Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukilijua hili....hutakereka ng'o nakumbia; you'll find wayz za kuadapt........:clap2:
Wana JF
Huyu ni mama wa 2 kids
Mtoto wa kwanza alimzaa na mwanaume mwingine miaka 6 iliyopita ,yalitokea matatizo hawakuweza kuwa an uhusiano na huyu baba wa mtoto na akawa ameoa,Ila katika kipindi chote hicho Baba wa mtoto hakuwahi kuwasiliana na huyu dada wala kutoa matumizi ya mtoto wala kukumbuka kama aliwahi kuzaa dada alisononeka mpaka akazoea
Mungu si Athuman huyu dada nae akapata mwenza na akafunga ndoa mwaka jana.wanaishi na mmewe kwa amani na upendo na mungu kamjalia mtoto mwingine ana 6 month sasa.
Tatizo limeanza baada ya huyu mzazi mwenzie kufukuzwa kazi ,pia biashara zake zimefirisika sasa hana kitu kabisa amerudi kwa mama mtoto wake huyu na anabembeleza asaidiwe angalau aanze tena maisha na ameanza kumlaumu eti ajaribu kukumbuka fadhira alizomfanyia kipindi walipokuwa B/F na G/F na anaomba asahau tofauti zao
Mbaya zaidi huyu Baba mtoto wake kaanza kupiga simu na kutuma msg za malalamiko mpaka usiku wa Manane
Huyu dada ana hofu kama mmewe akijua kinachoendelea ndoa yake iko matatani ,kamuelewesha huyo baba wa mtoto wake lakini inaelekea haelewi na amekuwa kinganganizi
Anajiuliza amwambie mmewe au afanyeje maana jamaa haachi usumbufu
Kila anapojisikia anapiga simu na kutuma msg .
Pls msaada wenu kimawazo kwa dada huyu
alimpa namba yake ya simu ya nini naye???...kama alimuacha siku nyingi na hakutaka kujua lolote kuhusu yeye means hakuwa hata na contact naye...au ametafuta mawasiliano kutoka kwa rafiki zake? kama ni hivyo hawakumueleza sasa kama ameolewa?...mnh
Ni vizuri amuambie mumewe,hivi maana ya mume ni nini kama hamshirikishani magumu kama haya?!!
Ataanzaje kumwambia mumewe?
Kwamba amekutana na X wake, akampa namba yake ya simu na sasa kaanza kumtongoza tena?
Mi naona huyu dada hana msimamo. Mtu alikuacha zamani, ukahangaika na hatimaye Mungu akakushushia mana... unataka kuila jangwani? Wala usibadili namba yako ya simu.. mwambie mumeo yanayokusibu. Huyo X-wako kama angekuwa na busara na anajuta kweli wala asingekughasi namna hiyo. Huyu ni mchfuzi wa ndoa za watu. Alishakuona nyani.. je sasa umekuwa tumbili? Huyo ni shetani katika sura ya binadamu, mkatae kwa nguvu zako zote.
alimpa namba yake ya simu ya nini naye???...kama alimuacha siku nyingi na hakutaka kujua lolote kuhusu yeye means hakuwa hata na contact naye...au ametafuta mawasiliano kutoka kwa rafiki zake? kama ni hivyo hawakumueleza sasa kama ameolewa?...mnh
Ndio maana alikuja kuomba msaada kimawazoHili nalo ni la kuomba msaada? How far can she handle the disturbances?
Thanx kwa ushauri mzuri ST RRIf a crap is crapping.....kindly amshauri aje kumwomba 'mzee' mwenyewe...then amtaarifu 'mzee'!
Hicho ndio kinaniacha hoi na mie hapa ,kwa nn aanze kumlaumu mwenzie eti kashindwa kumsaidia ?Kwakuwa tayari yupo kwenye ndoa, so mumewe anajua kuwa alizaaa na mtu mwingine. ni suala la kusema kwa mumewe juu ya mawasiliano yaliyopo na huyo Baba wa mtoto. na ikiwezekana awakutanishe ( kwa simu au ana kwa ana), ni jambo la kawaida kama umeamua kufunga ndoa na mtu aliezaa. Hilo litamtia adabu huyo mwanaume, na hapo huyu dada atajua kama shidaza huyo mwanaume zina zinaukweli au la . kwa maoni yangu huyu dada amesha msaidia sana huyo bwana kwa kumlelea mtoto, sasa anaporudi tena kuomba msaada ilihali bado anasaidiwa kulelewa mwanae , ni kukosa shukurani.
Amwambie huyo mume wake mapema na asimfiche chochote.
Mambo yakiharibika zaidi patakuwa hapatoshi.
Wanaume wengine bwana...aaaahgggrr.
alimpa namba yake ya simu ya nini naye???...kama alimuacha siku nyingi na hakutaka kujua lolote kuhusu yeye means hakuwa hata na contact naye...au ametafuta mawasiliano kutoka kwa rafiki zake? kama ni hivyo hawakumueleza sasa kama ameolewa?...mnh
Hili nalo ni la kuomba msaada? How far can she handle the disturbances?
