Dabi ya Kariakoo Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027 kupigwa Oktoba 10, 2026

Dabi ya Kariakoo Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027 kupigwa Oktoba 10, 2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 12, 2026 wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC, timu hizo mbili zitaendelea na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2026/2027. Yanga SC itasafiri kuelekea Ruangwa, Lindi, ambapo Agosti 15, 2026 itacheza dhidi ya Namungo FC katika mchezo wake wa mwanzo wa ligi.

Kwa upande wa Simba SC, baada ya mchezo huo wa Ngao ya Jamii, kikosi hicho kitaelekea Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Agosti 16, 2026 katika Uwanja wa Kaitaba. Wakati huo huo, mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu NBC msimu wa 2026/2027 utakuwa kati ya Pamba Jiji FC na Dodoma Jiji FC, utakaochezwa Agosti 14, 2026 katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Katika msimu huo mpya, mashabiki wa soka Tanzania wanatarajia kushuhudia tena Dabi ya Kariakoo katika Ligi Kuu NBC. Mchezo wa kwanza wa ligi kati ya Simba SC na Yanga SC umepangwa kuchezwa Oktoba 10, 2026, huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kufanyika Februari 6, 2027 ambapo Yanga SC itakuwa mwenyeji wa Simba SC.

Dabi ya Kariakoo Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027.

10 Oktoba 2026
Simba SC vs Yanga SC

6 Februari 2027
Yanga SC vs Simba SC

Hizi hapa mechi tano za kwanza za Yanga SC, Simba SC na Azam FC:

Yanga SC


Namungo (Away)
Coastal Union (Home)
JKT Tanzania (Home)
Pamba Jiji (Home)
Fountain Gate (Away)

Simba SC

Kagera Sugar (Away)
Pamba Jiji (Away)
Singida Black Stars (Away)
Coastal Union (Home)
Geita Gold (Home)

Azam FC

Polisi Tanzania (Away)
TRA United (Home)
Pamba Jiji (Home)
Geita Gold (Away)
Kagera Sugar (Away)
Ratiba ya @ligikuu ya @nbc_tanzania msimu 2026-2027.@tanfootball @ligikuu @nbc_tanzania @azamtvs.jpg

Ratiba ya @ligikuu ya @nbc_tanzania msimu 2026-2027.@tanfootball @ligikuu @nbc_tanzania @azamt...jpg

Ratiba ya @ligikuu ya @nbc_tanzania msimu 2026-2027.@tanfootball @ligikuu @nbc_tanzania @azamt...jpg

Ratiba ya @ligikuu ya @nbc_tanzania msimu 2026-2027.@tanfootball @ligikuu @nbc_tanzania @azamt...jpg

Ratiba ya @ligikuu ya @nbc_tanzania msimu 2026-2027.@tanfootball @ligikuu @nbc_tanzania @azamt...jpg
 
Jambo moja naloweza kuwa na hakika nalo ni kuwa hii ratiba inaweza kuharibika muda wowote kuanzia mwezi wa 10..
Pia inaeza kubadilika hata kabla ligi kuanza.. naona Kuna timu ina Mechi tatu mfululizo home ,na nyingine tatu mfululizo away
 
Kwa hizi game 5 za mwanzo za Yanga Simba atakua anaongoza Ligi.

Simba Asipoongoza hapa mwanzon asitarajie kuongoza au kubeba ubingwa
 
Back
Top Bottom