POTOSHI Cyril Ramaphosa: Trump usitupangie cha kufanya, hauimiliki Afrika Kusini. Jishughulishe na Marekani, tuache na matatizo yetu

POTOSHI Cyril Ramaphosa: Trump usitupangie cha kufanya, hauimiliki Afrika Kusini. Jishughulishe na Marekani, tuache na matatizo yetu

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Baada ya Trump kutangaza kusitisha misaada nchini humo kisa madai ya ukiukwaji wa haki za Binadamu na Wazungu kunyanyaswa na kupokonywa ardhi wanazomiliki ambapo Ramaphosa amemtaka Trump aache kuingilia mambo ya Afrika Kusini kwakuwa hayamuhusu na kusema ardhi ya Afrika Kusini sio ya Trump.

1738590887296.png


“Hii ishu ambayo Donald Trump anaiogopa sana, hii ardhi ni ya kwetu, sijui Donald Trump anahusika vipi na atafanya nini kuhusu ardhi ya Afrika Kusini kwasababu hajawahi kuwa hapa, aitunze America yake na tutaitunza Afrika Kusini yetu, Afrika Kusini ni ardhi yetu na inamilikiwa na Watu wote wanaoishi Afrika Kusini, Afrika Kusini haimilikiwi na Donald Trump”

“Nikikutana na Trump nitamwambia, nitamwambia wewe Trump ni Mtu mbaya kwasababu unapendelea upande mmoja, Marekani kulikuwa na Watu wenye asili ya Marekani waliwaondoa na kuwaua karibu wote, sisi tunaishi kama Taifa la wote Watu weusi na weupe na tunatafuta suluhisho sisi wenyewe kuhusu ardhi, Trump atuache, atuache”

“Wakati tukiwa tunakandamizwa na kunyanyaswa (na Makaburu ) hakuwepo hapa, hakupigana bega kwa bega na sisi na sisi wenyewe tulitatua tatizo kwa msaada wa Watu wengine Duniani Trump hakuwepo, kwahiyo aendelee na mambo yake White House na tutaendelea na mambo yetu, pambana na mambo yako na sisi hatutoingilia mambo ya Marekani”


 
Tunachokijua
Cyril Ramaphosa ni Rais wa tano wa Afrika Kusini ambaye ameingia madarakani mwaka 2018. Donald Trump ni Rais wa 47 wa Marekani ambaye ameingia ofisini January, 2025. Tangu Donald Trump aingie madarakani amekuwa akifanya mabadiliko mbalimbali hususani kwa bara la Afrika ikiwemo kusitisha misaada kwa nchi hizo na kuwarudisha wahamiaji haramu kwenye nchi zao ambapo watu kutoka Afrika pia ni wahanga.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Truth 3 Februari, 2025, Trump aliandika ujumbe kuhusu kusitisha misaada Afrika Kusini ameandika;

“Afrika Kusini inachukua ardhi, na inawafanya baadhi ya makundi ya watu vibaya sana. Ni hali mbaya ambayo Vyombo vya Habari vya Kushoto vya Kikali havitaki hata kugusia. Ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu, angalau, unafanyika mbele ya macho ya kila mtu. Marekani haitakubaliana na hili, tutachukua hatua. Pia, nitakata msaada wote wa kifedha kwa Afrika Kusini hadi uchunguzi kamili wa hali hii ukamilike!”

Baada ya ujumbe huo kumekuwapo na kinachodaiwa kuwa Ramaphosa amemjibu Trump kuhusu kusitisha misaada Arika. kipande hiko video kinachomunesha Ramaphosa akieleza kuwa Trump asiwapangie cha kufanya kwani haimiliki Afrika kusini. Baadhi ya maneno yanayosikika kwenye video hiyo ni;

“Wakati tukiwa tunakandamizwa na kunyanyaswa (na Makaburu) hakuwepo hapa, hakupigana bega kwa bega na sisi na sisi wenyewe tulitatua tatizo kwa msaada wa Watu wengine Duniani Trump hakuwepo, kwahiyo aendelee na mambo yake White House na tutaendelea na mambo yetu, pambana na mambo yako na sisi hatutoingilia mambo ya Marekani”. Tazama baadhi ya watu waliochapisha video hizo hapa na hapa.


Ukweli upoje?

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa video hiyo ni halisi lakini si ya hivi karibuni hivyo kuhusianishwa na tukio la mwaka huu (2025) ni upotoshaji.

