaka kwangu.
 
Exim temeke BrancH wamefunga Account yangu kwa maelekezo ya police without my concernt. Kuna kabalance kangu huko mwezi sasa nahangaiKa nao wanifungulie nikakwangue wapi. wananiambie niende Police nikapate maelezo na mimi naogopa police kama maana cjui hata kuna issue gani sijui. Wahuni tu Exim
 
Wameshatengeneza menu system ya ATM zao?

Nishawahi kuambiwa kuna network error kumbe kisa nimetaka kutoa fedha nyingi kwa mkupuo.

Nilivyopunguza kiasi ATM ikafanya kazi poa tu!
 
Wameshatengeneza menu system ya ATM zao?

Nishawahi kuambiwa kuna network error kumbe kisa nimetaka kutoa fedha nyingi kwa mkupuo.

Nilivyopunguza kiasi ATM ikafanya kazi poa tu!
Kiranga mimi nina fixed account na sio muda mrefu hivyo matatizo yao mengi mnayoyasema sijakumbana nao.
 
Last edited by a moderator:
Labda hujataka kutoa hela "nyingi" kama Kiranga.

pesa yenyewe iliyowekwa hata mkononi haijai hiyo nyingi yakutoa hadi ATM iseme network error itatoka wapi ndugu yangu.
Habari yako lakini.
 
pesa yenyewe iliyowekwa hata mkononi haijai hiyo nyingi yakutoa hadi ATM iseme network error itatoka wapi ndugu yangu.
Habari yako lakini.

Hahahaha,

Habari yangu nzuri zaidi sasa nimecheka. Umenifurahisha sana.

Angalau naweza kujitapa nimekuja bongo nikataka kutoa fedha "nyingi" ATM mpaka zikasababisha "network error".

Thamani ya mtu kazi, pesa ni matokeo.

Hivi kuna watu wanaamini hivi bado?
 
Kweli mkuu mabank mengi yaende kujifunza kwao hata kama unaweka buku 2 kwao wewe ni mteja mhimu.
 
Ndugu yangu alipatwa na personal emergency issue. aliniomba nimtumie mshiko via Moneygram ili atatue matatizo yake nyeti ASAP. Alipoenda Exim branch akaambiwa system iko down na jamaa ambaye huwa anai-fix yuko off hadi 2 days later. 3 days later alipoenda tena akaambiwa jamaa hajarudi na ajaribu kesho yake. Hakuna moneygram agent anakoishi ndugu yangu zaidi ya Exim bank. Aliporudi kesho yake akaambiwa ajaribu wiki ijayo. Ndipo alipoamua kupanda basi mwendo wa masaa 6 kuja mjini. Exim bank sucks!!
 
Back
Top Bottom