If a crap is crapping.....kindly amshauri aje kumwomba 'mzee' mwenyewe...then amtaarifu 'mzee'!
Kwakuwa tayari yupo kwenye ndoa, so mumewe anajua kuwa alizaaa na mtu mwingine. ni suala la kusema kwa mumewe juu ya mawasiliano yaliyopo na huyo Baba wa mtoto. na ikiwezekana awakutanishe ( kwa simu au ana kwa ana), ni jambo la kawaida kama umeamua kufunga ndoa na mtu aliezaa. Hilo litamtia adabu huyo mwanaume, na hapo huyu dada atajua kama shidaza huyo mwanaume zina zinaukweli au la . kwa maoni yangu huyu dada amesha msaidia sana huyo bwana kwa kumlelea mtoto, sasa anaporudi tena kuomba msaada ilihali bado anasaidiwa kulelewa mwanae , ni kukosa shukurani.
Ni vizuri amuambie mumewe,hivi maana ya mume ni nini kama hamshirikishani magumu kama haya?mumewe aweza kuwa wa msaada sana kwa mkewe kwenye hili.....nafikiri huyu dada awe na boundaries,she is married for God's sake,yanini kuwasiliana na X kiasi cha kujadili hadi fadhila za zamani na kuwa sasa kafilisika anahitaji msaada......kajiachia sana na hili litamgharimu akicheza........
Mumewe atagundua tu siku si nyingi,kwa kuwa huyu dada pia anajua analofanya si sahihi na hilo litajionyesha tu....amshirikishe mumewe na akate mawasiliano na huyo mwanaume wa zamani.....let the past remain the past!!!!
Ndo najiuliza kwa mtaji huu, nikisema siwapendi wanaume wa jinsi hii nitakuwa nimekosea??
Hivi kweli huyu dada anahangaisha kichwa chake na crap kama huyu!!
Mungu amekupa mume, unataka ubomoe ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe?
Dada simama kwa miguu yako kumkataa huyo X-something wako, uilinde ndoa yako.
Yani unataka uwe na waume wawili au?? Manake mwanaume huyo unamwamini je kama nia yake ni nzuri,
kwenye hiyo ndoa yako. Mijitu mingine wakati mwingine inadhamiria kukuharibia maisha milele wewe dada!!
Acha huruma ya kijinga wewe. Usije mlaumu Mungu bure. Amekupigania kote huko unataka uharibu tena.
Think!!!!! Mwambie ukukome, wakati utaamua mambo, kwanza akafight huko alete matunzo ya mtoto kama anataka mtoto!!
Yaani hata kama huyo mwanaume ni baba yangu, nita mdefine hivi hivi!!
Nafikiri alichokosea huyu dada ni kuacha hii ishu ku-prolong kwa muda mpaka huyo X ameaanza kumpigia simu usiku wa manane, kwangu mimi naona muda bado upo wa kuweza kutatua ili tatizo ni bora akachukua maamuzi mapema ya kulizungumzia hili suala na mumewe wake ingawa sijui mumewe atachukuliaje lakini inabidi tu amwambie otherwise mambo yatakuwa mabaya zaidi kama mumewe akigundua kabla ya yeye mwenyewe hajamwambia.Kwa mtazamo wangu nikiwa kwenye ndoa ,Najua haya maisha yana leo na kesho na hasa ukizingatia huyu dada kazaa na huyo X- wake kuna leo na kesho kuwa na mawasiliano si mbaya,Kwani inawezekana mtoto akapata tatizo ambalo baba yake anaweza kufahamishwa kwa namna moja au nyingine ,
Lakini huyu mwanaume si muungwana hata kidogo kwa nn amsumbue mwenzake wakati tayari anajua yuko kwenye ndoa yake ? hili nalo wanaume inabidi mjifunze kuwa makini kama maisha yamekuchanganya kwa nini ubebeshe lawama kwa mtu asiyehusika.?:sick:
Kama wengi walivyoshauri ni vyema dada huyu atafute namna ya kukaa na mmewe na kumweleza linalomkabili ingawa ,inawezekana pia mwanzo mme anaweza asimuelewe kwa sababu za wivu wa mapenzi lakini muda unavyokwenda atamuelewa mkewe .
kama alivyosema Michelle kwa nini anawasiliana na X wake
Dada anadai X-wake alimpigia simu akiwa kazini na kuanza kumweleza mlolongo wa matatizo kama binadamu alimsikiliza na mpaka mwisho kabisa alimweleza hataweza kumpa msaada wowote kwani yeye yupo kwenye ndoa na maamuzi yote wanafanya na mmewe
Ndipo alipoanza kuambiwa akumbuke fadhira.:coffee:
Huyu madame anasoma post hizi na imani atayafanyia kazi kabla ndo hii haijaingia matatani
Mungu ni mwema
Dah!!! Hata mimi?????