Mbwichichi
JF-Expert Member
- Dec 19, 2018
- 297
- 1,687
Poleni na pilika na mbio mbio za maandalizi ya uchaguzi,vita ya congo na changamoto binafsi za maisha.
Mimi Mbwichichi katika kuhangaika kwangu kuyatafuta maisha nimebahatika kukutana na watu mbalimbali wa kila aina,zaidi nimejifunza sana kutambua saikolojia za watu baada tu ya kuona matendo yake kwa muda mfupi au baada ya kuongea kauli chache tu.Kwahiyo niko makini sana kwenye kujua nani ni nani na ninavyodeal naye nideal naye kwa angle gani.
Basi bhana…Nina dada yangu ambaye kiumri ni kama tunalingana tu,kwa umri alionao sasa hivi anatosha kabisa kuitwa “shangazi” na bado hajaolewa ila ndio vile watoto wa mjini walishamuwahi wakatia mimba na ana mtoto “single mother” Ninaandika uzi huu baada ya kurudi nyumbani kwa ajili ya kumjulia hali mzee ambaye hali yake ya kiafya sababu ya umri siyo nzuri sana.
Bahati nzuri katika kurudi tukacollide na sister nyumbani,lakini mara hii akiwa kaambatana na kijana mmoja ambaye nyumbani alimtambulisha “rafiki yake” ,rafiki huyu wanafanya naye kazi na kamuomba amuendeshe kwenda nyumbani sababu yeye sister hakua kwenye hali nzuri ya kuendesha gari lake.
Sababu ilibidi alale basi alimtafutia lodge ya karibu hapo na yeye sister alilala home na kuendelea na ratiba za kawaida za nyumbani kama ilivyo desturi zetu.
Kwa sababu ya ukaribu wa umri kati yetu ilikua rahisi kunitambulisha “privatelly” kwamba huyo ni shemeji yangu na wako kwenye michakato ya kutambulishana siku moja wawe rasmi mke na mume.
Lakini pia alinitambulisha kamba huyo bwana anafanya kazi “nyeti” na ilibaki hivyo tu,kwa akili ya kawaida nilijiongeza kwamba huyu bwana ni kitengo maalumu hawa wanaojiita watu wa mama,vijana wa dodoma na kizimkazi.
Unajua tena wanawake wakipata bwana…akawa free kuniambia jinsi gani kapata mtu wa maana,kwamba hatumii pombe na ni mtu wa sala sana,siyo kama wanaume wengine ambao ameshawahi kutana nao wakaishia kumuumiza moyo….jamaa kwa wakati niko naye pale muda wote kambeba mtoto wa sister na kila akichafuka anamfuta vumbi na zile care zote anafanya dingi mwenye mapenzi makubwa sana na mtoto wake…..mi machale yakaanza😇🔊
Basi nikasema haya….lakini nikaanza kushtuka baadhi ya mambo kutoka kwa yule bwana,kama nilivyosema ni mtaalamu sana wa kuona vitu kwa watu ambavyo wengine hawaoni.
1. wakati tunaondoka nyumbani tumeshaagana jamaa alimtonya sister kijanja wakaenda pembeni kidogo,wakati wakijua hakuna anayewacheki basi mimi jicho langu lilikua active…alitoa ishara kwamba hana pesa,sister alifungua pochi akampatia pesa ya kutosha hivi,mwana anaikunja akaiweka mfuko wa tako chap….nikapata kitu hapo💥
2. huyu jamaa alivaa suti ya kaunda ya damu ya mzee akiwa na kilabel cha bendera ya taifa kifuani kushoto,muda wote alikua kapiga tinted nyeusi na mkimya sana sana…nikasema haya sawa😃
3. tukaondoka zetu kwenda walikokubaliana atalala,tulifika kufanya booking na malipo,mi nikakausha nione atafanya nini,alichukua simu kapiga kwa namba ambayo namna ya maongezi yao yaliniambia ni sister…mwisho wa maongezi ilikua ni kutumwa lipa namba ili sister afanye muamala kwa ajili ya chumba…nikasema huyu mbona ana mashaka?!!…kama mtu kweli (a) hawezi kuomba pesa ya kulipia chumba (b) alipewa pesa tunavyotoka,kama yuko timamu alitakiwa lipia ile pesa alipewa kiungwana.
3. tukakaa zetu mara akaniambia anapata wapi m-pesa,alienda kuweka pesa pale akafanya muamala fulani wa kutuma pesa ambao sikutambua ni kwenda kwa nani ila nina uhakika haikua kwenda kwa sister…hii siyo issue sana,lakini iliacha pia alarm kichwani mwangu.
4. niliagiza pombe zangu “tusker lager” baridi tano…yeye akaagiza “red bull” nikamtania kiongozi hupigi vitu????😂😂😂😂😂 akasema yeye hapigi labda kwa dharura sanaaa na anapigaga tu pombe kali ile kistar siyo hizi kama nazopiga mimi….nikasema sawa kiongozi.
Kikweli sura yake anaonekana ni mlevi aliyetopea…nikasema huyu muache tu avunge….haikupita muda akasema wacha nijiboost kidogo akapmba k-vant
😅😅😅 ikawa sasa kafungilia mbwa….yule bwana kitengo ni mlevi mtepetevu….wale watu konki,alikunywa ile na kuchanganya kila pombe…bila kujali sare zake za “kazi” na nembo ya bendera alianza kukatika hadharani pale huku akiimba kila wimbo kwa kumuita DJ na kila fujo inayofanywa na mlevi mzoefu.
Alitoa miwani mpaka viatu….mimi nilichofanya cha “kinoko” ni kumrekodi tu video kwa ajili ya masuala yangu ya “ujasusi” ili kuweka kumbukumbu sawa mbeleni.
Basi bhana…:sababu ya hali yake wakati wa bili alishindwa kulipa nikaingia mfukoni nikalipa,nikahakikisha kaingia chumbani kwake na kalala….nikachukua zangu boda nikarudi kulala nyumbani.
Kesho yake asubuhi ilibidi nikamfate kwa ajili ya wao kuja kuaga na kuondoka…..
Ebwanaaaa eehh…..yule bwege nilimkuta kapiga vitu vyake saaaafi sana,smart na makini kama ambavyo alikua hajalewa jana,ukiambiwa alilewa hadi kusahau viatu na miwani huwezi amini….karudi kwenye “default” setting za kumdanganyia sisiter kwamba yeye ni mtu mwema sana.
Ndio kwabza akauliza kama jana alifanya kitu chochote kilichoacha alama mbaya,nikamuambia hakuna kitu blaza…akaomba malimao,tangawizi nk kwa ajili ya kukata harufu.
All i all…..kwa uzoefu wangu huyu jamaa nimeconclude ni TAPELI….yuko kwa sister kimkakati kwa hiyo hata akifanikiwa kumuoa basi ni kwa mkakati,kutumia advantage ya umri na usingo maza wa sister kaona fursa ya kuishi pale kwa kitonga.
Sasa kuna haja ya kuanza kumpanga sister au niache nione mwisho itakuaje? sababu hata mimi baada ya kupata changamoto kwenye utafutaji bado nasubiria wakati wa kuoa nioe ila home naonekana miyeyusho sana na mtu wa ovyo….lakini suala ni woga wa kurudia tena makosa.