Watanzania / Waafrika tuna safari ndefu sana.
Freedom of speech hatuna na freedom of thought hatuna. Uzi wa majambazi wa Marekani huko mtu bado unaogopa ku think aloud eti wamekuonya sababu za kijamii...
Kamanda Siro atakufuatilia kwa uchochezi wa kutoa siri za kijambazi? This is a new one.
Anyhow, Cooper to me, was far from a genius. Aliruka nje kwenye milima na misitu usiku, 200mph wind blizzard, minus 69 degrees cold, drenching rain storm, kavaa suti na dress shoes na parachute moja zima.
Cardinal rule of sky diving, lazima uwe na parachute mbili. Reserve chute ya Cooper ilikuwa imeandikwa haifanyi kazi, kwa mafunzo tu...
Tell me where the genius in that is.
Nakubaliana kabisa na wewe kabisa mkuu.. Wazo hili kuwa Cooper hakutua salama ardhini pia FBI walilipata siku ya kwanza tu walipoanza upelelezi wa tukio, lakini kwanini upelelezi udumu kwa miaka 45 kama FBI wenyewe wanaamini Cooper alikufa?? Ni kwamba hiyo nadharia ina ukakasi mwingi mno na inaleta maswali mengi kuliko majibu.
Kama Cooper hakutua salama kwanini washindwe kubata mabaki ya mwili wake??? Kama waliukosa mwili kwanini washindwe kupata walau hata mabaki ya vitu vyenyewe alivyoruka navyo?? Parashuti? Nguo? Fedha? Mabegi??
Jambo lingine; Sidhani kama Cooper uchaguzi wa parashuti ulikuwa ni wa bahati mbaya. Mtu aliyejiamini kuruka kwenye ndege umbali wa futi 10,000 kutoka ardhini huyu kwangu nahisi ni mtu mzoefu kabisa katika Skydiving.. Kumbuka yeye ndiye aliyetoa maelekezo ndege iinuliwe umbali huo ambao ndio umbali wa juu kabisa (maximum) ndege ya Boeing 727 inaweza kufika. Kwahiyo alikuwa na sababu yake kwanini alitaka ndege iruke juu hivyo.
Kuhusu hili suala la labda hakutua salama; nimewahi kusikiliza intavyuu ya Bw. Carr ambaye ndiye aliongoza upelelezi wa tukio la Cooper mtangazaji alimuuliza kuwa kama wanahisi labda Cooper hakutua salama kwanini wanaendelea na uchunguzi?? Carr akamjibu kuwa inawezekana labda Cooper alidhamiria kuwafanya FBI wafikiri hivyo kuwa hakutua salama! Unapokabiliana na muhalifu wa daraja la kwanza (master criminal) ni lazima ufahamu kuwa ni mabingwa wa kupandikiza mawazo na kukushawishi uwaze vile wao wanataka (manipulation) Cooper aliwafanyia hivi toka siku ya kwanza alipoamuru apewe parashuti nne (rejea kipengele kwenye stori kuu).
Hivyo basi Bw. Carr akamueleza mtangazaji kuwa kwa kiwango fulani wanadhani labda Cooper hakutua salama lakini pia hawaamini nadharia hiyo kwa asilimia mia kwasababu inawezekana labda Cooper alifanya hivyo kusudi ili FBI waamini hakutua salama.
Jambo lingine; ipo nadharia nyingine FBI wanadhani labda Cooper alikuwa ni Veterani wa askari wa anga (Air force).
Kwasababu wakiwa wanamuhoji muhudumu baada ya tukio, katika maelezo yake muhudumu (Bi. Schaffner) aliwaeleza kuwa wakiwa wanakaribia kutua uwanja wa ndege Cooper alikuwa anawapigisha stori na katika muda fulani wakiwa wamekaribia ardhini nyumba zikionekana Cooper aliwaonyesha eneo Fulani na kuwaambia "pale kuna kituo cha jeshi la anga cha McChord (McChord Air Force Base) na ni mwendo wa kama dakika 20 na gari kutoka uwanjani". Wahudumu hawakutilia maanani sana kitu hiki lakini walipowasimulia FBI, maofisa wa FBI walishangaa kwasababu haikuwa rahisi kwa raia wa kawaida kulijua hilo na hata kama angefahamu jambo hilo raia wa kawaida isingekuwa rahisi kwake kuongelea suala kama hilo kwenye maongezi ya kawaida.
Kwahiyo ipo nadharia kuwa Cooper alikuwa ni vetereni wa jeshi la Anga. Na kama ni kweli alikuwa vetereni wa jeshi la Anga maana yake ana uzoefu wa kutosha kwenye kuruka angani na uchaguzi wake wa parashuti labda (nasisitiza 'labda') ilikuwa ni sehemu ya mkakati wake wa kucheza na akili za FBI (manipulation).
Kuhusu kuruka usiku; hii nisema kwa ujumla tu kuwa hata FBI wenyewe wanaamini kuwa kila kitu cooper alichokifanya kilikuwa amekipanga kabla na ilikuwa sehemu yake ya mkakati. Kuanzia siku ya kufanya tukio Novemba 24 (rejea kipengele kwenye stori), muda wa kufanya tukio, ndege gani aiteke n.k. vyote hivi vilikuwa sehemu ya mkakati.
Kwahiyo kuruka jioni haikuwa Bahati mbaya, kama angetaka kuruka mchana kweupe angeenda kuiteka ndege ya asubuhi! Aliteka ndege ya jioni kwasababu alikuwa anakita kiza, ilikuwa ni sehemu ya mkakati.
Kama hiyo haitoshi hata uchaguzi wake wa eneo la kurukia pia kwangu unanambia kuna kitu nyuma ya pazia! Walipotoka uwanja wa ndege Seattle akawaamuru marubani wapite njia ya Vector 23 kuelekea Reno. Njia hii ardhini ina mito mikubwa mitatu (mto lewis, mto Columbia na mwingine siukumbuki jina) na pia sehemu ambapo aliruka chini kuna maziwa makubwa mawili (ziwa Merwin, na lingine kama sijakosea linaitwa St. Louis ) na pia kuna bwawa kubwa la kuchimbwa. Kwangu mimi hii sioni kama ilikuwa ni coincidence, naamini hii ilikuwa ni sehemu ya mkakati.
Kwahiyo mkuu; nachelea kufanya hitimisho haraka haraka kuwa hakutua salama, pengine ni kama alivyosema Bw. Carr labda alichagua parashuti lile makusudi ili apandikize wazo kwa maofisa wa FBI kuwa hakutua salama. Sijui lakini ila kwa muhalifu daraja la kwanza kama Cooper, hakuna kilichopo kama kinavyoonekana. Kila jambo na kila hatua ni fumbo na mkakati.