KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkiwashitaki mahakamani na ikathibitika kuwa walifanya uzembe, mtalipwa fidia.

Wapelekeni mahakamani ili liwe fundisho kwa wengine.
 
Hapa ishu naona ni counseling, Kwa hx hiyo ya mgonjwa plus Dx hiyo na ukizingatia muda ambao mgonjwa ameumwa ukweli ni kwamba ndugu yetu alikuwa very serious. Pole mkuu ila km unaona hujatendewa haki Chukua hatua zaidi.
 
Mkuu pole sana kwa kufiwa na dada yako lakini mkiambiwa kuwa mujaribu na kutumia Dawa za Asili kutibu maradhi sugu kama hayo ya Saratani Ukimwi Hepatiti B Virus maradhi ya kisukari na maradhi Presha munadharau dawa za asili maradhi hayo niliuyoyataja hakuna dawa Yoyote ya Hospitali itakayoweza kutibu na kuponyesha mgonjwa. Ukimpeleka mgonjwa Hospitali akiwa na hayo maradhi ujuwe unampeleka kwenda kwenye kifo kwani hataweza kupona kwa dawa za Hospitali sio rahisi kabisa.Pole sana na uguwa pole kwa kumkosa Dada yetu RIP.
Sasa dawa za asili ni zipi na zinapatikana wapi?je uliwahi kwenda hospital kuwaeleza hizo dawa zako ili wajaribu?
 
Kama ningalikua Mimi baada ya sis kufariki ningerudi muhimbili ningetembeza ngumi hadi askari waje wanichukue…. Najua ningeenda jela tu

Pole sana mkuu.
 
Nilikuwa na mgonjwa wangu ambaye alikuwa anasumbuliwa na Saratarani, alikuwa anapatiwa huduma Ocean Road, tukiwa hapo tukapata referral ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga), Dar es Salaam.

Wakati tunaelekea Muhimbili tukapita Hindu Mandal kwa kuwa kuna Daktari ambaye pia tulihitaji kumuona, wakati tukiwa hapo tukapata huduma nzuri tu ya muda.

Tukapatiwa Ambulance iliyotupeleka hadi Muhimbili, wakampokea vizuri mgonjwa na kumpa huduma mbalimbali.

Muda mfupi baadaye wakatuambia kuwa tunatakiwa kulipia chumba kwa gharama ya Shilingi 50,000, pale Mwaisela, huku akiwa anaendelea kupatiwa matibabu ikiwemo kupewa Oxygen kwa kuwa mgonjwa alionakana ana shida ya kupumua.

Baada ya kulipa, wakatuambia hakuna vitanda hivyo wanataka kutupeleka Hospitali ya Mloganzila.
Sisi tukakataa, muda huo ni saa kumi alfajiri, tukawambia tunaomba kama kweli hakuna kitanda basi mgonjwa abaki pale ‘Emergency’ hadi asubuhi kwa kuwa tayari tulishalipia chumba na kuanza kuangaika n ambulance kuelekea Mloganzila wakati tumeshafanya vipimo na taratibu nyingine itakuwa ni usumbufu na pia sio njema kwa mgonjwa.

Ukatokea ubishani pale, sisi tukakataa, lakini Madaktari wa Muhimbili waliokuwepo wakafanya maamuzi ya kibabe wakasema mgonjwa wetu anaingizwa kwenye Ambulance kupelekwa Mkoganzila.

Wakati wakifanya maamuzi hayo, kuna Nesi mmoja akasema “fanyeni haraka Oxygen inaisha”.

Walipofika Kimara, ndugu yetu aliyekuwa kwenye Ambulance akanijulisha kuwa Oxygen imekata, hadi wanafika Mbezi tayari Oxygen ilikuwa imeshakata na mgonjwa wangu akafariki.

Inawezekana ni siku yake ilikuwa imewadia lakini kilichotokea ni uzembe wa baadhi ya Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili na watendaji wengine kadhaa waliokuwepo.

