Dada yangu anatishia kujiua, nishaurini tafadhari

Nasisitizaem zero,mwenye nia9777dhatimber: yenu2anayetaka kikubwa bihuyokili ni hasara kwa miguu yako. Kama huna cha kuchangia ungekaa kimya tu wala kisingeharibika kitu. Acha kujichoresha kwa upumbavu wako mtu mzima hovyooi[/QUOTE]
Nasisitiza hakuna mwenye nia ya dhati kati yenu anayetaka kumsaidia huyo mtoto.
 
Kichwa kikubwa bila akili ni hasara kwa miguu yako. Kama huna cha kuchangia ungekaa kimya tu wala kisingeharibika kitu. Acha kujichoresha kwa upumbavu wako mtu mzima hovyooi
Watu wanakaa na watoto waliozaliwa na vichaa na hao vichaa kila siku wanawadai watoto wao bado wanakomaa sembuse huyo ndugu yenu anayetishia kumuua mtoto.
 
Hana maumivu yoyote huyo mleta mada, kama angekuwa nayo kuna juhudi za awali angechukua kumsaidia ndugu yake kabla yakuomba ushauri. Wote wanakwepa majukumu.
Hivi mpaka mtu kaamua kuomba ushauri ina maana kuna njia kajaribu zimeshindikana, msaada wa karibu hakuna. Je nimbebe mgongoni ndo utaelewa? Ndo maana nikasema naomba ushauri ina maana uwezo wangu wa kufikiri umefika mwisho hivyo nahitaji mawazo ya watu wengine ili nifike mwisho. Fikiri kwa makini kabla hujaongea ili kulinda heshima yako.
 
Kwenu wote mna roho mbaya kwa maelezo yako hayaonyeshi kama kunajuhudi zozote mmefanya za kumsaidia mtoto na huyo ndugu yenu.
Watoto katika familia ni sawa na vidole vya mikononi. Vidole vina shepu tofauti tofauti hivyo hata watoto pia kitabia hawawezi kufanana hivyo usilazimishe tufanane. Tuache na roho mbaya yetu we mwenye roho nzuri endelea na mambo yako
 
Hivi mpaka mtu kaamua kuomba ushauri ina maana kuna njia kajaribu zimeshindikana, msaada wa karibu hakuna. Je nimbebe mgongoni ndo utaelewa? Ndo maana nikasema naomba ushauri ina maana uwezo wangu wa kufikiri umefika mwisho hivyo nahitaji mawazo ya watu wengine ili nifike mwisho. Fikiri kwa makini kabla hujaongea ili kulinda heshima yako.
Ikiwezekana mtoto mbebe mgongoni, aiwezekani mtoto atishiwe maisha na mama yake then anakuja kwako kumchukua mtoto huyohuyo na wewe kwa akili yako unamkabidhi!!.
 
Chikueni mjomba wenu endeleeni na maisha yenu subirini kuzika huyo mfu!kifo hakikimbiwa kila mtu atakufa at a certain time na huyo keshamaliza maisha yake amebakiwa na uhai tu subirini hitimisho na kama nyie waislam basi jitayarisheni kumlipia madeni yake maana kwa taratibu za kiislam kufa na madeni ni mushkel kwa maiti labda wadeni wakusamehe.
Na kama hamtaki kufika huko basi chukueni dada yenu uzeni hivyo viwanja lipeni madeni na mumsaidie kurejesha maisha yake .
Pia kwa mujibu wa maelezo yako inaonekana familia yenu haiko tight kivile !unaogopa asife pia hauko pale kumsaidia?undugu maana yake for better or for worse you should have been there for her to give her strenght to guide her to mend her life am assuming hata dogo atakuwa uswazi tu school haend ilhalu wajomba na mashangazi mpo!
Asante kwa ushauri wako
 
Huu ndio undugu,kumpenda ndugu yako hta kama anashida nyingi au tabia mbaya kias gani
 
Watoto katika familia ni sawa na vidole vya mikononi. Vidole vina shepu tofauti tofauti hivyo hata watoto pia kitabia hawawezi kufanana hivyo usilazimishe tufanane. Tuache na roho mbaya yetu we mwenye roho nzuri endelea na mambo yako
Ukweli ndio huo ndio maana dada yenu anaona afadhari afe pamoja na mtoto wake mana anawajua kwamba hamuwezi kumsaidia mtoto wake akimuacha. Mna matatizo mpaka huyo dada yenu anajua.
 
Tanzania inadaiwa Trilion 50+ na hawaja tishia kujiuwa!

Sasa huyo dada yako anadaiwa Milion 10 anachanganikiwa kiasi hicho!

