CWT 'imewauza' Walimu?

Mkwanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,293
Reaction score
5,163
Kutokana na hukumu iliyotolewa na Mahakama juu ya mgogoro wa waalimu na serikali, nashawishika kusema kwamba Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT) chini katibu wake Mukoba kimeamua kuwa uza waalimu kutokana na sababu zifuatazo;
1. Sitaki kuamini kwamba CWT hawakujua matokeo ya wao kupeleka hati ya kugoma serikalini siku zitazoangukia mapumziko na hivyo kuipa serikali nafasi ya kwenda mahakamani kutengeua mgomo. Hili ni kosa la 'kitekinikali' lililofanywa makusudi ili kupoza hasira za waalimu na wakati huo huo kuifavor serikali
2. Sijawahi kuwa na imani kuwa Mukoba ana dhamira ya dhati ya kushughulikia madai ya waalimu kama mnakumbuka kikao kilichofanyika mwaka 2009 (sina uhakika sana) pale diamond jubilee na kuambulia kipigo kutokana na kutaka kuwaviriga waalimu waliokuwa na msimamo thabiti juu ya madai yao
3. Maelezo ya mwanasheria wa waalimu ambaye aliiwakilisha CWT mahakamani yanaonesha kabisa alijiandaa kushindwa kesi kwani alijua maamuzi ya mahakama yatavyokuwa baada ya wao kufanya kosa la kitekinikali

NB. Haya ni maoni yangu huru na naamini maelezo ya Mukoba hapo baadae hayatakuwa na jipya zaidi ya kusalimu amri ya mahakama kwani ndivyo walivyokuwa 'wamepanga'
Waalimu mpo?
 
Kwani sheria inasema unapotaka kugoma na kuserve notice kwa mwajiri usifanye hivyo siku inayoangukia mwisho wa juma? Hapa tutoe mchango kwa kuangalia sheria inasemaje. Na je common laws zetu zinatoa mwanya wa kutumia reasonableness au zimekaa kimya kwenye mambo kadha wa kadha. Nawakilisha. Lakini kitu kingine hii kitu inaitwa CMA imeghubikwa na matatizo lukuki na imekuwa ni kichaka cha waajiri kuficha uonevu na ukandamizaji wa haki za wanyonge
 
"Myonge mnyongeni" Hiki ndicho kitu serikali inachowafanyia watumishi wake.
 
Serikali ijue kuwa inaweza kuwalazimisha waalimu kurudi kazini lakini haiwezi kuwalazimisha kufanya kazi yao kwa dhati!! Matokeo ya mgomo baridi wa waalimu utakaondelea nchini yatakujakujitokeza kwa kukosa ubora kwa wanafunzi siku za usoni na hii itakuwa legacy ya utawala wa mkwereee!! Anathamini zaidi kushinda chaguzi kuliko kuwaletea maendeleo wananchi!!!
 
Mukoba bado tuna imani kubwa na wewe safari hii umefanya kile walimu wote wenye kutumia vichwa vyao wanataka .
Endeleza mapambano sisi walimu tuko mbele yako wewe kama kamanda wetu.
Nafikiri safari hii ujumbe umefika ipasavyo hata kama hawataukubali ila utakuwa umewaingia
hakuna kifungu chochote kinachoeleza muda na siku ya kutoa notisi kwa mwajiri.
Wao wana mahakama sisi tuna mungu hawezi kututpa waja wake kilio cha wengi lazima hakisikie.
mshikamano daima hadi kieleweke wamezoea kutunyanyasa sasa basi imetosha walimu
SAFARI HII TUTAWAFUNDISHA MAANA YA MWALIMU
BAAD
Baaddh
 
Chama cha walimu tanzania kimewataka walimu kurejea kazini kama kawaida.SOURCE ITV BREAKING NEWS
 
Nilisema kuwa walimu hawataweza mgomo wamesha fikiria safari ya mwabepande!
 
Kama kweli hawa viongozi wao ni zile pandikizi za serikali
 
Kama kweli hawa viongozi wao ni zile pandikizi za serikali

Warejee kazini ...enhe malizia basi.. au hujasikiliza vizzuri breaking news? Yaani baada ya kurejea kifuate nini?
 
Huyu jamaa ninapomuona akitembelea shangingi la CWT, huwa napata hasira sna.
 
KakaJambazi acha ujinga,unataka rais CWT atembelee gari ya nani?.Kwani ananunua kama njugu?.Kina vyombo vya maamuzi makao makuu ya CWT, acha akili tope hizo.Mie namfagilia Mukoba amejaribu katika mazingira magumu haya na kafanikisha mgomo japo wahuni wachache wapambe wa serikali wanaodhihaki.HUREEEEEEEEEEEEEEE MUKOBA, HUREEEEEEEEEEEEEE ----------------CWT.
 
Last edited by a moderator:
Mbona mahakama nayo iliwahi kufanya kazi usiku wa manane katika mgomo ule wa walimu?
 
NI MKUMBUSHE MTOA HOJA KWAMBA MUKOBA NI RAIS NA SI KATIBU.Ila kidogo walimu mwaka huu mmeonyesha kwamba mnaweza ila mnaihurumia serikali na raia wake naamini wakati mwingine Kikwete akisikia walimu wanataka kugoma atatia adabu.Mukoba sio mbaya sana kutii amri ya mahakama ila najua huko kwenye mazungumzo wenyewe watakuogopa.Naomba umuambie JK kwamba walimu wanachotaka ni si mishahara mikubwa ila ni posho kama sekta nyingine.
 
mkwanzania inaonekana una chuki binafsi kwa sababu hata hujui mukoba ni nani mpaka ukaamua kumpa cheo cha UKATIBU wa CWT wakati yeye ni rais wa CWT. Pili mwaka 2009 serikali yenyewe ilienda mahakamani siku ya jumapili usiku sasa mwaka huu wameshindwa nini kufanya hivyo???
 
From the trend of things maoni yangu ni kuwa CWT imeanza kupoteza credibility yake kutokana na kufanya kazi kama corporate body hivyo baadhi ya waalimu mikoani kuanza kujitoa toka chama hicho na kuanzisha chama kingine. hivyo basi hawa ma cream wa CWT ili wa survive ni lazima kitu kama hiki kifanyike katika kipindi hiki vinginevyo kina mukoba[mtaniwia radhi kama jina nimekosea] wanapigania matumbo yao. Ni kweli waalimu kutokana na wingi wao na uwepo wao kwenye remote places na bureaucracy iliyokuwepo wana matatizo lakini matatizo yao siyo makubwa kama yalivyokuwa miaka ya nyuma.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…