Kwanza najiuliza kwanini walitulipisha kitanda wakijua hakuna kitanda, pili kwanini walimwekea mgonjwa Oxygen kidogo na kwa kauli iliyotolewa pale ni wazi walijua hiyo haitamfikisha Mgonjwa Mloganzila.

Tatu kulikuwa na haja gani ya kumpeleka Mloganzila wakati tayari kulikuwa kunaelekea kukucha na mmoja wa Madaktari aliwaambia wenzake tubaki pale lakini wenzake hawakumsikiliza.
Baada ya msiba nilipouliza mmoja wa Madaktari wa Muhimbili kwanini walitupa Oxygen kidogo anadai lile lilikuwa jukumu la watu wa Ambulance kukagua na sio jukumu lao.

Walichokifanya Madaktari hao wa Muhimbli waliokuwa zamu Usiku wa tukio hakikuwa cha kibinadamu na kama wanafanya hivi basi maisha ya watu wengi yapo hatarini.

Kwa nini nimewasilisha malalamiko yangu hapa JamiiForums, nataka Dunia ijue kuwa kuna baadhi ya Watumishi wa Muhimbili wanatakiwa kujirekebisha, najua roho ya dada yanu haiwezi kurudi ila basi angalau wasingetuonesha wazi kuwa wanataka ndugu yetu afe, pia iwe somo kwa wengine wawe makini.
View attachment 3065744
Miamala ya malipo tuliyofanya kabla ya Mgonjwa kulazimishwa kupelekwa Mloganzila
Tanzania ni miongoni mwa nchi ngumu Sana hapa duniani kwa Wananchi kuishi kwa amani na utulivu bila kupata misukosuko kutoka kwa Watawala.
 
Baada ya msiba nilipouliza mmoja wa Madaktari wa Muhimbili "kwanini walitupa Oxygen kidogo anadai lile lilikuwa jukumu la watu wa Ambulance kukagua na sio jukumu lao.

Walichokifanya Madaktari hao wa Muhimbli waliokuwa zamu Usiku wa tukio hakikuwa cha kibinadamu na kama wanafanya hivi basi maisha ya watu wengi yapo hatarini."
 
Poleni sana. Bado nasisistiza: hii nchi bila raia kujua wajibu wao wa kuhakikisha tunapata viongozi wawajibikaji na kuwasimamia tusitegemee mazuri. Kla mtu atakumbukana na madhara ya CCM kwa wakati wake. Na Samia pamoja na uozo wake wote ameshasema yuko kwenye madaraka mpaka 2030 ndiyo anarudi Kisimkazi. Utadhani ana mkataba na Mungu.
 
Nilikuwa na mgonjwa wangu ambaye alikuwa anasumbuliwa na Saratarani, alikuwa anapatiwa huduma Ocean Road, tukiwa hapo tukapata referral ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga), Dar es Salaam.

Wakati tunaelekea Muhimbili tukapita Hindu Mandal kwa kuwa kuna Daktari ambaye pia tulihitaji kumuona, wakati tukiwa hapo tukapata huduma nzuri tu ya muda.

Tukapatiwa Ambulance iliyotupeleka hadi Muhimbili, wakampokea vizuri mgonjwa na kumpa huduma mbalimbali.

Muda mfupi baadaye wakatuambia kuwa tunatakiwa kulipia chumba kwa gharama ya Shilingi 50,000, pale Mwaisela, huku akiwa anaendelea kupatiwa matibabu ikiwemo kupewa Oxygen kwa kuwa mgonjwa alionakana ana shida ya kupumua.

Baada ya kulipa, wakatuambia hakuna vitanda hivyo wanataka kutupeleka Hospitali ya Mloganzila.
Sisi tukakataa, muda huo ni saa kumi alfajiri, tukawambia tunaomba kama kweli hakuna kitanda basi mgonjwa abaki pale ‘Emergency’ hadi asubuhi kwa kuwa tayari tulishalipia chumba na kuanza kuangaika n ambulance kuelekea Mloganzila wakati tumeshafanya vipimo na taratibu nyingine itakuwa ni usumbufu na pia sio njema kwa mgonjwa.

