PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mwanaharakati huru Cyprian Musiba ameshindwa kupenya katika mchujo wa wagombea walioteuliwa kupigiwa kura za maoni kuwania Ubunge wa Jimbo la Mwibara, mkoani Mara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imeteua jumla ya wagombea saba watakaoshiriki katika hatua inayofuata ya mchakato wa kura za maoni.
Walioteuliwa ni Charles Kajege (Mbunge anayemaliza muda wake) Kangi Lugola, Wilson Maregesi Mukama, Mbuke Makanyaga Majula, Idd Mabala Yazid, Emmanuel Makalle Busanya
Hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa Mwaka 2020, Musiba alikuwa ni miongoni mwa vinara wa tatu wa juu waliopata kura nyingi za wajumbe kwenye kura za maoni