joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 17,420
- 35,765
Mnapenda kulalamika ndio maana unaambiwa hujui mpira?Timu haina wachezaji wake watatu Key Player ulitaka wachezaje?Mamelodi walikuja kwalengo la kupata sare na wamefanikiwa je sisi kule kwao tutaweza??? Isije kua yaleyale ya kubanabana ila mwisho wa siku tukatolewa, ikawa tulichelewesha muda tu
Halafu timu zinazo miliki mpira formula ya kuwafunga ni kuwaacha wao wamiliki mpira then ww ukiwa accurate kwenye nafasi upatazo. Hivi ushaiona Barca ya Messi,Inesta,Busquet,Xavi nk Mourihno alikuwa na vikosi bora Inter na Chelsea, aliwafunga japo possession walidominate Barca. Njoo Arsenal, ya Wenger na Man ya Ferguson,Arsenal anapigwa na Man huku akiwa na possession kubwa.
Mamelod wawe ugenini, wawe nyumbani haijalishi wanacheza na timu upande wa possession watadominate wao na timu zote wanazo cheza nazo huwaacha wachezee mpira,huku wakiwa Vizia kwenye mashambulizi ya kushtukiza. Wewe unazani mwaka jana Wydad alimpiga Mamelod kwake, unazani walicheza mpira mzuri au Mazembe wamempiga kwenye makundi, unazani walitawa mpira Mazembe au ww hutizamagi mechi za Mamelod unasimuliwa na kucoclude.
Team haina key player watatu, wanacheza na timu bora Africa, wamepata droo unalalamika. Hivi unaujua mpira? Haipo timu Africa inayo ifikia Mamelod kwa kuweka mpira chini, ndio maana wanamwacha achezee mpira, ila wao wanadeal na nafasi zao, sema tu Yanga hakuwa striker mzuri kwani ile mechi zile chance alizo zipata Mzize na Musonda yote magoli na mpango wa Yanga ulikuwa sahihi kwa asilimia mia.