Nguva Jike
JF-Expert Member
- Jan 22, 2018
- 1,226
- 1,757
- Thread starter
-
- #21
Wewe hujui adha wanazokutana nazo walimu ndio maana unaongea vima hapa.Alissfiri ili akapewe hela Dodoma?! Kama hakuwa na fedha kwanini alilazimisha safari?! Mbona hujaelewa kama alifanikiwa kushughurikia suala lake?!
Mwalimu posho yake ni mpaka kusimamia mtihani Tena uchaguliwe sio lazima.... Ama vitokee visemina vya masomo ..mwalimu kukutana na posho ni kama kukutana na trafiki ziwani....Inafikirisha sana mkuu stahiki Zake una maanisha mshahara hajalipwa pia vip kuhusu kadi ya bima pia?? Na hana hata nauli wala hela ya kula?? au umeamua kunogesha story kidg.
Any way lkn mimi sio mwl hayanihusu pole ake Mungu amsaidie atimiziwe haja zake
Ndio maana watoto shule za gvt performance huwa ni avarage sana kwa kuwa hakuna motisha
Wakifanya hivyo kitakufa, walimu wote wata leftHiki chama kiwe na uhuru wa kujiunga na kujitoa.
Hujui eenh, hao ni km wazazi ukizaliwa tuu huwezi kuwabadili.Kwamba unachama ni lazima!?
Wewe ni makiKuna mahali mwandishi anasema mwalimu aliomba alale ofisini...
Huyu mwalimu anaibua maswali mengi.
Wewe na huyo mwalimu wako wote ni vilaza, hiyo ofisi ya CWT ni gesti hadi mtu aombe kulala?Wewe ni maki
Habari za muda huu.
Chama cha walimu makao makuu Dodoma chamtelekeza mwanachama wake bila huruma ndani ya jiji la Dodoma.
Hayo yalijiri siku ya tarehe 03.10.2024.Ambapo katika tarehe hiyo mwalimu kutoka Kilindi Tanga (jina na shule anayotoka inahifadhiwa)
Mwalimu huyo alifika Dodoma siku ya tarehe 02.10.2024 kwa usafiri wa Lori la mizigo kwani hakuwa na nauli ya basi.
Lengo la safari ya Dodoma ilikuwa ni kufika ofisi ya raisi-Tamisemi kupeleka malalamiko kadhaa dhidi ya mwajiri wake ikiwemo kutopatiwa stahiki za uhamisho na pesa za matibabu.
Kutokana na ukata aliokuwa nao ikambidi afike Dodoma cwt hq kuomba msaada.Ikumbukwe siku ya tarehe 02.10.2024 alilala booking office za Simba mtoto hakuwa na pesa ya gesti.
APOKELEWA NA MHUDUMU WA HUDUMA KWA WANACHAMA.
Siku ya tarehe 03.10.2024 akapokelewa na mhudumu tajwa na kuamrishwa aandike barua ya kuomba msaada.Alipoandika akapewa majibu kuwa hakuna cash kwa siku ile.
AOMBA HIDADHI YA KULALA AKATALIWA.
Siku ile ile akaomba msaada alale pale ofisini kwakuwa hakuwa na fedha ya gesti wala chakula lakini ofisi ilikataa na ikamlazimu alale kwenye basi siku ya 03.10.2024.
04.10.2024 AONDOKA DODOMA KWA KUUZA SIMU.
Baada ya kukosa msaada ikabidi auze simu ili ajikimu na kusafiri kurudi Kilindi.Ikumbukwe cwt wilaya ya Kilindi haikuonesha ushirikiano wowote kwa mwalimu yule japo wao ndio wenye jukumu la kumsaidia mwanachama wao.Viongozi wenyewe kwa wenyewe pale Cwt kilindi husaidiana kutatuliana shida zao na zinakaa vizuri.Katibu alivyotoka likizo alikwenda kwa ded kilindi akafuatilia shida za mwenzie na akafanikiwa kulipwa stahiki nyingi huku za wanachama wachangiaji wapo kimya.Mungu atashusha adhabu juu Yao amen.
VIONGOZI CWT HQ WAPO BUSY MIKOANI.
Mpaka kufikia tarehe ya leo 13.11.2024 wahasibu na viongozi wa Cwt Hq wapo busy mikoani hivyo kushindwa kumhudumia mwalimu alipe madeni aliyoingia akiwa Dodoma.
CWT YAMPUUZA MWALIMU NA KUJALI VIKAO.
Inaonekana viongozi CWT Makao makuu Dodoma wanajali vikao zaidi kuliko huduma kwa wanachama.Siku ya 03.10.2024 walionekana wakiwa busy na kuandaa mabegi ya vikao huku wakimtelekeza mwalimu Dodoma ambae michango yake ndio inayowaweka hao viongozi mjini.
Hii ni laana wanajitengenezea na napata mashaka na utendaji wao kwa wanachama.
Nawasilisha
Mbona Tughe,ipo tuu inasongesha mi ningekuwa ticha aiseee.Wakifanya hivyo kitakufa, walimu wote wata left
Aisee mbona kazi ina kazi sana mkuuMwalimu posho yake ni mpaka kusimamia mtihani Tena uchaguliwe sio lazima.... Ama vitokee visemina vya masomo ..mwalimu kukutana na posho ni kama kukutana na trafiki ziwani....
Uhuru upo njoo chakuhawataHiki chama kiwe na uhuru wa kujiunga na kujitoa.
Sijui Kwa Nini waliwaondolea " teaching allowance" ambayo walikuwa wanalipwa kama tu wanavyolipwa majeshi na Sasa wanawalipa na watendaji wa vijiji na kata pamoja na Walimu wakuu na waratibu elimu wa kata yaani wanawalipa....yaani Walimu ,madaktari na manesi Hawa watu ndio wakulipwa Sasa allowance za mazingira magumu sio kuzipeleka polisi na majeshini Ili tu walinde utawala wao. Walimu Wana hali ngumu.Aisee mbona kazi ina kazi sana mkuu
Wote wanaowatesa walimu kwa makusudi kiama Chao kimefikaPole sana mwalimu
Hamna kitu inaitwa laana.Hii ni laana wanajitengenezea na napata mashaka na utendaji wao kwa wanachama.
Mpaka pale litakapomfika mtu ndipo ataongea kimoyomoyo na kukiri yeye mwenyewe CWT wana dhambi kwakuwa hawawatendei haki kazi yao ni kufurahia michango ya walimu lkn nasema muda utaongea.Hamna kitu inaitwa laana.
Ukiamini hicho, utateseka kwa kuamini fulani anakukosea kusudi hivyo atapata laana na utaishia kuona akidunda tu na wewe ukizidi kutaabika.
Na hata akianguka, anguko lake halitakunufaisha wewe utaishia kujifariji kua kapata laana.