frem zero
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 595
- 875
Habari zenu wakuu. Mimi ni binti wa miaka 25 ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano. Nina dada yangu ambaye ni wa tatu kuzaliwa, ndugu huyu ananifanya niishi kwa wasi wasi na huzuni kuu huku nilipo, kwa sababu mara kwa mara amekuwa akitishia kujiua yeye na kumuua mtoto wake.
Sabababu kubwa ya kufanya hivyo ni madeni. Dada yangu huyu mnamo mwezi wa nane alichukua mkopo katika bank fulani wa shilingi milion kumi ambao ataulipa ndani ya miaka mitano. Cha kusikitisha hakufanyia kitu cha maana sana zaidi ya kubadili vitu vyote vya ndani, akanunua viwanja viwili na nyingine akalewea pombe na kuwapa ofa marafiki zake.
Hadi imefika mwezi wa tisa mkopo wote ukawa umeisha, akawa mtu wa kuomba omba. Hapo ndipo akaamua kukopa mitaani kwa watu wanaokopesha fedha kwa riba. Akawa anadaiwa kama laki nne. Sasa ikawa akipata mshahara analewea wote na akilewa anamtukana mwenye nyumba na kutishia kumuua mtoto wake na kujiua yeye mwenyewe(mtoto ana miaka kumi).
Kutokana na hali hiyo mwenye nyumba akamsitishia mkataba na kumrudishia hela iliyobakia na akamwambia ahame. Kweli dada yangu alihama lakini hakuwa na pa kwenda hivyo vyombo vyake akawekeza kwa majirani. Sasa akawa mtu wa kutangatanga mara alale barazani mara nje na kazini akawa haendi. Wakati huo mtoto wake kamuwekeza kwa majirani.
Habari zote za yeye kufukuzwa nilipigiwa simu na msamaria mwema mmoja ambae alifanikiwa kuchukua namba yangu wakati dada yangu akiwa amelewa.
Baada ya kupata taarifa hizo niliamua kuwapigia ndugu zangu wakubwa na kuwaeleza. Hakuna aliejali majanga anayopitia dada yangu huyo kila mtu yupo bize na maisha yake madai yao ni kuwa kama huyo dadangu kaona pombe inamsaidia basi aendelee nayo.
Sasa wiki iliyopita huyu dada yangu alienda kwa dada yetu mkubwa ambae kafanikiwa kujenga maeneo ya tabata. Alipofika huko alileta vurugu sana na akatishia kuichoma moto nyumba.
Kutokana na matendo yake ndugu wamemsusa kabisa hakuna anaetaka kujua habari zake. Yaani amekuwa mpweke sana hana msaada , kwa kifupi hakuna anayemjali. Kadiri siku zinavyozidi kwenda roho ya kutamani kujiua naona imemkolea.
Leo hii nimeongea nae kwa simu akasema kuwa niende nikachukue vitu vyake vyote vya ndani kwa sababu hataki mtu yeyote avichukue atakapokufa. Sio siri roho inaniuma sana nimejaribu kuongea nae mara kwa mara kuwa asiyakimbie matatizo kwa kukikaribisha kifo lakini hanielewi. Nikiwaeleza ndugu wakubwa wananijibu mwache afe ila mtoto amuache kwa kweli nazidi kukata tamaa ya kumuepusha dada yangu huyu katika roho ya mauti.
Namnukuu juu ya kifo alichochagua anasema" NITAMPA MWANANGU SUMU AKIANZA KUTATARIKA/KUHANGAIKA NA MIMI NAKOROGA SUMU NAKUNYWA ILI TUFE PAMOJA. Nampenda sana dada yangu sitaki kumpoteza hata kidogo.
Ndugu zangu wanajamii forum wakubwa kwa wadogo naombeni mnishauri nifanye nini juu ya dada yangu asipate mawazo ya kujiua na kumuua mtoto wake? Mwenzenu chakula hakipiti kooni kwa mawazo[emoji22] [emoji22]