Dada kaanza kampeni mapema mno!

Dada kaanza kampeni mapema mno!

Kaanza mapema mno na hakika anaogopa upepo unaomtikisa!,Tena zaidi anaogopa upepo wakaka yake maana inaonekana upepo wa kaka ni mkali zaidi unampa shida,madira yake yanapeperuka huku na kule!.

Hakika dada hawezi kuvaa viatu vya kaka vimemshinda ndio maana ameanza kuviponda!.. niwaambieni yule mzazi wa kijani aliemzaa dada na kaka sasahivi ameharibikiwa kwani hawana sera tena zaidi ya kupondana wenyewe!,Moto unawaka tena moto wakijani.

Dada unamlaumu kaka kwani hujui sahivi hayupo..? Wakati akiwepo wewe si ulikuwa msaidizi wake..! Jua Kila anguko lake ni lako pia!,picha yake ilikuwa kubwa nawe tengeneza yakwako pasipo kukanyaga picha ya kaka! Adui zako sio waliokufa bali waliohai!.

Umefanya upatanisho na adui zako kwa kuingia mtegoni sasa umekosa adui umeanza kugusa visivyojitetea!. Sasa ni hivi kama alivyopita nawe utapita ila fahamu haya,hata Kama leo Kaka atasemwa vibaya ila hataacha kukumbukwa kwani toka katika ukuaji wake kazi zake nzuri zinafahamika. Asingeweza kukaa miaka kumi na bwana yule kama asingefanya vyema!. Ukweli huonekana dhahiri dada.

Ulipo ndipo kipimo kilipo sasa ni muda wa kufanya kazi na sio masimango,uzuri wa mtu hauji kwa kumponda mwengine tena ambae hawezi kusema!. wanaokupigia makofi hivi sasa wanakudanganya maana usitegemee uliozaliwanao wakakusaliti wakati wanajua umeshika sufuria la pilau na wanataka wazijaze sahani zao!. Tena wanataka ulegeze mikono ili wazijaze vizuri! Kaka yako alikaza mikono kwani alijua tabia za ndugu zake!.

Sisi unaotuona jamaa wa koo nyengine ndio tunaolima na kujaza wali hilo sufuria!,piganeni,gombanieni lakini msijisahau tunawaona na wewe ndio tunakuona vizuri zaidi.

Nikukumbushe ule muda bado haujafika,kazi ya mikono yako itakuja kuhesabika kushinda kazi ya mdomo.
Sio kila msaidizi anaishi kwa furaha na anayemsaidia. Msaidizi ni mfungwa wa utiifu na wakati mwingone hutamani siku ziende kasi aondokane na hicho kifungo.
Inaonesha dada hakuwahi kuwa furahani akiwa na kaka . Alifunika tu kombe...
Sasa kwa vile kaka hayupo ni muda kupumua kidogo na ku rewind memory card na kutikisa kichwa kwa mguno mhhh.
Dada ana moyo mzuri kwa mwonekano . Dada hawezi kuwa kama kaka akasalimia bila kubonyea kidogo.
Dada anataka vya kwake mwenye sio vya kaka na 2025 ndio muda wake.
La kwetu ni kupima kama kweli anaweza au hawezi kwa vigezo vinavyokubalika.
Ila ka kutoweza au kuweza kwa dada kunaanzia kwetu mjue. Akiweza tumeweza sisi akishindwa tumeshindwa sisi. Tupige kazi na kazi iendelee .
 
Kwani uwongo. Eti wewe kwako urais ni kufokafoka kuua watu hovyo hovyo kulamba matrilion hazina.

Yani jamaa kuruka ruka hovyohovyo hapa na Pale kama swala eti kwenu bonge la rais
Kama ni kwl Magufuli alikuwa akiua watu,
Mbona Magufuli hayupo tena na kuna watu bado wanaendelea kuuwawa na kupotea?

Kwa Mambo yanayoendelea sasa hapa inchini,

Kuendelea kutetea uozo ni Sawa na kujivua nguo mbele ya binti zako.
 
Lengo la kumfanya Ridhiwani Naibu waziri ni nini?

Kama sio kumuandaa kuwa Rais kama ilivyokua kwa karume na mwinyi?

Hivi ni lini hizi familia zitatupumzisha tukapata maendeleo kama taifa na sio kujali maslahi yao tu.
 
Wasukuma na MaCHADEMA jueni kwamba 2022-2030 Rais wa Tanzania ni Samia Suluhu Hassan. Mwanamke Mama na Kiongozi mwenye maono kuliko yeyote nchi hii.
Hutaki lalia moto. Bumbaaafu
 
Lengo la kumfanya Ridhiwani Naibu waziri ni nini?

Kama sio kumuandaa kuwa Rais kama ilivyokua kwa karume na mwinyi?

Hivi ni lini hizi familia zitatupumzisha tukapata maendeleo kama taifa na sio kujali maslahi yao tu.
tutaomba mabeyo atuongoze kuliko huyo aliekamatwa china na madawa
 
kule idodomya wagogo wanalonga eti hapakaliki mzimu unamsumbua 😄😄😄
 
Kaka alikufa siku nyingi, lakini hwaaishi kumsema na kumsengenya! Ni wakati wao wafanye kazi, tutakuja kuona.. mzee mmoja aliwahi kuniambia ukiona mbuzi yupo mtini ujue kapandishwa.
 
Dada ana wakati mgumu ni dhahiri chama limemuelemea na ameomba msaidizi kunbe ndio kaingizwa chaka zaidi.
Anaumizwa kwa kufuata nyayo za timu kutoka msioga
 
Hakuwa mtu sahihi alikuwa muuaji na katili sana mwizi wa ubabe huku akiwahadaa wajinga wajinga kwamba yey ni kiongozi wa wanyonge alikuwa muongo ndio maana anapendwa na wasio ma elimu
Kumbe wewe hapo una elimu?!! Tatizo lako hujaelimika kabisa kuna uwezekano ulihudhuria darasani tu lakini hukuelimika!
 
Back
Top Bottom