D.R.C Taifa lililolaniwa tangu wapate Uhuru

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kongo imelaaniwa, tangu wapate Uhuru hawajawahi kupata utulivu. Dalili kuu ya mtu au Taifa lililolaniwa ni kukosa utulivu.
Your browser is not able to display this video.


DRC nchi iliyojaa madini. Kuna sehemu ukiingia msituni kabisa huko ukichota mchanga gunia 1 unaweza kupata pure gold debe moja lakini kwasababu ya laana iliyotokana na ardhi kushiba damu za watu hayo madini hayajawahi kuwa na mchango wa maana kwa wananchi.

DR Congo kuna ufukara uliokithiri. Kongo kuna nuka damu.

Viongozi nao shetani kawaziba macho wanadhani kutumia upanga kutalituliza Taifa. Juzi wameuwawa kikatili vijana wadogo (panya road) 102 na wengine wanatarajiwa kunyongwa kikatili pia soon.

Ni unyama, unyama na ushetani.

Wanadhani wanaliponya Taifa kumbe wanalinywesha damu zaidi lizidi kulaaniwa.
 
Unamaanisha Chaga zone wakichukua Nchi watafanya mapinduzi within 15 yrs?
 
Tanzania tunatakiwa tumfukuze barozi wa DRC ili kuonesha hatujapendezwa na kunyongwa Kwa vijana.kuua siyo njia sahihi ya kumaliza tatizo,Tatizo la kuwepo Kwa hayo magenge yalitokana na serikali yenyewe kutokutengeneza mazingira mazuri Kwa watu.
Sasa mbona milio mingi inatokea Rwanda badala ya Congo baada ya hao vijana kunyongwa?

Tena siyo kunyongwa! Nasikia wamemiminiwa njugu!
 
Nchi ya wajinga hiyo imekuwa shamba la MABEBERU

Kila beberu lenye madevu linatia kambi congo kuleta fujo.

Naagiza hiyo nchi ilipuliwe yote tuanze upya.
 
Tanzania tunatakiwa tumfukuze barozi wa DRC ili kuonesha hatujapendezwa na kunyongwa Kwa vijana.kuua siyo njia sahihi ya kumaliza tatizo,Tatizo la kuwepo Kwa hayo magenge yalitokana na serikali yenyewe kutokutengeneza mazingira mazuri Kwa watu.
Tokeni zenu, yaan muwatetee majambazi? Mbona hata Tz ukileta upuuzi wanakupoteza chap tu stories zitabaki mitaan kuwa hujulikani ulipo.

Kila nchi ina namna yake ya kupambana na hawa vibaka wanaoharibu uhai na mali za wengine, hizo haki za kipuuzi mnazotetea ndio chanzo cha kulea ushenzi wa kila aina.

Huwa nashangaa wajinga mnaotetea wauaji kupewa malipo yao ya kifo, sidhani mtu mwenye akili timamu ambaye anaujua uchungu wa kupotezewa ndugu, rafiki, mzazi na hao vibaka, ataweza kuwatetea eti wasiuliwe, malipo ya kifo ni kifo hakuna njia mbadala wala mkato, anayeua kwa makusudi lazima afe hiyo ndio haki.

Acheni kutetea upuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…