Cyprian Musiba aikacha ACT Wazalendo, aomba ridhaa ya kurudi CCM

Cyprian Musiba aikacha ACT Wazalendo, aomba ridhaa ya kurudi CCM

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Mwanaharakati na Mwanasiasa Cyprian Majura Musiba, ametangaza rasmi kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia Januari Mosi, 2026, akisema amefanya uamuzi huo kwa hiari yake bila kushawishiwa na mtu yeyote.

Katika barua ambayo imenaswa na Royal TV ikionesha uamuzi huo tangu mapema Januari mwaka huu akiwa amemwandikia Katibu wa CCM Tawi la Nyarugoma, Kata ya Iramba Musiba ameomba kupokelewa tena kama mwanachama wa kawaida wa chama hicho, akisisitiza kuwa yuko tayari kufuata taratibu, kanuni na katiba ya CCM.

Soma Pia: Baada ya kutemwa ubunge CCM, Cyprian Musiba akimbilia ACT Wazalendo

“Nimeamua kwa ridhaa yangu kurejea katika chama cha mapinduzi kuanzia leo tarehe 01/01/2026 kama mwanachama wa kawaida tu,”

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Septemba 2025, Musiba alihamia Chama cha Act Wazalendo na kugombea Ubunge Jimbo la Mwibara Mkoani Mara ambako alishindwa na Kangi Lugola katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

musi.png
 
Back
Top Bottom