--- AI imeboresha---
Dada yetu kipenzi, pole sana sana.
Kwa kifupi, mimi ni mdogo wako fulani. Ulipokuwa unajiandaa kugombea ubunge Kawe, nilikuonya usiwaamini wajumbe kabisa. Nilisema watakukula mpaka na mifupa huku wakikupa moyo.
Haikutosha, nikakushauri hata hizo pesa za kuwapa usizigawe ovyo, kwani wajumbe ni kama Yuda; wanapenda pesa utadhani wote wamezaliwa Marangu sehemu moja. Lakini linapokuja suala la kura, utawapenda kwelikweli! Hahaha, dada ulikuwa unajipa moyo tu.
Kando na hayo, wananchi wa Kawe walishasema hawataki kuongozwa tena na mwanamke, tangu yale yaliyowakuta kwa Halima Mdee. Walikuwa radhi wamchague hata jiwe, lakini si mwanamke mwingine. Haya maneno walikuwa wakiyasema punde tu walipomaliza vikao na wewe.
Pia, unahitaji kubadilika kimaneno. Kuna baadhi ya kauli zako, ulikuwa ukitoka tu kwenye kikao, wajumbe walikuwa wanasema, "Huyu anajifanya nani? Anatuwekea mikwara."
Hao ndio wajumbe; baba zao na mama zao ni tofauti, lakini damu zao zote zinanukia pesa.
Kila la kheri. Kama utakuwa hai, jaribu tena mwaka 2030.
Angalizo:
Tatizo sio jimbo la Kawe... tatizo ni WAJUMBE!
Sio watu wazuri, hahaha!
Wajumbe oyee!
The power of wajumbe! Wengine wanacheka tu.