Tanzania ikiwa inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Mwanaharakati huru Cyprian Musiba amesema kuwa tafiti zinaonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), anaungwa mkono kwa asilimia 91 katika kaya mbalimbali za Tanzania Bara. Wakati huo huo, vyama vya upinzani vinaungwa mkono kwa asilimia 9 pekee.
Akizungumza Machi 3, 2025, kuhusu utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Global Watch African Limited kutoka Malawi, kwa kushirikiana na CZI Tanzania Limited, ya Jijini Dar es salaa. Musiba ameeleza kuwa taasisi hizo zilipeleka watafiti wao katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Kulingana na matokeo yao, watu 10 walihojiwa katika kila mtaa
Watu 7 kati ya 10 walionyesha kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Watu 2 walionyesha kumuunga mkono Tundu Lissu, Mmoja alikiri kutokuwa na msimamo kuhusu uchaguzi
Aidha, Musiba amebainisha kuwa, ingawa tafiti zinaonesha Rais Samia ana uungwaji mkono mkubwa, vyama vya upinzani vinaonekana kuongeza ushindani, hasa katika nafasi za Ubunge na Udiwani.