JamiiCheck imefanya ufuatiliaji kupitia Google reverse image search na kubaini kuwa video hiyo ni ya Agosti, 2018 ambapo Ramaphosa alimjibu Rais wa Marekani Donald Trump, akisema ni makosa kwake kuingilia masuala ya ndani ya Afrika Kusini baada ya Trump kumuagiza aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kuchunguza suala la unyakuzi wa ardhi na mashamba nchini Afrika Kusini pamoja na mauaji ya wakulima.

Aidha Ramaphosa ametumia mtandao wa X kujibu madai ya Trump aliyoyatoa 03 Februari, 2025 na siyo kipande cha video kinachosambaa, ambapo ameandika;

“Afrika Kusini ni demokrasia ya kikatiba ambayo imesimikwa katika utawala wa sheria, haki na usawa. Serikali ya Afrika Kusini haijachukua ardhi yoyote.

Sheria ya Uhamasishaji ya hivi karibuni sio kifaa cha kuchukua ardhi, bali ni mchakato wa kisheria unaotambulika kikatiba ambao unahakikisha upatikanaji wa ardhi kwa umma kwa njia ya haki na usawa kama inavyoelekezwa na katiba.
” Tazama hapa
Wao USA wameungana sisi Waafrika tunasubiri nini na UNITED STATES OF AFRICA?
Kwa Afrika ni mara 1000 mipaka ikabaki kama ilivyo, UNITED STATES OF AFRICA haiwezi dumu hata siku moja kabla mtu hajapinduliwa. Pia kuna watu hatawatopata huduma za kijamii hata moja milele.
 
Siku hizi Rama mwamposa kawa mswahili sana kama hajimanara au kapata kimada tz.
 
Trump ni kibabu kijinga ambacho kinataka kuharibu mustakabali wa Dunia.

Hana busara wala diplomasia anaongozwa na mihemuko mwisho wake utakua wa aibu.
 
Pamoja na kuwaua wamarekani asili pia blacks walikuwa wanamiliki ardhi Ila ilitungwa Sheria ambayo walitolewa ama kunyang'anywa ardhi yao
 
  • Thanks
Reactions: X2Z
Kwa Afrika ni mara 1000 mipaka ikabaki kama ilivyo, UNITED STATES OF AFRICA haiwezi dumu hata siku moja kabla mtu hajapinduliwa. Pia kuna watu hatawatopata huduma za kijamii hata moja milele.
Mimi bado nina imani kuwa tutaweza tuonyeshe mfano sisi East Africans, halafu tuungane na Southern Africans, halafu kwa pamoja twende kwa West Africans.

Tutengeneze katiba ambayo itakuwa ni vigumu kupindua Serekali ya umoja wa Afrika vipi hapo 👆
 
Mimi bado nina imani kuwa tutaweza tuonyeshe mfano sisi East Africans, halafu tuungane na Southern Africans, halafu kwa pamoja twende kwa West Africans.

Tutengeneze katiba ambayo itakuwa ni vigumu kupindua Serekali ya umoja wa Afrika vipi hapo 👆
Rate ya ubinafsi ni kubwa Sana sijui kama Tunaweza
 
Uyo Ramaphosa apuuzwe,ni lifisadi sanaa ilii jamaaa,alafu unawezaje kusema U.S.A ijitenge na wewe wakati misaada yao kila kukicha unawaomba?/
 
Wao USA wameungana sisi Waafrika tunasubiri nini na UNITED STATES OF AFRICA?
Bado mtoto wewe, ulishasikia UNITED STATES OF EUROPE?
Waambie wazungu waungane kama unafikiri USA zilikuwa nchi kama UK, France, German nk.
 
European Union ni malengo yao kuelekea kwenye muungano kamili sisi Waafrika tunashindiwa nini?
Mtaungana vipi na kupata uongozi wakati hata uchaguzi tu hamuwezi kufanya bila kufanya hujuma kwenye huo uchaguzi. Afrika bure kabisa.
 
Mtaungana vipi na kupata uongozi wakati hata uchaguzi tu hamuwezi kufanya bila kufanya hujuma kwenye huo uchaguzi. Afrika bure kabisa.
Sasa mbona tena kuna Waafrika wanasifia Mapinduzi ya Kijeshi huko Burkina Faso Mali na Niger ambako hata huo uchaguzi wa kiraia umepigwa marufuku?!
 
Sasa mbona tena kuna Waafrika wanasifia Mapinduzi ya Kijeshi huko Burkina Faso Mali na Niger ambako hata huo uchaguzi wa kiraia umepigwa marufuku?!
Hayo mapinduzi yanakuja kufuatia kufeli kwa raia ikiwa ni pamoja na hayo mambo ya kuhujumu chaguzi.
 
Back
Top Bottom