Nilisha consider adjustment for inflation kwenye bandiko hilo hilo, hukuona? Bado sio pesa nyingi kihivyo.
Well, sijui uchumi lakini hata economic historians hawakubaliani jinsi rahisi au uhakika ya kuthaminisha hela za miaka tofauti. Lakini ugumu hauzuii kujaribu.
Kuna vikokotozi mbali mbali vya mfumuko wa bei (infation calculators) kutoa walau picha ya wastani, mojawapo maarufu ni kutumia Consumer Price Index. Kwamba je, ungehitaji shilingi ngapi leo kununua sahani ya Mama Ntilie ambayo mwaka 1971 tulikula kwa shilingi 1? Jibu lake kwa leo buku jelo, buku mbili.
Kwa Marekani nimetumia Inflation Calculator inayotumia Consumer Prive Index ya Idara ya Kazi na Takwimu, US Bureau of Labor and Statistics. Nikapata hela ya Cooper $200,000 ni sawa na kama $1.2M kwa leo.
Ndo nikasema mshahara wa pilot wa Marekani haupishani sana na hela ambayo wa kina Cooper, ma pilot na flight attendants wangegawana. Bado hatujaongelea FBI waliokula njama kama wapo. I mean, sidhani kama wange risk career zao, maisha yao, kukamatwa (criminals wanajua mkiwa wengi mnaongeza risks za kuisha). Hailipi, sidhani kama ni njama.