KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkiwashitaki mahakamani na ikathibitika kuwa walifanya uzembe, mtalipwa fidia.

Wapelekeni mahakamani ili liwe fundisho kwa wengine.
 
Hapa ishu naona ni counseling, Kwa hx hiyo ya mgonjwa plus Dx hiyo na ukizingatia muda ambao mgonjwa ameumwa ukweli ni kwamba ndugu yetu alikuwa very serious. Pole mkuu ila km unaona hujatendewa haki Chukua hatua zaidi.
 
Sasa dawa za asili ni zipi na zinapatikana wapi?je uliwahi kwenda hospital kuwaeleza hizo dawa zako ili wajaribu?
 
Kama ningalikua Mimi baada ya sis kufariki ningerudi muhimbili ningetembeza ngumi hadi askari waje wanichukue…. Najua ningeenda jela tu

Pole sana mkuu.
 
Tanzania ni miongoni mwa nchi ngumu Sana hapa duniani kwa Wananchi kuishi kwa amani na utulivu bila kupata misukosuko kutoka kwa Watawala.
 
Baada ya msiba nilipouliza mmoja wa Madaktari wa Muhimbili "kwanini walitupa Oxygen kidogo anadai lile lilikuwa jukumu la watu wa Ambulance kukagua na sio jukumu lao.

Walichokifanya Madaktari hao wa Muhimbli waliokuwa zamu Usiku wa tukio hakikuwa cha kibinadamu na kama wanafanya hivi basi maisha ya watu wengi yapo hatarini."
 
 
Hii post imenipa simanzi kubwa sana.
Pole ndugu yangu kwa kupoteza dada kipenzi.

Serikali sasa inafanya biashara ya tiba ndo maana hata marehemu anazuiwa ili watu walipe bill.

Muhimbili siku hizi imejaa watumishi ambao WITO ni aghalabu kuwa nao.

Serikali imetuumiza sana
 
Pro pesa jaanaabii analeta siasa tu yani hospitali hiyo tangu aondoke mzee prof asiyetaka kiki Museru pamekuwa pahovyoooooo yani sijui wamekuaje kutwaaa kutafuta kiki mitandaoni lakini ufanisi zero, Pole sana mkuu tafuta wakili matata sana ufungue kesi hilo lisipite hivihivi.
 
Kuna hospital kama huna ndgu daktari hapo au huna hela ya kumnunua daktari ili mgonjwa wako ahudumiwe inavyostahili basi bora ungeenda dispensary ya mtaani tu utapoteza nduguyo na vihela vyako kidg hvyohvyo

Oxygen utaambiwa amna kitanda amna xray haifanyi kaz ambulance mbovu ct scan haipo ilimradi usiwasumbue
 
Jsmaa kawa siasa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…