Customer Care yetu waswahili- Fastjet wanabore

Mihayo

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2010
Posts
268
Reaction score
63
Nipatwa na msiba wa aunt yangu. Jana kutokana na pilika za ofisi nika amua kununua ticket online. Nikalipa kwa mpesa leo nadamka asubuhi kuelekea mwz nafika airport nikaona niprint ticket, kwenda dirishani my God" Ticket yako haipoinaonekana ulikosea na sina jinsi ya kukusaidia kama una pesa nunua nyingine" Dada sasa hivyo visenti vyangu ya return itakuwaje, Itarudishwa. Watu wengine bwana..... Duh nikapapasa nikalipia one way nikoon board lakini lazima nipambane na huyu mdada fedhuli. Nimepewa nkmber ya supervisor nikishuka tu namtwangia. But mwenye number ya MD hapa anirushie au ani pm. Kaharibu mood yangu asubuhi yote hii. Wakikosa kazi wanaenda kwa waganga kuroga, wakipewa kazi taabu tupu nani katuroga sisi wabongo?Shame on that ....lady
 
Hii post inatia wasiwasi.
Maana ni kesi ya kusikiliza upende mmoja
Kwa jinsi ulivyoandika na muonekano wa maneno hapo juu inaonekana nawe ulikwenda kwa jazba,na yule binti habari zakufiwa hajui ,maana kila abiria anasafiiri na matatizo yake na wala hakuna ticket inaandikwa huyu amefiwa au huyu mgonjwa.Watu wote mnakuwa treated sawa unless specified.
Ulipaji wa online unakukosea kwa namna nyingi:
-Kwanza utumaji wa pesa kiukamilifu
-Kukosea Jina wakati wa ku place booking
-Kuingiza details zako kwa makosa

Sasa unapofika Airport na pale inakuwa staff yupo busy na watu tunatabia tofauti,sasa kuanza kushughulikia tatizo lako ambalo anaweza kuona kwamba ni kubwa litafanya abiria wote wasubiri au folen iwe kubwa.

Na pia inashauriwa sana kuwahi mapema ili hata Staffs pale Airport waweze kukupa msaada na ku manage time.

Sasa inawezekana uli report muda wa kiswahili na ukaenda pale na tempa zako then na yeye akawa kaamka kama alivyoamka ndio habari ikawa hivyo.

Pesa zako hazitapotea,maana naimani zitakuwa zipo kwenye record zao au za kampuni ya sim au bank husika ila pia angalia Temrs and Conditions kwenye website yao kabla hujaamua kubook na Airline yoyote ili kujua ni pesa ipi inakuwa refundable.

Na hii si issue ya MD,ni issue ndogo sana unaweza kupata msaada kwa Branch yao yoyote tu.
Muhim nenda in person na usitumie siimu
 
suppose angekua hana hela nyingine ya kulipa? halafu na wewe unafuga uzembe! huwezi sema eti anaudumia wengine...ina maana akimsaidia huyu jamaa atakua hatoei uduma? kila mtu ana haki ya kuhudumiwa tatizo lake hadi mwisho!
 
Inaonekana hujanielewa.
Angekuwa hana hela nyingine sio tatizo la Airline,ni tatizo lake.Angebaki tu hakuna kusaidiwa kupanda ndege bure wakati tatizo halijaainishwa.

Sasa we unahukumu vipi kesi kwa kumsikiliza mtu mmoja tu,na unajua alipoenda pale na yeye alikuwa kwenye mood gani.
We unafikria mtu atapost humu alichofyatua na yeye pale.
Kusaidiwa kuna taratibu zake,sasa we unasema asaidwe je umeona hapo juu ameweka wapi wazi sababu ya kukosea.
Kama mtu ni mzoefu wa kusafiri kwa ndege huwezi kuhukumu moja kwa moja maana kunavitu vingi unawza kukosea na vikawa havihusiani na wao kama airline moja kwa moja.
Kuna makosa unayaona ni madogo ila kuna Baadhi ya Airline ukikosea hata herufi kwenye Jina na ticket ikiwa issued ni lazima ulipe Pesa ya kubadilisha Jina

Hembu muulize mwenzi hapo kwamba alikosea nini ndio uingilie maongezi
 
Huu mjadala mzuri sana na mimi ningependa nishiriki. Swala la kuwa na customer wengi sio issue kabisa, huyu mdada alitakiwa ampe huyu client muda wote unaohitajika kupata suluhu ya swala lake. Swala la kuwa na wateja wengi halimuhusu mteja, kampuni kwa kujua flow ya client wao wangetakiwa kuwa na staffing ya kutosha kukidhi haja zao. Kumwambia mteja akate ticket nyingine ni kumbebesha tatizo mteja na dhana nzima ya mteja ni mfalme imezikwa. Kampuni hii ilitakiwa impe mteja wake benefit of doubt, kwanza kwa kuomba aonyeshwe hiyo ref number na automated communication kwa kuangalia message iliyotoka fastjet. Tatizo sisi kama wateja pia hatujui haki zetu, katika nchi ambazo vyama vya walaji vinatambulika na vina nguvu, huyu bwana angedai usumbufu na embarassment na kampuni ingemlipa. Hili sio tatizo la fastjet tu, ni kwa makampuni mengi sana ya hapa nchini, hata zile za nje zinazofanya vizuri duniani zikija hapa kwa kujua kuwa watanzania ni wajinga, zinafanya shaghala baghala, tunachotakiwa kwa sasa ni kujiunga kwa wingi na vyama vya walaji ili kuvipa nguvu. Leo hii angalia kampuni za simu zinavyofanya uharo, unaweka kabang haiingii ukiwafuata hadith ndefu, uki scratch voucher ukaharibu huoni namba unaenda kwao wanakujazisha makaratasikibao na kukwambia usubiri processing ya mwezi mmoja, angalia ma benki, foleni hazieleweki na ukiuliza madirisha yenye matundu 7 wanaweka mhudumu mmoja au wawili, why? kwa sababu watanzania tumegeuzwa mamburukenge, kichwa cha wendawazimu na shamba la bibi, tukatae jamani
 

Fastjet wana email adress kama una malalamiko unaweza kuwaandikia kupitia Customer.Tanzania@fastjet.com watakusaidia na kama kuna makosa upande wa mfanyakazi pia watachukua hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…