Dada kanifananisha au anataka nimtafune. Ushauri tafadhali

Dada kanifananisha au anataka nimtafune. Ushauri tafadhali

MR.NOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
339
Reaction score
505
Wakuu! Heri ya Mwaka 2023. Mwenzenu mwaka Jana umeisha Kwa kufananishwa na dada mmoja mrembo ambaye anauza duka la bidhaa za jumla na rejareja jirani na ninapokaa.

Huyu dada siku nimekaa Kwa Hilo duka Kuna ka pub jirani take,na yeye ni mtu asiyetumia kilaji kabisa na amenyooka katika Imani, lakini alinifuata hapo pub mbele ya watu na kuniambia teacher habari za siku ,ilibidi nimuulize nilikufundisha shule gani, akanitajia secondary moja huko Moro twn,nikauliza Tena SoMo Gani akasema civics .

Ilibidi nimkubalie tu maana niliona nitamfedhehesha mbele za watu lakini kiukweli Mimi sijawahi kuwa mwalimu na sijawahi kufundisha popote.

Baada ya hapo amekuwa akifurahi sana akiniona na akijitapa kwa wenzie kuwa Mimi ni mwalimu mzuri sana,nilimfundisha vizuri na pia amekuwa akinipa vi OFA vya kulazimisha hata kama sitaki. Nifanyeje wakuu.
 
Yaani kakufananisha unahisi anataka umtafune((anajilengesha)

Si kushambulii, ila naamini hizo huwa ni akili za kike.. Yaani mwanamke hapo ndio angefikiria unamtaka, ila wanaume kwa hatu ya kwanza unachukulia tru kakufananisha.

MFANO
ukikutana njiani na mwanamke ukimsimamisha akili yake ya kwanza anahisi unamtaka, ila sisi wanaume akili yetu ya kwanza tunahisi anahitaji msaada.
 
Jogoo wa siku hawakamatwi kwa punje ya mahindi.

Inabidi utumie ndoano.

Samaki nao wameshtukia ndoano ndio maana wanavuliwa kwa baruti.

Kuku ndio wanawapa jogoo mchele ili waliwe kwa wali.Mjini mambo mengi muda mchache.
 
Back
Top Bottom