DOKEZO CWT makao makuu yamtelekeza mwanachama Dodoma

DOKEZO CWT makao makuu yamtelekeza mwanachama Dodoma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Alissfiri ili akapewe hela Dodoma?! Kama hakuwa na fedha kwanini alilazimisha safari?! Mbona hujaelewa kama alifanikiwa kushughurikia suala lake?!
Wewe hujui adha wanazokutana nazo walimu ndio maana unaongea vima hapa.
 
Inafikirisha sana mkuu stahiki Zake una maanisha mshahara hajalipwa pia vip kuhusu kadi ya bima pia?? Na hana hata nauli wala hela ya kula?? au umeamua kunogesha story kidg.

Any way lkn mimi sio mwl hayanihusu pole ake Mungu amsaidie atimiziwe haja zake

Ndio maana watoto shule za gvt performance huwa ni avarage sana kwa kuwa hakuna motisha
Mwalimu posho yake ni mpaka kusimamia mtihani Tena uchaguliwe sio lazima.... Ama vitokee visemina vya masomo ..mwalimu kukutana na posho ni kama kukutana na trafiki ziwani....
 
Habari za muda huu.

Chama cha walimu makao makuu Dodoma chamtelekeza mwanachama wake bila huruma ndani ya jiji la Dodoma.

Hayo yalijiri siku ya tarehe 03.10.2024.Ambapo katika tarehe hiyo mwalimu kutoka Kilindi Tanga (jina na shule anayotoka inahifadhiwa)

Mwalimu huyo alifika Dodoma siku ya tarehe 02.10.2024 kwa usafiri wa Lori la mizigo kwani hakuwa na nauli ya basi.

Lengo la safari ya Dodoma ilikuwa ni kufika ofisi ya raisi-Tamisemi kupeleka malalamiko kadhaa dhidi ya mwajiri wake ikiwemo kutopatiwa stahiki za uhamisho na pesa za matibabu.

Kutokana na ukata aliokuwa nao ikambidi afike Dodoma cwt hq kuomba msaada.Ikumbukwe siku ya tarehe 02.10.2024 alilala booking office za Simba mtoto hakuwa na pesa ya gesti.

APOKELEWA NA MHUDUMU WA HUDUMA KWA WANACHAMA.

Siku ya tarehe 03.10.2024 akapokelewa na mhudumu tajwa na kuamrishwa aandike barua ya kuomba msaada.Alipoandika akapewa majibu kuwa hakuna cash kwa siku ile.

AOMBA HIDADHI YA KULALA AKATALIWA.

Siku ile ile akaomba msaada alale pale ofisini kwakuwa hakuwa na fedha ya gesti wala chakula lakini ofisi ilikataa na ikamlazimu alale kwenye basi siku ya 03.10.2024.

04.10.2024 AONDOKA DODOMA KWA KUUZA SIMU.

Baada ya kukosa msaada ikabidi auze simu ili ajikimu na kusafiri kurudi Kilindi.Ikumbukwe cwt wilaya ya Kilindi haikuonesha ushirikiano wowote kwa mwalimu yule japo wao ndio wenye jukumu la kumsaidia mwanachama wao.Viongozi wenyewe kwa wenyewe pale Cwt kilindi husaidiana kutatuliana shida zao na zinakaa vizuri.Katibu alivyotoka likizo alikwenda kwa ded kilindi akafuatilia shida za mwenzie na akafanikiwa kulipwa stahiki nyingi huku za wanachama wachangiaji wapo kimya.Mungu atashusha adhabu juu Yao amen.

VIONGOZI CWT HQ WAPO BUSY MIKOANI.

Mpaka kufikia tarehe ya leo 13.11.2024 wahasibu na viongozi wa Cwt Hq wapo busy mikoani hivyo kushindwa kumhudumia mwalimu alipe madeni aliyoingia akiwa Dodoma.

CWT YAMPUUZA MWALIMU NA KUJALI VIKAO.

Inaonekana viongozi CWT Makao makuu Dodoma wanajali vikao zaidi kuliko huduma kwa wanachama.Siku ya 03.10.2024 walionekana wakiwa busy na kuandaa mabegi ya vikao huku wakimtelekeza mwalimu Dodoma ambae michango yake ndio inayowaweka hao viongozi mjini.

Hii ni laana wanajitengenezea na napata mashaka na utendaji wao kwa wanachama.

Nawasilisha
 
Mwalimu posho yake ni mpaka kusimamia mtihani Tena uchaguliwe sio lazima.... Ama vitokee visemina vya masomo ..mwalimu kukutana na posho ni kama kukutana na trafiki ziwani....
Aisee mbona kazi ina kazi sana mkuu
 
Aisee mbona kazi ina kazi sana mkuu
Sijui Kwa Nini waliwaondolea " teaching allowance" ambayo walikuwa wanalipwa kama tu wanavyolipwa majeshi na Sasa wanawalipa na watendaji wa vijiji na kata pamoja na Walimu wakuu na waratibu elimu wa kata yaani wanawalipa....yaani Walimu ,madaktari na manesi Hawa watu ndio wakulipwa Sasa allowance za mazingira magumu sio kuzipeleka polisi na majeshini Ili tu walinde utawala wao. Walimu Wana hali ngumu.
 
Walimu wengi kinacho waumiza ni tamaa mambo ya kufanya miezi 6 mtu ana taka ayafanye kwa wiki moja .mnaishia kwenye mikopo na ukianza kukopa utoki utakuwa hadi ustaafu
 
Hii ni laana wanajitengenezea na napata mashaka na utendaji wao kwa wanachama.
Hamna kitu inaitwa laana.

Ukiamini hicho, utateseka kwa kuamini fulani anakukosea kusudi hivyo atapata laana na utaishia kuona akidunda tu na wewe ukizidi kutaabika.

Na hata akianguka, anguko lake halitakunufaisha wewe utaishia kujifariji kua kapata laana.
 
Hamna kitu inaitwa laana.

Ukiamini hicho, utateseka kwa kuamini fulani anakukosea kusudi hivyo atapata laana na utaishia kuona akidunda tu na wewe ukizidi kutaabika.

Na hata akianguka, anguko lake halitakunufaisha wewe utaishia kujifariji kua kapata laana.
Mpaka pale litakapomfika mtu ndipo ataongea kimoyomoyo na kukiri yeye mwenyewe CWT wana dhambi kwakuwa hawawatendei haki kazi yao ni kufurahia michango ya walimu lkn nasema muda utaongea.
 
Hii story kama ni ya kweli basi kuna mahala hapo sawa upande wa mwalimu. Mwalimu utoke Tanga hadi Dodoma bila nauli wala hela ya kujikimu je ina maana hata jamaa(ndugu, marafiki, staff mate nk) wameshindwa kuguswa na tatizo lake mpaka wamwache ktk hali ya kudhalilika hivyo?
Pili mnaolaumu pia hivi vyama mtuambie ni chama gani cha wafanyakazi hapa nchini hutoa msaada wa kifedha kwa wanachama wao? Nachojua hivi vyama vipo kutoa msaada wa kisheria sijasikia popote kama vinatoa msaada wa kifedha. Vinginevyo watumishi wa umma tujifunze kuishi vizuri na wanaotuzunguka naamni baadhi ya mambo wanaweza kusaidia tusiingie fedheha
 
Nina mashaka na mwl .Yaani pesa za likizo ufunge safari toka Tanga vijijini hadi Tamisemi Dodoma!
Aeleze vema vinginevyo kuna tatio mahali
 
Back
Top Bottom