Pole sana kwa fundi kukuingiza hasara sababu ya ujinga wake huyo fundi.
Mimi magari yangu napeleka kufanya service kwenye hizi filling stations na haswa PUMA, oil na vifaa vyote nanunua mwenyewe na wakati gari linafanyiwa service nasimamia.
Epuka kuwaamini mafundi. Nilishakutana na issues tofauti kwa kumuachia fundi gari atengeneze.
Mojawapo alifanya kazi ya kubadilisha break pads na bushings nikamuachia gari sababu nilikuwa busy na kazi, akanirudishia gari jioni. Asubuhi najiandaa kusafiri nalo nakagua nuts za kwenye matairi nakuta nut 1 haipo, nampigia anadai ilikuja hivyo hivyo wakati yeye ndiye alikuwa mtengenezahi wa ilo gari siku zote, baadae akasema hapo nut aifungi stadi yake imeharibika. Nikamwambia sio kweli, tukutane dukani tutafute, tukakutana akapata alafunga ikafunga.
Issue nyingine nikapeleka kwa fundi kufanya matengenezo ya gari kubadili break pads, bushings na vitu vingine, kesho nikasafiri km zaidi ya 1,000, uko ugenini kulikuwa na mlio kwenye mguu wa mbele, nikapeleka kwa fundi wakati wa kufungua Nats za matairi, nuts 3 za tairi la upande mmoja zilifungwa vibaya, ilibidi afungua kwa kulqzikisha ila zile stadi zikawa zimeharibika nikaingia gharama kwenda kununua stadi zingine 3 ambazo nj Genuine. Nikasema kama ningepata panchayat njiani ingekuwaje alafu inanipatia nikiwa porini.