Niseme kitu wandugu. toka nimeanza kazi, kwashida zangu nilifanya kazi miezi nane serikalini bila ya mshahara, wala malipo yoyote yale kutoka serikalini. katika miezi hiyo nane nifamilia yangu ambayo ilikuwa nauelewa waliweza kunisaidia ku ishi katika kipindi hicho chote.
Hiyo mnayo iita CWT saut ya mwalimu sikuwahi kuiona wala kuisikia katika kipindi hicho chote cha miezi nane. na nakumbuka kuna siku niliwahi kwenda halmashauri kudai baadhi ya madai hao CWT walikuja halmashauri wakatuambia mimi pamoja na wenzangu hawana uwezo juu ya madai hayo kwani wao si azina hivyo tukomae tu kudai eti tutalipwa kama tukikomaa,wakawasha gari yao wakaondoka.
Chakushangaza baada ya miezi nane tena kwenye mshahara wangu wakwanza kabisa nikawakuta tayari nao wameanza kukata asilimia zao. na wananletea tisheti siku ya mei mosi. nilikaa nika jiuliza maswali kadhaa ambayo mpakaleo sija pata majibu.
1. hivi ha CWT wapo na mwalimu siku akiwa na furaha tu? maana wakati sina mshahara sikuona hiyo sauti ya mwalimu, baada ya kupata mshahara ndo sauti inaonekana, kweli ni haki?
2. himichango inayo katwa kwa waalimu zaidi ya laki mbili kila mwezi sh 12000/= imewasaidiaje waalimu? au nichanzo tu chama pato ya watu. kwa mpiga mahesabu hemu piga unambie hawa watu wanakusanya sh ngapi kwa mwezi na wanafanya nini namapato hayo?
3. wamejenga maghorofa katika baadhi ya mikoa je mapato ya maghorofa hayo yana fanya nini sasa au yanapangiwa kufanya nini?
waalimu sisi niwatu wakushangaza sana. ukijidharau wewe hakuna atakaye kuheshim. nimegundua sekta hii ya waalimu tukubali tusikatae wengi tunaelimu za kuunga unga na nafasi zimepatikana kwa kuunga unga, yaani tunamatokeo ovyo. ndio maana tu nakauoga flani hivi wakati wakudai madai kwani waweza ambiwa huna sifa toka kazini
pili wengi ni masikini. tunatoka katika familia masikini sana ndio maana tuna nyenyekea angalau kupunguza umasikini tulio nao.
tatu nikwamba, mfumo wa kiutawala uliopo nao kwa namna moja au nyingine umechangia sana kutufanya tulivyo.
ukitaka kujua ukweli wa haya waulize waalimu kwenye mgomo wa mwaka jana baada ya tamko la bosi kunaaliye bisha! lakini fatilia nchi za wenzetu waalimu waki azimia jambo ni wame azimia kweli!
kwa ushauri wangu CWT simtetezi wa wanyonge bali ni fuko lawatu la kujichotea pesa ya wanyonge. naunga mkono kwanza kuwepo na vyama vya waalimu ngazi tatu tofauti. primary, sekondary na vyuo vikuu. kila chama kitetee watu wake kulingana na mahitaji ya watu wake na ndiyo maama hata ufundishaji katika ngazi hizo ni tofauti
nyie mnao sema kuirekebisha CWT, unabadilishaje chama ambacho hata kadi huna ila kina kukata makato.na ukienda ofisi zao hakuna jipya zaidi ya dana dana tu. kama kweli wewe ni mwalimu fanya uchunguzi utagundua CWT wana agenda zao
by the way nimeamua kufata ushauri wa bosi kwani shule zitakapo funguliwa tena sitakuwa mwalimu nikazi niliyo ipenda nakuifanya kwa miaka mitatu sasa basi imetosha ngoja nikafanye napengine tuone mungu atabarikije
kwa vijana kama mimi mlio anza kazi hii na degree hiyo sio ishu fanya jitihada kaongeze elimu au jijenge katika ujasiliamali kwa kuwekeza kidogo unacho kipata lasivyo uta jenga kwa pesa ya pensheni ambayo nayo utaiangaikia mpaka ukome.
nihayo tu kwa leo