Magufuli kabana hadi raia haijielewi

Isitoshe. Hilo deni la benki watakuwa wanamkata direct kwenye mshahara. Issue ni vi madeni vya mtaani.
 
Huu ndio undugu,kumpenda ndugu yako hta kama anashida nyingi au tabia mbaya kias gani
Hawana upendo hao ndio mana dada yao pamoja na matatizo aliyonayo anataka afe na mtoto wake anajua akimuacha atapata shida. Nawashauri wabadilike.
 
😛. dawa yake ndogooo sana,/ kasi ya maisha ya wengine inamchanganya,then hapati mshauri wa karibu, ANGENIFAA KWELI.
 
Habari zenu wakuu. Mimi ni binti wa miaka 25 ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano. Nina dada yangu ambaye ni wa tatu kuzaliwa, ndugu huyu ananifanya niishi kwa wasi wasi na huzuni kuu huku nilipo, kwa sababu mara kwa mara amekuwa akitishia kujiua yeye na kumuua mtoto wake.
Sabababu kubwa ya kufanya hivyo ni madeni. Dada yangu huyu mnamo mwezi wa nane alichukua mkopo katika bank fulani wa shilingi milion kumi ambao ataulipa ndani ya miaka mitano. Cha kusikitisha hakufanyia kitu cha maana sana zaidi ya kubadili vitu vyote vya ndani, akanunua viwanja viwili na nyingine akalewea pombe na kuwapa ofa marafiki zake.
Hadi imefika mwezi wa tisa mkopo wote ukawa umeisha, akawa mtu wa kuomba omba. Hapo ndipo akaamua kukopa mitaani kwa watu wanaokopesha fedha kwa riba. Akawa anadaiwa kama laki nne. Sasa ikawa akipata mshahara analewea wote na akilewa anamtukana mwenye nyumba na kutishia kumuua mtoto wake na kujiua yeye mwenyewe(mtoto ana miaka kumi).
Kutokana na hali hiyo mwenye nyumba akamsitishia mkataba na kumrudishia hela iliyobakia na akamwambia ahame. Kweli dada yangu alihama lakini hakuwa na pa kwenda hivyo vyombo vyake akawekeza kwa majirani. Sasa akawa mtu wa kutangatanga mara alale barazani mara nje na kazini akawa haendi. Wakati huo mtoto wake kamuwekeza kwa majirani.
Habari zote za yeye kufukuzwa nilipigiwa simu na msamaria mwema mmoja ambae alifanikiwa kuchukua namba yangu wakati dada yangu akiwa amelewa.
Baada ya kupata taarifa hizo niliamua kuwapigia ndugu zangu wakubwa na kuwaeleza. Hakuna aliejali majanga anayopitia dada yangu huyo kila mtu yupo bize na maisha yake madai yao ni kuwa kama huyo dadangu kaona pombe inamsaidia basi aendelee nayo.
Sasa wiki iliyopita huyu dada yangu alienda kwa dada yetu mkubwa ambae kafanikiwa kujenga maeneo ya tabata. Alipofika huko alileta vurugu sana na akatishia kuichoma moto nyumba.
Kutokana na matendo yake ndugu wamemsusa kabisa hakuna anaetaka kujua habari zake. Yaani amekuwa mpweke sana hana msaada , kwa kifupi hakuna anayemjali. Kadiri siku zinavyozidi kwenda roho ya kutamani kujiua naona imemkolea.
Leo hii nimeongea nae kwa simu akasema kuwa niende nikachukue vitu vyake vyote vya ndani kwa sababu hataki mtu yeyote avichukue atakapokufa. Sio siri roho inaniuma sana nimejaribu kuongea nae mara kwa mara kuwa asiyakimbie matatizo kwa kukikaribisha kifo lakini hanielewi. Nikiwaeleza ndugu wakubwa wananijibu mwache afe ila mtoto amuache kwa kweli nazidi kukata tamaa ya kumuepusha dada yangu huyu katika roho ya mauti.
Namnukuu juu ya kifo alichochagua anasema" NITAMPA MWANANGU SUMU AKIANZA KUTATARIKA/KUHANGAIKA NA MIMI NAKOROGA SUMU NAKUNYWA ILI TUFE PAMOJA. Nampenda sana dada yangu sitaki kumpoteza hata kidogo.
Ndugu zangu wanajamii forum wakubwa kwa wadogo naombeni mnishauri nifanye nini juu ya dada yangu asipate mawazo ya kujiua na kumuua mtoto wake? Mwenzenu chakula hakipiti kooni kwa mawazo[emoji22] [emoji22]

Kwa kuanzia, peleka ripoti polisi haraka sana, halafu peleka ripoti ustawi wa jamii.

