Nguva Jike
JF-Expert Member
- Jan 22, 2018
- 1,226
- 1,757
Habari za muda huu.
Chama cha walimu makao makuu Dodoma chamtelekeza mwanachama wake bila huruma ndani ya jiji la Dodoma.
Hayo yalijiri siku ya tarehe 03.10.2024.Ambapo katika tarehe hiyo mwalimu kutoka Kilindi Tanga (jina na shule anayotoka inahifadhiwa)
Mwalimu huyo alifika Dodoma siku ya tarehe 02.10.2024 kwa usafiri wa Lori la mizigo kwani hakuwa na nauli ya basi.
Lengo la safari ya Dodoma ilikuwa ni kufika ofisi ya raisi-Tamisemi kupeleka malalamiko kadhaa dhidi ya mwajiri wake ikiwemo kutopatiwa stahiki za uhamisho na pesa za matibabu.
Kutokana na ukata aliokuwa nao ikambidi afike Dodoma cwt hq kuomba msaada.Ikumbukwe siku ya tarehe 02.10.2024 alilala booking office za Simba mtoto hakuwa na pesa ya gesti.
APOKELEWA NA MHUDUMU WA HUDUMA KWA WANACHAMA.
Siku ya tarehe 03.10.2024 akapokelewa na mhudumu tajwa na kuamrishwa aandike barua ya kuomba msaada.Alipoandika akapewa majibu kuwa hakuna cash kwa siku ile.
AOMBA HIDADHI YA KULALA AKATALIWA.
Siku ile ile akaomba msaada alale pale ofisini kwakuwa hakuwa na fedha ya gesti wala chakula lakini ofisi ilikataa na ikamlazimu alale kwenye basi siku ya 03.10.2024.
04.10.2024 AONDOKA DODOMA KWA KUUZA SIMU.
Baada ya kukosa msaada ikabidi auze simu ili ajikimu na kusafiri kurudi Kilindi.Ikumbukwe cwt wilaya ya Kilindi haikuonesha ushirikiano wowote kwa mwalimu yule japo wao ndio wenye jukumu la kumsaidia mwanachama wao.Viongozi wenyewe kwa wenyewe pale Cwt kilindi husaidiana kutatuliana shida zao na zinakaa vizuri.Katibu alivyotoka likizo alikwenda kwa ded kilindi akafuatilia shida za mwenzie na akafanikiwa kulipwa stahiki nyingi huku za wanachama wachangiaji wapo kimya.Mungu atashusha adhabu juu Yao amen.
VIONGOZI CWT HQ WAPO BUSY MIKOANI.
Mpaka kufikia tarehe ya leo 13.11.2024 wahasibu na viongozi wa Cwt Hq wapo busy mikoani hivyo kushindwa kumhudumia mwalimu alipe madeni aliyoingia akiwa Dodoma.
CWT YAMPUUZA MWALIMU NA KUJALI VIKAO.
Inaonekana viongozi CWT Makao makuu Dodoma wanajali vikao zaidi kuliko huduma kwa wanachama.Siku ya 03.10.2024 walionekana wakiwa busy na kuandaa mabegi ya vikao huku wakimtelekeza mwalimu Dodoma ambae michango yake ndio inayowaweka hao viongozi mjini.
Hii ni laana wanajitengenezea na napata mashaka na utendaji wao kwa wanachama.
Nawasilisha