huyo dada yako anakaribisha matatizo makubwa sana katika maisha yake mapenzi ni kama upofu na huyo dada yako ameshapofuka hawezi kuona tena, hizo ni tamaa tu anazoonyesha kwa nn ukubali zawadi kama hizo za muda mfupi. Matokeo yake yatakuwa hivi (naandika kwa kuwa nimeshayaona kwa watu haya):
1.wataanza uhusiano au wameshaanza,
2. kuna siku mume wake atagundua na kumwacha tena itajulikana ofisini kote na sababu,
3. baada ya kuachwa huyo dada yako ataaibika sana ofisini kwake na bosi pia na hiyo habari itatapakaa na kumchafua sana bosi,
4. dada yako atakuwa hana pa kukimbilia na kumtaka bosi amchukue jumla,
5. kwa kuwa mambo yameshaharibika bosi nae ataanza kumkwepa
6. dada yako atamjia juu kwa nini amemharibia maisha yake
7. bosi atakasirika na kuamua kumfukuza kazi ili aponye kibarua chake na kuzima hiyo kashfa
8. dada yako atachanganyikiwa sana na anaweza hata kujiua na kuleta simanzi kwako wewe na familia nzima kwa jumla
kwa hali hiyo naomba umwambie huyo dada yako ahamue moja kuacha kazi au kumwambia ukweli mme wake na kumuonya bosi wake otherwise mnakaribisha msiba wa dada yako na matatizo makubwa sana kwa watoto wake
hizo zawadi na hilo gari hakika litamletea matatizo makubwa mara 1000 ya hizo zawadi na atatamani hazitapike kabisa
Pesa zinatafutwa jamani lakini si utu tufanye kazi kwa bidii maisha hayana short cut,