Nenda kaongee na Psychiatrist kwenye hospitali yenye wodi ya kuwalaza wenye matatizo ya akili ili mumkamate na kumpeleka hapo azuiliwe kwa muda akipatiwa matibabu ya kitaalam.

Tumuombee kwa Allah amsaidie kumuondoshea na kumuongoza katika njia zenye heri.
 
Habari zenu wakuu. Mimi ni binti wa miaka 25 ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano. Nina dada yangu ambaye ni wa tatu kuzaliwa, ndugu huyu ananifanya niishi kwa wasi wasi na huzuni kuu huku nilipo, kwa sababu mara kwa mara amekuwa akitishia kujiua yeye na kumuua mtoto wake.
Sabababu kubwa ya kufanya hivyo ni madeni. Dada yangu huyu mnamo mwezi wa nane alichukua mkopo katika bank fulani wa shilingi milion kumi ambao ataulipa ndani ya miaka mitano. Cha kusikitisha hakufanyia kitu cha maana sana zaidi ya kubadili vitu vyote vya ndani, akanunua viwanja viwili na nyingine akalewea pombe na kuwapa ofa marafiki zake.
Hadi imefika mwezi wa tisa mkopo wote ukawa umeisha, akawa mtu wa kuomba omba. Hapo ndipo akaamua kukopa mitaani kwa watu wanaokopesha fedha kwa riba. Akawa anadaiwa kama laki nne. Sasa ikawa akipata mshahara analewea wote na akilewa anamtukana mwenye nyumba na kutishia kumuua mtoto wake na kujiua yeye mwenyewe(mtoto ana miaka kumi).
Kutokana na hali hiyo mwenye nyumba akamsitishia mkataba na kumrudishia hela iliyobakia na akamwambia ahame. Kweli dada yangu alihama lakini hakuwa na pa kwenda hivyo vyombo vyake akawekeza kwa majirani. Sasa akawa mtu wa kutangatanga mara alale barazani mara nje na kazini akawa haendi. Wakati huo mtoto wake kamuwekeza kwa majirani.
Habari zote za yeye kufukuzwa nilipigiwa simu na msamaria mwema mmoja ambae alifanikiwa kuchukua namba yangu wakati dada yangu akiwa amelewa.
Baada ya kupata taarifa hizo niliamua kuwapigia ndugu zangu wakubwa na kuwaeleza. Hakuna aliejali majanga anayopitia dada yangu huyo kila mtu yupo bize na maisha yake madai yao ni kuwa kama huyo dadangu kaona pombe inamsaidia basi aendelee nayo.
Sasa wiki iliyopita huyu dada yangu alienda kwa dada yetu mkubwa ambae kafanikiwa kujenga maeneo ya tabata. Alipofika huko alileta vurugu sana na akatishia kuichoma moto nyumba.
Kutokana na matendo yake ndugu wamemsusa kabisa hakuna anaetaka kujua habari zake. Yaani amekuwa mpweke sana hana msaada , kwa kifupi hakuna anayemjali. Kadiri siku zinavyozidi kwenda roho ya kutamani kujiua naona imemkolea.
Leo hii nimeongea nae kwa simu akasema kuwa niende nikachukue vitu vyake vyote vya ndani kwa sababu hataki mtu yeyote avichukue atakapokufa. Sio siri roho inaniuma sana nimejaribu kuongea nae mara kwa mara kuwa asiyakimbie matatizo kwa kukikaribisha kifo lakini hanielewi. Nikiwaeleza ndugu wakubwa wananijibu mwache afe ila mtoto amuache kwa kweli nazidi kukata tamaa ya kumuepusha dada yangu huyu katika roho ya mauti.
Namnukuu juu ya kifo alichochagua anasema" NITAMPA MWANANGU SUMU AKIANZA KUTATARIKA/KUHANGAIKA NA MIMI NAKOROGA SUMU NAKUNYWA ILI TUFE PAMOJA. Nampenda sana dada yangu sitaki kumpoteza hata kidogo.
Ndugu zangu wanajamii forum wakubwa kwa wadogo naombeni mnishauri nifanye nini juu ya dada yangu asipate mawazo ya kujiua na kumuua mtoto wake? Mwenzenu chakula hakipiti kooni kwa mawazo[emoji22] [emoji22]
Ushauri mchukueni huyo mtoto make naye mumpe huduma. Yeye mwacheni maana yaonesha hana akili timamu, siku zikirudi atajua tu cha kufanya. Maana hii hadithi kama sio ya kutunga, kazi ipo
 
Back
Top Bottom