Daah jamani wadaiwa

Kuna Jamaa namdai lakini kila siku anapost picha akiwa anacheka hizi si dharau za wazi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mm Kuna jamaaa namdai laki 5 alafu kila leo anakunywa bia tu ukimfuata anakwambia bia za wadau hz kuwa mpole ila nimepanga niende kwa boss wake daaadek jumatatu

kilicho akilini kitumie
 
Kuna jamaa alikopa, kabla hajalipa akakopa tena.

Tarehe za kulipa zimefika haonekani, hata udhuru wa kusema ana tatizo gani hajatoa!
 
Kuna jamaa nimemkopesha kama laki 8 hivi, kinachonikera amekuwa akihudhuria kwenye mikusanyiko ya watu, halafu ushauri wa kunawa mikono huwa hata hauzingatii halafu ndio jijini Dar

Huyu mtu nimfanyeje wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kuna mtu namdai , kila saa yuko Facebook.
Na kuna mwingine kila kitu kinachouzwa kwa mkopo, anachukua kwa mkopo, nadhani tunamdai wengi sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…