Dada wa kazi atoweka na watoto wawili mara baada ya kwenda dukani

Dada wa kazi atoweka na watoto wawili mara baada ya kwenda dukani

Mohammad Kassim ambaye ni Baba Mzazi, ametangaza kupotelewa na Watoto wake wawili ( wanaoonekana pichani ), ambao wamepotea jana jioni majira ya saa kumi na mbili maeneo ya Temeke Jijini Dar es salaam wakiwa na Dada wa Kazi.

Akizungumza Kassim amesema Dada huyo wa kazi ambaye jana ilikua ni siku ya tatu tangu kuanza kufanya kazi kwenye Familia hiyo, aliondoka na Watoto hao akiaga kuwa anakwenda nao Dukani lakini wakatokomea moja kwa moja.

Soma Pia:
“Aliowachukua Watoto ni Dada wa kazi aliyekaa nao kwa siku tatu tu, inaonekana kuiba Watoto ndilo lilikua lengo lake kwasababu baada ya kutokomea simu yake haipatikani na hata wale waliomuunganisha kupata kazi kwetu nao simu zao hazipatikani, tunaomba Watanzania watusaidie kusambaza taarifa hizi” - Kassim ameiambia AyoTV.

“Tunaomba yeyote mwenye taarifa za Watoto hawa aende Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nae au anipigie kwa namba yangu 0744-555-574” - Kassim.

View attachment 3200914
mkiishi na wafanyakazi msiwanyanyase!!!
 
Alafu vidada vya hivyo vinajifanyaga vinajua dini hivyo

Kila dakika salamaleko na ushungi juu kumbe vizi tu

Pole sana kwa Baba na Mama waliopotelewa na watoto
Siyo tu salamaleko na pia huwa na bwana asifiwe na tumaini letu nyingiiiii.
 
mkiishi na wafanyakazi msiwanyanyase!!!
Mengine yana roho mbaya tu hata usipolinyanyasa lawaza fanya ubaya.
Niliishi na house girl kama mtotowangu nikampeleka shule na huduma nzuri sana lakini hakuwa mwema hata kidogo mwisho wa yote aliiba mtoto akishirikiana na Jirani MUNGU NI MWEMA WAKATI WOTE ALIMUOKOA MWANANGU KABLA YA SAA 24 KUFIKA
 
Mengine yana roho mbaya tu hata usipolinyanyasa lawaza fanya ubaya.
Niliishi na house girl kama mtiyowangu nikampeleka shule na huduma nzuri sana lakini hakuwa mwema hata kidogo mwisho wa yote aliiba myoto akishirikiana na Jirani .
jini likujualo halikuli ukaisha!!!!,,,,,manyanyaso si kumnyima chakula tu,ata maneno ya asimango ni hatari,,,hivi unajua chanzo cha UGAIDI???,,,,,,,,,,,,magaidi ni wa2 waliochoshwa na mfumo kandamizi,so wanaamua kufanya lolote baya ili kulipiza kisasi,,,ujue,ata kwa sisi wafugaji,ukijijua wewe ni mlevi usipipige mbwa koko ,wakikufamania ukiwa umelewa na wao wapo kwenye kipindi chao cha kupandana[joto] utaokotwa ukukiwa umetafunwa,,,,,ata hao masela unaowaona mtaani hawaheshimiki,,,wewe kwa nafasi yako waheshimu tu kwani watakusaidia siku moja!!
 
jini likujualo halikuli ukaisha!!!!,,,,,manyanyaso si kumnyima chakula tu,ata maneno ya asimango ni hatari,,,hivi unajua chanzo cha UGAIDI???,,,,,,,,,,,,magaidi ni wa2 waliochoshwa na mfumo kandamizi,so wanaamua kufanya lolote baya ili kulipiza kisasi,,,ujue,ata kwa sisi wafugaji,ukijijua wewe ni mlevi usipipige mbwa koko ,wakikufamania ukiwa umelewa na wao wapo kwenye kipindi chao cha kupandana[joto] utaokotwa kukiwa umetafunwa,,,,,ata hao masela unaowaona mtaani hawaheshimiki,,,wewe kwa nafasi yako waheshimu tu kwani watakusaidia siku moja!!
Yaani kwangu hayo hayapo ni ndugu kama ndugu nimeishi na house girls 4 na wote leo wanamaisha bora zaidi Elimu kazi na ndoa zenye kueleweka.
Unapo ishi na house kumbuka ana maisha zaidi ya kuwa dadawakazi.
YAPASA KUMJENGEA UWEZO WA MAISHA YAKE YA BAADAE NAWE UTABARIKIWA.
Lakini kwasasa house girl wengi sio waaminifu.
 
Yaani kwangu hayo hayapo ni ndugu kama ndugu nimeishi na house girls 4 na wote leo wanamaisha bora zaidi Elimu kazi na ndoa zenye kueleweka.
Unapo ishi na house kumbuka ana maisha zaidi ya kuwa dadawakazi.
YAPASA KUMJENGEA UWEZO WA MAISHA YAKE YA BAADAE NAWE UTABARIKIWA.
Lakini kwasasa house girl wengi sio waaminifu.
sawa mazee!!!!! bu "KARMA is REAL"
 
Back
Top Bottom