A
Anonymous
Guest
Naomba msaada kwa ajili ya dada yangu, ambaye ni mtumishi wa umma kwa sasa. Anapitia hali ngumu sana kiafya na kiutumishi, na hadi leo hajapatiwa msaada unaostahili.
Alipata ajali mwaka 2024 mwezi Oktoba akiwa anafanya kazi katika kiwanda cha vyombo vya plastiki Kibada, Kigamboni, ambapo mkono wake ulivunjika vibaya. Alifanyiwa upasuaji wa kwanza, kisha wa pili mwezi Februari 2025. Baada ya matibabu hayo alianza kuimarika, hasa alipokuwa akiishi Rufiji ambako hali ya hewa ni ya joto.
Mwezi Mei 2025 alipata ajira kama mtendaji wa kijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Hata hivyo, tangu alipofika Moshi, hali ya hewa ya baridi imekuwa ikimletea maumivu makali kwenye mkono wake kila siku. Ilibidi aripoti kwa mkurugenzi wake, ambaye alimshauri aende hospitali kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Baada ya kufika Hospitali ya Muhimbili, madaktari walimueleza kuwa kutokana na kufanyiwa upasuaji mara mbili, anatakiwa kuishi katika maeneo yenye hali ya hewa ya joto ili kuepuka maumivu. Walimpa ripoti rasmi ya kitabibu inayoshauri akae sehemu yenye joto muda mwingi.
Tuliporudi Moshi na kuwasilisha ripoti hiyo kwa mkurugenzi, tulielezwa kuwa bado hajathibitishwa kazini, hivyo akaandike barua kwenda kwa Katibu Mkuu ili kuomba uhamisho. Tulijaribu kufuatilia TAMISEMI, lakini hatukufanikiwa kukutana na wahusika wakuu—tuliambiwa watawasiliana na Afisa Utumishi wa Moshi, lakini hadi sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Kwa sasa, anaendelea kuteseka sana na baridi ya Moshi, hali inayozidisha maumivu yake kila siku. Pia, licha ya kuwa kazini kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, bado hajapewa barua ya kuthibitishwa kazini.
Tunaomba sana mamlaka husika ziangalie kwa huruma suala hili. Anaomba uhamisho kwenda Mkoa wa Pwani, Halmashauri ya Mji wa Rufiji, ambako hali ya hewa ni rafiki kwa afya yake. Hali yake siyo nzuri, na anahitaji msaada wa haraka ili aweze kuendelea na maisha na kazi kwa hali bora zaidi.”