Ukatokea ubishani pale, sisi tukakataa, lakini Madaktari wa Muhimbili waliokuwepo wakafanya maamuzi ya kibabe wakasema mgonjwa wetu anaingizwa kwenye Ambulance kupelekwa Mkoganzila.

Wakati wakifanya maamuzi hayo, kuna Nesi mmoja akasema “fanyeni haraka Oxygen inaisha”.

Walipofika Kimara, ndugu yetu aliyekuwa kwenye Ambulance akanijulisha kuwa Oxygen imekata, hadi wanafika Mbezi tayari Oxygen ilikuwa imeshakata na mgonjwa wangu akafariki.

Inawezekana ni siku yake ilikuwa imewadia lakini kilichotokea ni uzembe wa baadhi ya Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili na watendaji wengine kadhaa waliokuwepo.

Kwanza najiuliza kwanini walitulipisha kitanda wakijua hakuna kitanda, pili kwanini walimwekea mgonjwa Oxygen kidogo na kwa kauli iliyotolewa pale ni wazi walijua hiyo haitamfikisha Mgonjwa Mloganzila.

Tatu kulikuwa na haja gani ya kumpeleka Mloganzila wakati tayari kulikuwa kunaelekea kukucha na mmoja wa Madaktari aliwaambia wenzake tubaki pale lakini wenzake hawakumsikiliza.
Baada ya msiba nilipouliza mmoja wa Madaktari wa Muhimbili kwanini walitupa Oxygen kidogo anadai lile lilikuwa jukumu la watu wa Ambulance kukagua na sio jukumu lao.

Walichokifanya Madaktari hao wa Muhimbli waliokuwa zamu Usiku wa tukio hakikuwa cha kibinadamu na kama wanafanya hivi basi maisha ya watu wengi yapo hatarini.

Kwa nini nimewasilisha malalamiko yangu hapa JamiiForums, nataka Dunia ijue kuwa kuna baadhi ya Watumishi wa Muhimbili wanatakiwa kujirekebisha, najua roho ya dada yanu haiwezi kurudi ila basi angalau wasingetuonesha wazi kuwa wanataka ndugu yetu afe, pia iwe somo kwa wengine wawe makini.
View attachment 3065744
Miamala ya malipo tuliyofanya kabla ya Mgonjwa kulazimishwa kupelekwa Mloganzila
Hii post imenipa simanzi kubwa sana.
Pole ndugu yangu kwa kupoteza dada kipenzi.

Serikali sasa inafanya biashara ya tiba ndo maana hata marehemu anazuiwa ili watu walipe bill.

Muhimbili siku hizi imejaa watumishi ambao WITO ni aghalabu kuwa nao.

Serikali imetuumiza sana
 
Pro pesa jaanaabii analeta siasa tu yani hospitali hiyo tangu aondoke mzee prof asiyetaka kiki Museru pamekuwa pahovyoooooo yani sijui wamekuaje kutwaaa kutafuta kiki mitandaoni lakini ufanisi zero, Pole sana mkuu tafuta wakili matata sana ufungue kesi hilo lisipite hivihivi.
 
Kuna hospital kama huna ndgu daktari hapo au huna hela ya kumnunua daktari ili mgonjwa wako ahudumiwe inavyostahili basi bora ungeenda dispensary ya mtaani tu utapoteza nduguyo na vihela vyako kidg hvyohvyo

Oxygen utaambiwa amna kitanda amna xray haifanyi kaz ambulance mbovu ct scan haipo ilimradi usiwasumbue
 
Pro pesa jaanaabii analeta siasa tu yani hospitali hiyo tangu aondoke mzee prof asiyetaka kiki Museru pamekuwa pahovyoooooo yani sijui wamekuaje kutwaaa kutafuta kiki mitandaoni lakini ufanisi zero, Pole sana mkuu tafuta wakili matata sana ufungue kesi hilo lisipite hivihivi.
Jsmaa kawa siasa sana.
 
Back
Top Bottom